Wanawake hawapendani, Una deal vipi na vita ya kimya kimya ya mke, dada zako na mama yako?

Wanawake hawapendani, Una deal vipi na vita ya kimya kimya ya mke, dada zako na mama yako?

G Tank

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2023
Posts
2,297
Reaction score
8,760
Ni vita ambayo wao hudhani hatujui ipo lakini huwa tunajifanya washamba mambo yaende, kwa wanaume wengine huwa hawajui haya mambo wanaishia kuharibu.

Wanaume wengi wanavuta jiko pale mambo yanapoanza kukaa sawa panapokuwa na chanzo cha kipato, nguvu ya pesa inakuwepo unaanza kusaidia nyumbani na ndugu wengine.

Upande wa wanaume (baba, kaka zako, n.k) hawana tatizo, hata kaka zetu waliotutangulia kuoa wakipunguza msaada tunajua wanayopitia, suluhisho ni sisi wenyewe kuongeza juhudi kupambania tonge. shida inakuja kwa mama, dada zako na ndugu wengine wa kike !!

huwa kuna wivu wa wanawake unaanza, kina mama na dada wanaona mke anaingilia kati kwenye vitu ilivyobidi wavipate wao, hata kama hujapunguza kiasi na pengine umeongeza kuwatumia pesa huwa wanadhani mke anafaidi zaidi, inaweza tokea kwenu pesa zipo nyingi sana kina dada / mama hawana shida ya pesa lakini bado kunaweza kuwa na wivu kwamba mke analipata penzi lako kuzidi wao wanavyopendwa au walivyopendwa na waume zao.

Hata saa mbovu kuna muda ina faida, hii ishu kwa upande mwengine huwa inawanyoosha vizuri wale wake wasumbufu, yani mke awe mjuaji akutane na mama mke / mawifi konki zaidi, mambo huwa ni faya 😂

Hii ishu kitamaduni niliwahi kusikia ina elimu yake kwa wanawake wa Pwani lakini sikuwahi sikia kwa wanaume, Tuelimishane hapa.
 

Attachments

  • 1725383293365.png
    1725383293365.png
    112.4 KB · Views: 7
Deal na ndugu zako kimya kimya asijue mkeo ila deal na ndugu zake kwa kumshirikisha ataona mzani umeegemea kwake mtakuwa na furaha
Wanawake complicated sana, Kuna ile tabia ya kupenda kuringishiana, Umempa mama au dada msaada kimya kimya yeye anaweka status na lengo ni ujumbe ufike kwa mke wako,

Ila ni mbinu nzuri, tuliambiwa tuishi nao kwa akili, ukitumia akili unaweza kufanikisha iwe utakavyo.
 
Cheka nao wote, jifunze kuyapuuza mengi wanayokwambia kuwahusu hasa yakilenga kuleta ugomvi.

Lakini usifanye wakajua unayapuuza, just sikiliza kwa makini wanachokwambia then kwenye utekelezaji ndio uwe mzito.

Wacha muda upite ili nayo yapite huku ukiendelea kudumisha amani kati yao, hata kama watakuwa hawaelewani.
 
Back
Top Bottom