Wanawake hawapendani, Una deal vipi na vita ya kimya kimya ya mke, dada zako na mama yako?

🙏
 
Attachments

  • Screenshot_20240903-205736.png
    Screenshot_20240903-205736.png
    101.3 KB · Views: 4
shida ni watu kuishi as if they are in competition na watu wengine, kila mtu ashinde mechi zake, kinachoumiza zaidi tusielewane saa zingine hata nyie mnachangia mtu umeoa lakini majukumu ya dada yako aliyeachika kwenye ndoa na watoto watatu unataka majukumu uyabebe wewe ukiambiwa unakaza shingo kwa nn tusigombane,??

ndugu za mume wengi huhisi kaka yao akishaoa mambo mengi atakua anafaidi mka mwana kumbe watu wanavumiliana tu
Sasa utaki nimsaidie wifi ako?
 
Kuna watu wame tengana sabb hiyo
Ndugu wa jamaa wamekuja juu wakamtafutia chuma mpya tena yenye pesa nyumba ikauzwa
mimi ndio wasijaribu mana nitahakikisha kaka yao anabakia kama tulivyokutana na tufungiane tu vioo kwan sh ngap
 
Jamaa ame kubaliana na aliye kuwa mkewe jumba liuzwe kiroho safi
Ndugu zake wamemtafutia chuma kipya
 
Kuolewa sio kuwa na tabia nzuri ni bahati tu ya mtu tunao watu mtaani wameolewa lkn hawajiheshimu mtaani lkn wapo kwenye ndoa na wapo wanaojiheshimu hawana ndoa,alafu punguza ukali wa maneno hao unaoita mapaka shume unaweza na wewe ukawazaa
Ukiwa na dada ambaye HAOLEKI kwa tabia mbaya, Nina maana ya haya mapaka shume yaliyozalishwa ovyo, yasiyopitwa na umbea usiruhusu mkeo awe na mawasiliano naye.
 
Ni vita ambayo wao hudhani hatujui ipo lakini huwa tunajifanya washamba mambo yaende, kwa wanaume wengine huwa hawajui haya mambo wanaishia kuharibu.

Wanaume wengi wanavuta jiko pale mambo yanapoanza kukaa sawa panapokuwa na chanzo cha kipato, nguvu ya pesa inakuwepo unaanza kusaidia nyumbani na ndugu wengine.

Upande wa wanaume (baba, kaka zako, n.k) hawana tatizo, hata kaka zetu waliotutangulia kuoa wakipunguza msaada tunajua wanayopitia, suluhisho ni sisi wenyewe kuongeza juhudi kupambania tonge. shida inakuja kwa mama, dada zako na ndugu wengine wa kike !!

huwa kuna wivu wa wanawake unaanza, kina mama na dada wanaona mke anaingilia kati kwenye vitu ilivyobidi wavipate wao, hata kama hujapunguza kiasi na pengine umeongeza kuwatumia pesa huwa wanadhani mke anafaidi zaidi, inaweza tokea kwenu pesa zipo nyingi sana kina dada / mama hawana shida ya pesa lakini bado kunaweza kuwa na wivu kwamba mke analipata penzi lako kuzidi wao wanavyopendwa au walivyopendwa na waume zao.

Hata saa mbovu kuna muda ina faida, hii ishu kwa upande mwengine huwa inawanyoosha vizuri wale wake wasumbufu, yani mke awe mjuaji akutane na mama mke / mawifi konki zaidi, mambo huwa ni faya 😂

Hii ishu kitamaduni niliwahi kusikia ina elimu yake kwa wanawake wa Pwani lakini sikuwahi sikia kwa wanaume, Tuelimishane hapa.
Ugomvi wa wanawake sio kipato au maslahi tu bali hii ni asili yao kutompenda mwanamke ngeni kuletwa au kuolewa na kaka au ntoto wao.
Haya nimeyashuhudia hadi kwa baadhi ya jamii ya kizungu.
Mama mkwe na binti zake hawampendi mke wa kijana=kaka yao
 
Ni vita ambayo wao hudhani hatujui ipo lakini huwa tunajifanya washamba mambo yaende, kwa wanaume wengine huwa hawajui haya mambo wanaishia kuharibu.

Wanaume wengi wanavuta jiko pale mambo yanapoanza kukaa sawa panapokuwa na chanzo cha kipato, nguvu ya pesa inakuwepo unaanza kusaidia nyumbani na ndugu wengine.

Upande wa wanaume (baba, kaka zako, n.k) hawana tatizo, hata kaka zetu waliotutangulia kuoa wakipunguza msaada tunajua wanayopitia, suluhisho ni sisi wenyewe kuongeza juhudi kupambania tonge. shida inakuja kwa mama, dada zako na ndugu wengine wa kike !!

huwa kuna wivu wa wanawake unaanza, kina mama na dada wanaona mke anaingilia kati kwenye vitu ilivyobidi wavipate wao, hata kama hujapunguza kiasi na pengine umeongeza kuwatumia pesa huwa wanadhani mke anafaidi zaidi, inaweza tokea kwenu pesa zipo nyingi sana kina dada / mama hawana shida ya pesa lakini bado kunaweza kuwa na wivu kwamba mke analipata penzi lako kuzidi wao wanavyopendwa au walivyopendwa na waume zao.

Hata saa mbovu kuna muda ina faida, hii ishu kwa upande mwengine huwa inawanyoosha vizuri wale wake wasumbufu, yani mke awe mjuaji akutane na mama mke / mawifi konki zaidi, mambo huwa ni faya 😂

Hii ishu kitamaduni niliwahi kusikia ina elimu yake kwa wanawake wa Pwani lakini sikuwahi sikia kwa wanaume, Tuelimishane hapa.
Hayo mambo madogo, chamsingi maswala ya wanawake achana nayo na hata huyo mkeo akiomba support achana nae, dada zako wakiomba support achana nao na hata mama yako pia, wewe endelea na mambo yako ya msingi mpaka watakapo taka usuluhishi wao wenyewe
 
Back
Top Bottom