Vien
JF-Expert Member
- Mar 6, 2020
- 8,508
- 15,276
Hawa viumbe, mbali na changamoto zao mbalimbali, wana baadhi ya sifa ambazo kwa kweli zinaweza kuwasaidia sana kimaisha.
Sifa ya kwanza: Wanawake wanajipenda.
Kihisia, kiuchumi na hata kwenye mazingira yanayowazunguka. Mara nyingi wanajipa kipaumbele kwenye mambo yanayowahusu na wanajitahidi kuhakikisha wanakuwa comfortable na maisha yao.
Sifa ya pili: Hawapendi kabisa kubaki na deni.
Chochote utakachomfanyia mwanamke–kiwe kizuri au kibaya–akihisi ana deni kwako, atatafuta namna ya kulipa ili moyo wake utulie.
Mfano mzuri ni pale unapomsaidia mwanamke kutatua changamoto fulani bila hata kuwa na lengo la kuwa naye kimapenzi. Ukimsaidia, akimaliza shida yake, mara nyingi ataanza kutafuta namna ya kukulipa. Anaweza kukuuliza, “Nitakulipa nini?” kwa sababu tu hataki kujisikia ana deni la mtu.
Hata kwenye mambo kama Vikoba, unaona namna ambavyo baadhi yao wanavyopambana kuhakikisha michango na madeni yao yanalipwa kwa wakati. Wanatafuta kila aina ya njia kuhakikisha hawabaki nyuma, kwa sababu kukaa na deni ni kitu kinachowasumbua sana.
Na hapa ndipo ninapoona kuna potential kubwa sana ambayo wanawake wengi hawajaitumia vizuri.
Hii tabia ya kutopenda kuwa na deni, kama wangeielekeza vizuri kwenye kujenga maisha yao, biashara na maendeleo yao, wengi wangefika mbali sana.
Tatizo ni kwamba wakati mwingine wanatumia nguvu kubwa kulipa madeni waliyoyatengeneza wenyewe, huku njia wanazotumia kuyamaliza zikiwa zinawaingiza kwenye matatizo mengine.
Kwa kifupi:
Wanawake hawapendi deni. Wanataka kulipa. Tatizo si kulipa deni – tatizo ni njia wanayochagua kulipa deni
Hii tabia hiyo hiyo ikiwekwa kwenye biashara, uwekezaji na kujenga financial stability, naamini wanawake wengi wangekuwa mbali sana kiuchumi.