Wanawake jitahidini kutoweka wazi shida zenu mapema mnapoingia kwenye penzi jipya

Wanawake jitahidini kutoweka wazi shida zenu mapema mnapoingia kwenye penzi jipya

Tafuta pesa kijana[emoji36] Hivi kweli elfu 80 ni hela ya kunung'unika adi uvunje mahusiano na mtu unayesema unampenda?Je kuhudumia familia utaweza kweli ukiwa nayo maana vya kwenye familia gharama zinatiririkaga automatically mara mtoto aumwe mke ameze mswaki yaani tafrani hahaa.
Kwa hiyo akitafuta ndo aanze kuhonga tu sio!!!?
 
Nakumbuka niliwahi kuingia kwenye mahusiano na binti mmoja wa ki Arusha ambae tulijuana kupitia social media, yeye alikua Arusha na mimi nilikua Dar es salaam

Huyu binti kwanza alikua ananikera kitu kimoja, anapenda sana video call sasa sijui alikua anataka kugundua nini

Ingawa nilikua sipendi lakini nikaona anyway kwakua ndo tumeanza mahusiano wacha nimlizishe

Hali hiyo haikunisumbua sana mana nikajua kadri tutakavyozoeana nitamueleza ukweli kwamba mimi sio mpenzi sana wa video call

Tulipanga kuonana na nilimuahidi kwamba ningeenda Arusha kuonana nae

Huyu binti alinivunja moyo kitu kimoja, kabla hata sijaenda kuonana nae kwa mara ya kwanza akanipiga mzinga wa 80k akidai kioo cha simu yake kimepasuka hivyo anataka akakibadirishe.

Alivyonambia hivyo tu nikaona hapa hamna mtu, yani hata kuonana physically kwa mara ya kwanza bado hatujaonana lakini nishapewa invoice ya 80k wakati yeye mwenyewe anafanya kazi na ana kipato.

Nilikua na uwezo wa kumpa ile hela lakini niliona mbona mapema sana kashaanza kuleta matatizo yake it means yupo after something.

Huyu binti nilimkatia mawasiliano 100% mana niliona hana tofauti na Golddigger na safari yenyewe nilii cancel

Ni kweli wanawake mnahitaji kuhudumiwa na wawanaume ila jitahidini kuficha shida zenu mwanzoni tu mwa mahusiano mana mtajikuta watu wanapiga kisha wanatembea yani ni kama vile kununua malaya Riverside kisha kila mtu anachukua hamsini zake.


Wanaume tujutahidi kutotaka kuwalala wapenzi wetu wapya mapema, ukitaka kumlala tu mwanamke, na yeye atataka kufaidika.
 
Madem wa arusha kweli wanapenda video call ila sioni kama ni shida alaf mwanaume ukiombwa hela usiwe mchoyo asee jifunze kutoa bila sababu ukiwa na familia nahisi kuna mambo watakosa maana hujui kutoa..... Kumnyima hiyo 80k haijamuathiri chochote zaidi anatafuta jamaa lake analichuna maisha yanasonga.

: Ukiona dem naaomba msaada mapema basi huyo kakupenda mpe tena ikiwezekana usisubiri aombe ww ukiwa na 5k mpe sio mpka siku akuombe 100k uanze kupagawa jf😂😂😂
 
Mkuu kuna wanaume wajinga utakuta ana Mpangia chumba changudoa na kumuhudumia, na hicho chumba kinageuzwa guest.
Hakuna mwanaume mjinga asee ukiona kaamua kufanya hivyo basi anaajua nini anafanya kwenye mapenzi kuna upofu mbaya sana kile ww unachoona huwez fanya mwenzako ndio hasikii haambiliki na swala linalohusisha hiisia tena za moyo sio akili basi linaweza kukuchanganya muda wowote.

Muda mwingine sisi wanaume tunajisemea mwanamke hawezi nisumbua ila uhalisia ni pale anapokua mwenyewe yeye na nafsi yake unakuta anaendeshwa sana na mapenzi kwakua sio jambo rahisi kulicontroll.
 
Ni kamgogoro kakubwa sana haka ka kuombana ombana, kila mtu abaki na chake, maana ke ukijifanya mstaarabu usiombe ombe ndo utakopwa kei mpaka ikome, so ni nipe kitu nitoe vituz hivyo yani
Si bora uweke bei elekezi, Au ujipange barabarani usiku tujue Moja Kapeace
 
Watu wa humu nawajua vizuri kipenzi,, ni kwamba tu napenda kusimamia ukweli.. na ushauri kama ni mzuri unafuatwa tu regardless nani ameleta.. and by the way am not a feminist,, nadhani hatuwezi kuwa na mitazamo sawa
Jibu murua kabisa bidada umeupiga mwingi sana
 
Tafuta pesa kijana[emoji36] Hivi kweli elfu 80 ni hela ya kunung'unika adi uvunje mahusiano na mtu unayesema unampenda?Je kuhudumia familia utaweza kweli ukiwa nayo maana vya kwenye familia gharama zinatiririkaga automatically mara mtoto aumwe mke ameze mswaki yaani tafrani hahaa.
Acha umatonya tafuta vyako.
 
ngoja nikujibu mojamoja, kua na mpenzi haimaanishi kwamba natafuta ndoa.. and by the way am too young for marriage (am only 22) which means I can't compete with anyone here, just was an advice to these girls ambao walikua wanatoa povu kwa mleta mada wakati kaongea kitu cha msingi... pia mitazamo yangu na yako ni tofauti cause naona kama una chuki binafsi na wanaume hadi ukaamua kua leisbian, so pole sana maana dawa yako mimi sina kipenzi...
Am Sorry kama nimetumia maneno magumu, lengo ni kukufanya tu uache kubishana na mimi kwasababu sipo kwenye hiyo mood 😊😘
Dah! Hili jibu lako lifanyiwe lamination tukahifadhi kwenye maonesho ya kumbukumbu ya Taifa
 
Na hao watu wa maana unadhani wanapitakana huku jf?? [emoji23][emoji23][emoji23]

Jipe moyo dada ila huku hamna kitu. Unachekesha kweli hahahahaha
Ila watu mnachekesha😃😃😃... aliyewaambia mimi niko humu kutafuta mtu nani🤣🤣🤣🤣🙌.,, ushauri kama haukufai unaachana nao tu kwani shida iko wapi??🤔🤔.. ukiona unaumizwa hadi na comments za humu jua una shida mahali sio bure🤣🤣
 
Hiyo ni mbinu moja wapo kumweka mbali mwanaume usiyemtaka.

Unampiga mzinga unatulia.

Tatizo most men mnaona mna haki ya kuomba sex earlier kabisa in the relationship pengine hata siku ya pili kujuana ila mwanamke akikuomba hela kidogo tu... Weeeeee mnamaindiiii[emoji23][emoji23]. Na mnapenda kutangaza mkiombwa hela hahahaha mbona sisi tunawasitirii,..
kinachowakera wanaume wengi ni usanii wa wanawake wengi unakuta wanagharamia sana na mzigo hawapati nauli inaliwa manzi hatokei.
 
kinachowakera wanaume wengi ni usanii wa wanawake wengi unakuta wanagharamia sana na mzigo hawapati nauli inaliwa manzi hatokei.
Poleni kwa hilo ila ni ngumu kuamini.

Ila most men, unaweza kumpa penzi na mkawa vizuri, anajipakulia tu anavyotaka ila hata kujiongeza kwamba atoe hata hela ya sabuni kwa mpenzi wake wapii???

Kama unahudumia, kwanini mwanamke aanze kukuomba omba hela?
 
Back
Top Bottom