Melki Wamatukio
JF-Expert Member
- May 3, 2022
- 6,156
- 10,974
Alikwama katika harakati zake za hapa na pale, hivyo akaniomba nimpatie elfu thelathini asogezee siku kisha kuahidi kunirudishia siku iliyofuata.
Cha ajabu siku iliyofuata akanilia buyu, kisha kesho yake! Nikaona kama nikiendelea kuwa kimya nitaisubiri mpaka ukamilifu wa dahali. Nikaona nimtingie ghetoni kwake. Baada ya kufika, nikawakuta nje yeye pamoja na sponsor wake, nikashuhudia akikabidhiwa minoti ya kutosha myekundu, nikavunga somewhere, baada ya lile jitu lenye miraba minne kuondoka nikamfuata binti na kumkumbusha.
Cha ajabu ananambia, "kwani wewe hujawahi toa sadaka?". Katika harakati za kubishana nae akanambia hana hela. Nikamwambia nimeshuhudia ukikabidhiwa minoti still anakataa. Nikatikisa kichwa kwa majonzi nikaondoka. Baada ya masaa mawili (jana saa 1 jioni) kamtuma mtoto aniletee hiyo 30k. Mida ya saa tatu nikakutana nae dukani, kumsemesha japo kwa salamu hajajibu chochote kitu, kabaki amenuna tu
Funzo: Usimkopeshe mwanamke pesa ambayo unamalengo nayo