Bush Viper
Member
- Nov 19, 2018
- 9
- 55
Rafiki yangu leo amekuja kwangu na kunikopa laki moja, nikampatia kama kawaida yetu ya kusaidiana. Lakini cha ajabu ni kwamba baada ya dakika kadhaa akarudi na kunieleza kuwa alikuwa anataka aogezee kwa laki tano hili ifike laki sita aliyoombwa na bimdada atengeneze gari.
Nikabaki nimeshtuka! Jamaa hajaoa, wala si wachumba, lakini yupo tayari kutoa pesa nyingi kiasi hicho, na mshahara wake ni laki nne na elfu arobaini tu. Nimejaribu kumshauri kwa upole, lakini ukweli nimesikitika.
Hii imenifanya niwaulize wanaume wenzangu, hivi huwa mnapewa nini mpaka mnahonga kiasi hiki? Au mimi ndio sijawahi kupata penzi la kunifanya niweweseke? 😂 Mimi binafsi sijatoa hela ila nimeumia, maana nimeamini kwamba wanaume wengi hatuendelei kwa sababu ya mapenzi.
Nimebaki najiuliza kuwa

- Je, ni busara kutoa fedha nyingi kwa mwenza ambaye huna uhakika wa hatma ya uhusiano?
- Je, kuna njia bora za kuonyesha mapenzi bila kuhatarisha hali ya kifedha?
- na huwa mnapewa nini hadi akili zinawaruka.