Wanavyuo, kwanini huwa mnaona noma kutaja majumbani kwenu?

Wanavyuo, kwanini huwa mnaona noma kutaja majumbani kwenu?

Good morning....
Enzi hizo naanza chuo nlikua nashangaa kila mwana chuo anasema kwao dar, mtu anaongea lafudhi yani kisukuma cha ndani kabisa huko mwamashimba ila ukimuuliza kwao anasema dar tena anajitahidi na kumix kidogo lafudhi ya dar mi naiita kuvunja nazi..... Hiyo mixer ya kisukuma plus kuvunja nazi sasa mweh!!!

Juzi nlikutana na masista duu wa chuo, tunafamiana wakawa wananiaga wanaenda likizo, wa kwanza nikamuuliza home wapi, akajibu naenda dar af kesho kutwa narudi, nikamuuliza kwanini unarudi soon akasema narudi afu ndo naenda home Arusha. Dar kunani huko nami nije? Mtu anaona noma kusema arusha kisa dar?

Wa pili sasa lol nae nikamtel safari njema home wapi, akajibu napita dar kwanza nisipoenda itakua lawama, Ha ha nkauliza tena so home wapi nkaona sura yake imenyong'onyea, imejaa wasiwasi, kwa sauti ya chini akajibu nikitoka dar naenda kigoma kwa mama nilijizuia tu kucheka ila kweli ilinichekesha sana.

Jamani dar kuna nini huko? Wahenga walisema mkataa kwao mtumwa. Wasomi tabia mbaya hiyo kwani ukisema kwenu mwamashimba kuna ubaya gani?
wanavyuo nawatakia likizo njema, BILA SHAKA WOTE MPO NDANI YA SHABIBY KWENDA DAR HAKUNA ALIEPANDA SARATOGA YA KIGOMA LOL
Mbona mimi ni msukuma wa misungwi niko pale nyakato mwanza na huku chuo huniita mwamasu lakin poa tu,mkataa kwao ni mtumwa,dar tunapita tu
 
But sio sababu ya mtu kupakana kwao
Itafute sababu sasa ulete kama haitabaki kuwa dar ndo city iliondelea tz nzima, hiyo tu inajenga notion ya kila mtu kuona kutokea dar ndo ujanja,fanya tafiti my dia,mikoa mingine ipo nyuma sana kimaendeleo na haimjengi mtu kupenda alipotokea.
 
Itafute sababu sasa ulete kama haitabaki kuwa dar ndo city iliondelea tz nzima, hiyo tu inajenga notion ya kila mtu kuona kutokea dar ndo ujanja,fanya tafiti my dia,mikoa mingine ipo nyuma sana kimaendeleo na haimjengi mtu kupenda alipotokea.
Kwahiyo jirani yako akiwa na mjengo mkali kapaki ndinga kali ndo utawaonesha kuwa pale ndo kwenu? Ulimbukeni
 
Kwahiyo jirani yako akiwa na mjengo mkali kapaki ndinga kali ndo utawaonesha kuwa pale ndo kwenu? Ulimbukeni
Yes ma dia kwa hiyo Umeona eeehhh, wenye dhana hiyo kweli ni ulimbukeni na ni utoto,na ndo maana nilisema mwanzano kwamba yote hiyo ni fallacy,lakini chanzo cha haya yote itabaki kuwa kwenye point yangu ya hapo juu.
 
Kwa sisi tunaoishi vijijini kama hujafika Dsm unaonekana wewe ni mshamba hatari. Ndio maana rikizo watoto wanapenda kwenda Dar
 
hahahahaaaaa.....yan mbavu sina rafiki angu mmoja kila likizo anaenda dar kwanza kisha ndo arud chuo kubadili mavazi na mitindo mingine ndo aende kwao bariadi
Hahahaha dah umetaja nyumbani kwetu kabisa.....They call it bariadi,we call it home.... Simiyu Express
 
Swali la nyongeza, kwa nn waTz wengi wakiwa nje ya Africa hujitambulisha wanatokea Kenya? Thats my observation
 
Back
Top Bottom