Nadhani hapo kuna dhana kuhusu matumizi ya muda. Fikra kichwani ni matumizi mabovu ya muda. Ndio kinachowatesa watu. Lakini hebu tuangalie haya.
Una kazi umemaliza kazi saa 11. U akimbia kwenda kwenye kaduka kako, kanafunga saa 4 usiku. Unaaza kupiga hesabu zi balance saa nzima. Je, utarudi saa 2 usiku?
Una kazi, na ka elimu kidogo, unataka kujiendeleza, unamaliza kazi saa 11 unakimbia chuo, mnamaliza saa 4 usiku. Je, utalala saa 6 usiku?
Una biashara ya baa, unaisimamia mwenyewe. Mpaka wateja waishe saa 6 usiku, je, utalala saa ngapi.
Ninajua kabisa wafanyabiashara wakubwa wanatumia masaa 18 na zaidi macho. Hayo mambo ya kulala saa ngapi ni wale watakaozeeka walalahoi.
Asanteni.