Nilikuwa sifahamu kwann wanaume tunapofumania au kupata elements zozote za usaliti basi hatutakiwi kirudi nyuma.
Jibu ni rahisi. Wanawake ni jamii ya binadamu ambayo inapenda kuishi kwa kukadiria au kupimia ila sio watu wa standard za uhalisia.
Unaweza kuwa mwanaume wa kiwango cha mume Bora na baba safi wa familia ila yeye akata kukukadiria ziada ya hapo yaani akataka zaidi ya kile unachofanya na usipompa ndipo atatoka nje kutafuta na ukisitisha kumpa kile anachopata kwako bado ataanza kilalamika kuwa anaonewa.
Tazama katika hicho kisa hapo, mwanamke ametoka nje ya ndoa so it means hakuwa anakubali kuridhika na anachopewa na mumewe akataka ziada.
Ukimsamehe kwenye swala kama hili atakukadilia uwezo wako wa kufanya maamuzi lakini pia kuwa hauna maisha nje yake. Hivyo basi kumsamehe ni kama kumwambia nimekubali kuwa mpumpavu kwako na kudharaulika nifanye utakavyo. Hapo Guarantee ni kuwa atarudia tena upuuzi wake kama kawa kwa namna nyingine sababu ameshakukadilia kuwa wewe kwake ni dhaifu na hauna pa kwenda.
Anyways, katika mahusiano, mwanaume anajukumu moja tu la kumpenda mkewe na hilo linaonekana kupitia kumjali, kumhudumia, kumtunza na kumlinda. Mwanamke ana jukumu moja kwa mume wake la kumheshimu na kutii maelekezo na miongozo yake hii atafanya kwa kumsikiliza mwanaume, kumshauri , kumtunzia Siri na aibu, kumhudumia mahitaji kama ya chakula, usafi na watoto, kutunza mali za mumewe ikiwepo fedha etc.ila muhimu kabisa ni kutomuweka mbele mwanaume mwingine yoyote nje ya mumewe , awe baba mkwe, mjomba, rafiki, kaka, binamu, hata mchungaji.
Sasa hapo ukienda kinyume na hizo principles imekula kwako ndio haya yanatokea.
Mwanamke akikucheat usirudiane nae..... Utakuja kujuta baadae