Wanaume wenzangu, huwa mnapewa nini hadi mnahonga pesa ambazo zipo juu ya uwezo wenu?

Wanaume wenzangu, huwa mnapewa nini hadi mnahonga pesa ambazo zipo juu ya uwezo wenu?

Mkuu huwez tenganisha pesa na mapenz

Ukimpata mdada anae kutumikia vzr utafungua pochi bila kuambiwa

Hawa single mum wanao kaa mbali na watoto wao ndio Hatari kbsa,

Kwakuw bado nipo kwenye majonz baada ya mkewangu kuiingilia kati na kuvunja penzi langu huyu dada acha niendelee kusema
#iwillBefine#
 
Rafiki yangu leo amekuja kwangu na kunikopa laki moja, nikampatia kama kawaida yetu ya kusaidiana. Lakini cha ajabu ni kwamba baada ya dakika kadhaa akarudi na kunieleza kuwa alikuwa anataka aogezee kwa laki tano hili ifike laki sita aliyoombwa na bimdada atengeneze gari.

Nikabaki nimeshtuka! Jamaa hajaoa, wala si wachumba, lakini yupo tayari kutoa pesa nyingi kiasi hicho, na mshahara wake ni laki nne na elfu arobaini tu. Nimejaribu kumshauri kwa upole, lakini ukweli nimesikitika.

Hii imenifanya niwaulize wanaume wenzangu, hivi huwa mnapewa nini mpaka mnahonga kiasi hiki? Au mimi ndio sijawahi kupata penzi la kunifanya niweweseke? 😂 Mimi binafsi sijatoa hela ila nimeumia, maana nimeamini kwamba wanaume wengi hatuendelei kwa sababu ya mapenzi.

Nimebaki najiuliza kuwa
  • Je, ni busara kutoa fedha nyingi kwa mwenza ambaye huna uhakika wa hatma ya uhusiano?
  • Je, kuna njia bora za kuonyesha mapenzi bila kuhatarisha hali ya kifedha?
  • na huwa mnapewa nini hadi akili zinawaruka.
Huyo Jamaa yako akishafikisha 40 ndio atakuja kuhangaika na slgan ya Kataa Noda kwa ujinga wake.

Wakati huo kashachoka kachakaa......ana kazi ya kulaumu ccm ni wezi
 
Siku ukipewa hii ndo utajua
downloadfile-58.jpg
style ya "bandari imeuzwa"
 
Huenda wana plan na hiyo gari iwaingizie kipato ...🤔🤔

Ila binafsi siwezi tumia pesa zaidi ya ninayoingiza unless Dharura inayohitaji chukuliwa hatua haraka sana ..🤔🤔
 
Back
Top Bottom