Sijawahi amini km shoga anatongoza mwanaume straight, km wapo kweli bas ni wale waliojichokea na maisha, wazee waliokosa soko, na wale wasiokua na mvuto, akili wala ufahamu.
Shoga smart na anayejitambua, anakua buzzy na maisha yake binafsi ktk kujipatia mahitaji yake kuweza ku survive, kwa njia halali kabisaa, tena yeye ndo anatongozwa kwa heshima na taratibu zote za utongozaji, huduma, na nguzo zote za mapenzi anapatiwa kwa ufanisi zaidi.
Kuhusu kupata mwenza wa kuridhishana nae hisia za mwili, anapata kutoka ktk Gayism site, tena anakua na Basha halisi haswaah sio hawa wavamiaji, yaan shoga anamtongoza straight eti kisa mvuto, kwan mbona mabasha wengi wapo wenye mvuto wa kuwavutia hao mashoga,
Jambo liliopo ni kuwa hao straight wenyewe ndio wanawa shobokeaa na kuwaonesha ishara za kuwakubali hao mashoga, ndipo na wao wanafungukia ukweli,
Straight wao wenyewe wanafukunyua na kulike hata ku comment site za gays why wasitongozwe? Maana wanajua na wao ni wadau.
Hapa nchini kwetu kuna unafiki sana tena mno, jamii inapinga suala la ushoga, ila ndio jambo ambalo limekua na linazidi kukua siku hadi siku ndani ya jamii zetu. Ina maana pingamizi halifanywi ipasavyo au? Na km kuna vikwazo bas viondolewe hivyo vikwazo ili tatizo litatulike sio kupiga kelele na kutoa hoja za pingamizi tena zisizo na ukweli wala uhalisia, huku suala likizidi kuenea kwa kasi pindi linavozidi kujadiliwa.
Ushoga haujaanza leo wala jana, ulikuwepo tangu enzi na enzi, wala hakuna ajabu yeyote.
Ushoga ni hisia za mtu zilizoko ndani yake, hivyo haipaswi kuzuiliwa wala kupingwa, kwani yeye ndiye mwenye dhamana ya kumanage hilo.
Kama Taifa ifike wakati tuwe bussy kujadili masuala ya msingi na ya maendeleo kwa ujumla, kwa mustakabali wa nchi yetu,
Na sio kujadili au kuzungumzuia masuala ya mtu binafsi tena mwenye uhuru wa kufanya vile apendavyo, ni upotevu wa muda tu.
.............