Wanawake jifunzeni mapishi, mnatia aibu

Wanawake jifunzeni mapishi, mnatia aibu

Mwanamke asiyejua kupika hana sifa ya kuwa mke

Hakuna kitu wanaume tunafurahia kama kula mapishi ya mkeo anayejua kupika
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Mtuache tupumue uku, mjifunze kupika, kwingine muache kuomba hela, kule muoshe papuchi TUMECHOKAAAAA [emoji119][emoji119]
πŸ˜… πŸ˜… πŸ˜…
 
Kwanza: Kama hujamuoa usimpe majukumu ya mke, kupika ikiwemo si ndivyo tulivyojadili katika nyuzi kibao humu?

Pili: Kama ni mke na umemuoa umegundua hajui kupika mrudishe kwao akajifunze.

Tatu: Wanawake wote wa JF tunajua kupika, kwa reference zaidi kaangalie uzi wa vyakula. Hivyo hii mada haituhusu na kwa heshima na taadhima tunaomba muwaambie watu wenu huko huko.

Nne, wanaume wa JF wengi wenu mnafanya Online gender based violence (OGBV) as if hao wanawake zenu hawana jema hata moja.

Mwisho siku nikigundua shemeji yenu yupo humu, ntampa likizo ya miezi 6, agghr wanaume humu mna gubu bwana!
Hawa wamezid kilakitu kutoa kasor Wana gubu hatari, kupika sio kitu Cha ajabu mtu akijifunza tu anaweza
 
mbona ni kitu kidogo sana atajifunza tu....

mambo mengine mnayapa sana umuhimu
As a man, lazima ujue umuhimu wa masaptasapta na maanjumati.!! Sio kila siku unakula vyakula vya ajabu uko kwa mama ntilie unarudi nyumbani unasingizia hujisikii kula kisa mkeo kwenye mapishi ni 0
 
Jomba unaoa mke mjenge familia au unaoa mpishi akupikie? Kama mkeo hawezi kupika si umpeleke hata kozi fupi VETA ya mapishi? Au mtafutie mtaalamu amfundishe. Pengine hata wewe mwenyewe umfundishe baadhi ya vitu.

Ifike sehemu wanaume tuwe na vifua vya kuficha madhaifu ya wenza wetu. Ishu ya kupika ni ndogo sana kiasi cha kuwaza upumbavu wa kufungua uzi wa kuwaponda wanawake. Ninashauri Mods wawe wanafuta hizi nyuzi za kudhalilisha wanawake. Hapa JF sasa zimezidi.
 
Mzee we usijali, kama huna mke we jifunze kupika.

Sijisifii ila katika njia mojawapo natumiaga kuwavutia wanawake waje ghetto ni mapishi yangu.

Tena hawa makucha marefu hawa wakija nawapikiaga wanakula vizur hadi wanajilamba, akimaliza kula lazima alipie chakula.

It's a win-win situation.
 
Back
Top Bottom