Wanawake, hivi kupika vizuri lazima mjaze mafuta kibao kwenye chakula?

mjinga kweli wewe...unatuhukumu wanawake woote kwa kosa la mwanamke wako? Pamabana na 'slay queen' wako huko!
BTW wanawake sio wa kupika tu, pikaga hata wewe siku nyengine
Haaaaaaaa mwambie huyo
 
Mwisho wa siku anaanza ....mbona unapiga kimoja tu....anakuwa amesahau kuwa ni yale mafuta anayozidisha kwenye msosi...
 
Pole sana kwa kupata mwanamke asiyejua kupika, ila ingekuwa busara kama ungemuelimisha huko huko nyumbani kuliko kuja kumuanika huku. Nimejaribu kufikiria hicho kitambi chako kitakuwa cha aina gani kitambi mchongoko, mviringo au kile cha dizain ya utapia mlo [emoji28][emoji28]
 
Kitambi mpakato [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mkuu nimeshaongea nae mno lakini wapiiii
Ataacha leo kesho mafuta kedekede.
Sasa napata hasira kugombana na mke wangu kisa jambo dogo kama hili, yaani ni jambo dogo mno lakini mwenzangu haelewi kabisaaa.
 
Mkeo umeogopa kumwambia unakuja kutuambia sie? Utakuwa hujatatua tatizo na leo ukirudi utakutana na yale yale. Mwambie nini unapenda, simple!
Nimesema mno, mpaka kwa friends zangu naona huu ugonjwa upo karibia sehemu nyingi kwa sasa.
Kama kwako hakuna hili tatizo shukuru Mungu, jaribu kutembea nyumba mbili tatu utapata majibu.
Hapa JF kuna watanzania wengi sana lazima niwambie wajue na wachukue tahadhari, Sharing is caring
 
Hawa wanawake wanao vaa suruali, wanaopaka rangi kucha, mdomo, nywele na uso, hawajui kupika...
Wala hawapendi... Wakubali wakatae ukweli ndo huo
 
Mi naambiwa mara moja nasikiliza. Ajiri mpishi maana ni mkeo huyo ataendelea kuwepo. Mvumilie ndo chaguo lako.
 
Mkeo ndio hajui kupika, unataka kuniambia hata aliyekuzaa au mlezi wako naye alikuwa anajaza mafuta hivyo hivyo? Kumbuka unapotaja wanawake unagusa wengi
 
Mkeo ndio hajui kupika, unataka kuniambia hata aliyekuzaa au mlezi wako naye alikuwa anajaza mafuta hivyo hivyo? Kumbuka unapotaja wanawake unagusa wengi
Acha kuleta weak arguments, wapi nimesema wanawake wote?

We kubali kataa hili ni tatizo jipya limejitokeza kama kwako halipo basi kwa baadhi ya ndugu zako lipo.
Ukinuna sawa ila huo ndio ukweli, kuna wanawake wengine ni hovyo mno.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…