Wanaume wenye ugonjwa wa Tezi dume vijijini wanakosa matibabu ya ugonjwa huo kutokana na umaskini

Bushmamy

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2019
Posts
11,208
Reaction score
20,517
Miaka hii miwili nilikuwa maeneo ya vijijini basi katika zunguka yangu huko nilikutana na wazee kadhaa huko wakiugulia huu ugonjwa uitwao Tezi dume.

Baadhi ya wazee niliongea nao Waliniambia ya kuwa wana tatizo Hilo Kwa muda mrefu ila ni kuwa hawana fedha Kwa ajili ya kwenda kufanya upasuaji. Na waliniuliza kuwa kama serikali Inatoa msaada wa kimatibabu Kwa watu kama wao ambao hawana uwezo wa kujitibia.

Ukweli ni kuwa umaskini umesababisha wananchi wengi sana katika hizi nchi zetu kufariki Dunia huku wakijiona na hata wanafamilia wakishuhudia.

Unakaribishwa kutoa maoni Yako hapa Nini kifanyike hao wazee au watu wasiojiweza waweze kupatiwa matibabu kuokoa maisha yao.
 
Serikali huku vijijini haina msaada wowote ule. Nawashauri unapofikia umri wa miaka 35+ anza kutumia nyanya ntole na kunywa supu yake, tezi dume utaisikia kwa wengine.
 
Nyanya ntole ndio nyanya gani mkuu??
 
Miaka hii miwili nilikuwa maeneo ya vijijini basi katika zunguka yangu huko nilikutana na wazee kadhaa huko wakiugulia huu ugonjwa uitwao Tezi dume.

Baadhi ya wazee niliongea nao Waliniambia ya kuwa wana tatizo Hilo Kwa muda mrefu ila ni kuwa hawana fedha Kwa ajili ya kwenda kufanya upasuaji. Na waliniuliza kuwa kama serikali Inatoa msaada wa kimatibabu Kwa watu kama wao ambao hawana uwezo wa kujitibia.

Ukweli ni kuwa umaskini umesababisha wananchi wengi sana katika hizi nchi zetu kufariki Dunia huku wakijiona na hata wanafamilia wakishuhudia.

Unakaribishwa kutoa maoni Yako hapa Nini kifanyike hao wazee au watu wasiojiweza waweze kupatiwa matibabu kuokoa maisha yao.
Mkuu acha kabisa HALI NI TETE

Na mbaya zaidi hali ikiwa mbaya zaidi mgonjwa anashindwa hata kupata haja ndogo ndio ndugu wanajipapatua kumpeleka Hospitali kubwa ambapo tayari tezi dume imekua imekwisha develop cancer…… too late
 
Back
Top Bottom