Good morning....
Enzi hizo naanza chuo nlikua nashangaa kila mwana chuo anasema kwao dar, mtu anaongea lafudhi yani kisukuma cha ndani kabisa huko mwamashimba ila ukimuuliza kwao anasema dar tena anajitahidi na kumix kidogo lafudhi ya dar mi naiita kuvunja nazi..... Hiyo mixer ya kisukuma plus kuvunja nazi sasa mweh!!!
Juzi nlikutana na masista duu wa chuo, tunafamiana wakawa wananiaga wanaenda likizo, wa kwanza nikamuuliza home wapi, akajibu naenda dar af kesho kutwa narudi, nikamuuliza kwanini unarudi soon akasema narudi afu ndo naenda home Arusha. Dar kunani huko nami nije? Mtu anaona noma kusema arusha kisa dar?
Wa pili sasa lol nae nikamtel safari njema home wapi, akajibu napita dar kwanza nisipoenda itakua lawama, Ha ha nkauliza tena so home wapi nkaona sura yake imenyong'onyea, imejaa wasiwasi, kwa sauti ya chini akajibu nikitoka dar naenda kigoma kwa mama nilijizuia tu kucheka ila kweli ilinichekesha sana.
Jamani dar kuna nini huko? Wahenga walisema mkataa kwao mtumwa. Wasomi tabia mbaya hiyo kwani ukisema kwenu mwamashimba kuna ubaya gani?
wanavyuo nawatakia likizo njema, BILA SHAKA WOTE MPO NDANI YA SHABIBY KWENDA DAR HAKUNA ALIEPANDA SARATOGA YA KIGOMA LOL