Wanavyuo, kwanini huwa mnaona noma kutaja majumbani kwenu?

Kuna lilojificha hapo?Dar kifursa, kimaendeleo,vyuo vingi pia vipo dar nk, dar imepiga hatua ukilinganisha na mikoa mingine,pamekuwa sehemu ya watu kupakimbilia na kuonekana ukiishi dar wewe ni mjanja,ni vyema sana serikali ingepanua wigo wa uwekezaji katika mikoa mingine, offisi za wizara mbalimbaili sisogezwe kwenye mikoa mbalimbali respectively na shughuli za wizara husika,na pia watumie system za decentralised sio centralised kwamba activities nyingi katika taasisi za serikali eg G. P. S. A ambapo depot zipo mikoani zifanyike huko huko mikoani kupunguza ulimbukeni wa kila kitu kifanyike dar.kwa hizi factors zitaondoa hiyo fallacy kwa kila mtu kujinadi anatokea dar na kupenda makwao,
 
But sio sababu ya mtu kupakana kwao
 
Mweh somo, sasa tusipoenda daslamu itakuwaje? Inamaana hatujawahi kuishi Tanzania jamani.
 
Taratibu jamani ambao hatujafika dar kawaida yetu kujionyesha tunakufahamu huko dar hatakama tunatokea mbeya, alafu hii ishu sio wanachuo tu hadi kwa baadhi ya watu wazima na nchi za jirani zetu mfano mzuri kama wiki mbili zilizopita nilienda hapa kwa wabwezi(malawi) nilikutana na majanki wakaniuliza natokea Tz mkoa gani nikawaambia mi jirani yao hapa karibu. Basi kila wakati wananiulizia ishu za dar ambako mie mwenyewe sijawahi fika, wabwezi wanakukubali sana dar na kwa matajiri wao lazima kwanza uwe umefika johnnesberg halafu dar wewe ndio tajiri mjanja
 
arusha nan atakuhonga 100,000
Mwanza nani atakupa lift ya alteza,mark x, subaru,.vitz
mikoani nan utamvalia milegezo.na.vimini zaidi ya kukuona mshamba
 
Wengi wanakuwa hawajawahi kufika dar wakiwa chuoni ndio wanapata uwezo wa kutembelea jiji
 
Mi huwa nacheka sana mtu ana lafudhi ya kihaya/kichagga bado atakwambia kwao dar na kazaliwa dar.....dah,hatari sana.
 
mimi nawaambiaga kwetu kigoma ila wanakuona mshamba balaa,

unakuta mtu anakwambia na anajisifia mm kwetu hapa hapa nimezaliwa hapa hapa, nikitzama maisha yake na yangu levo sawa sasa najiuliza MZIMA KWELI HUYU.KIJANA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…