Wanawake jifunzeni mapishi, mnatia aibu

Wanawake jifunzeni mapishi, mnatia aibu

Kuna hawa dada zetu wa migombani wanajua kupika mtori tu wengi wamejificha kwenye kivuli cha mabeki tatu ila mapishi yamewapitia kushoto sana
 
Sio kupika tu hata usafi hawafanyi usafi wao wa Mwili Mimi nilivyogundua hili Jambo niliamua kuchukua kadi kwa dronedrake .

Maana Ukila chakula unaishia kuhrisha ukimgusa Mwili unakula UTI Sugu shida tupu
 
Kwaili kaka umekosea kwaiyo unataka kusema tuwekeane zamu na mwanamke kuhusu kupika na kama sina uwezo wa kuweka house girl inakuaje tena unakuta maali yenyewe wamekomaa millioni 3 hawajapunguza hata mia alafu jitu lenyewe box kupika zero
Kwani kuna ubaya gani mkisaidiana kupika na mkeo/ mpenzi wako?? Mimi najua kupika kila chakula lakini baba watoto wangu huwa ananisaidia kupika ugali kila tukiwa na mlo huo mimi nitaandaa mboga. Sio kwamba siwezi kupika lah bali anaona kuna haja ya kusaidiana. Hakuna ubaya
 
Mwanamke kujua kupika ni muhimu sana kwa ustawi wa afya ya mwili na akili za watoto.

Asipojua kupika kashapoteza sifa ya kuwa mama bora wa watoto wako
Watoto sikuiz wanapikiwa vyakula havina lishe, kila siku mtoto anakula tambi, ubwabwa na sembe kila siku unategemea watakua lini? Unakutana na mtoto unafikiri yuko shule ya msingi kumbe sekondari tena form 4.!!
 
Kwanza: Kama hujamuoa usimpe majukumu ya mke, kupika ikiwemo si ndivyo tulivyojadili katika nyuzi kibao humu?

Pili: Kama ni mke na umemuoa umegundua hajui kupika mrudishe kwao akajifunze.

Tatu: Wanawake wote wa JF tunajua kupika, kwa reference zaidi kaangalie uzi wa vyakula. Hivyo hii mada haituhusu na kwa heshima na taadhima tunaomba muwaambie watu wenu huko huko.

Nne, wanaume wa JF wengi wenu mnafanya Online gender based violence (OGBV) as if hao wanawake zenu hawana jema hata moja.

Mwisho siku nikigundua shemeji yenu yupo humu, ntampa likizo ya miezi 6, agghr wanaume humu mna gubu bwana!
Sana yaani Wana gubu sanaaaaa utadhani wao malaika
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Mtuache tupumue uku, mjifunze kupika, kwingine muache kuomba hela, kule muoshe papuchi TUMECHOKAAAAA [emoji119][emoji119]
Tutapumzika mbunguni wallah yaani kukikucha Kuna jipya
 
Jomba unaoa mke mjenge familia au unaoa mpishi akupikie? Kama mkeo hawezi kupika si umpeleke hata kozi fupi VETA ya mapishi? Au mtafutie mtaalamu amfundishe. Pengine hata wewe mwenyewe umfundishe baadhi ya vitu. Ifike sehemu wanaume tuwe na vifua vya kuficha madhaifu ya wenza wetu. Ishu ya kupika ni ndogo sana kiasi cha kuwaza upumbavu wa kufungua uzi wa kuwaponda wanawake. Ninashauri Mods wawe wanafuta hizi nyuzi za kudhalilisha wanawake. Hapa JF sasa zimezidi.
Umeandika upupu.

Mwanamke mapishi.!!
 
Back
Top Bottom