Mkuu VIP mlifanikiwa kuweka mambo yenu sawaNafahamu hilo,
Ila huyu naweza sema ni mkorofi, maana anaeeza kutafuta sababu yoyote ile ili kunikwaza tu
Pia anajaribu kunitawala yaani anataka mimi niwe chini yake ( naweza kusema anataka mimi niwe mwanamke na yeye awe mwanaume )
Mfano hii leo na mvua hii inayonyesha imetokea dharula anataka mi nikamchukulie kitu sokoni ( katoka kujifungua ) mi nikamwambia na mvua siwezi kutoka kwa nini asingenunua au asingeniagiza tangu jana nirudi nacho mpaka aniagize leo asubuhi muda anaotaka kutumia?
Akajifanya kukasirika kufika saa 17:23 mvua ikapoa nikataka kwenda kumchukulia anadai basi kaghairi, kufika saa 20:00 anamwambia mzee kuna kitu anahitaji mimi nikamnunulie, mzee kuja kuniambia mimi nikapiga kimya
HUYU ANATABIA NYINGINE AMBAYO HII NDO ITAKUWA SABABU KUU YA KUMTALIKI
NI KWAMBA ANAWEZA KUNIKOROFISHA MAKUSUDI MWISHO WA SIKU MIMI NDO NAONEKANA MBAYA MAANA HUWA ANATABIA YA KUWAAMBIA NDUGU ZAKE NA HUYU RAFIKI YAKE AMBAYE NI MKE WA MPANGAJI MWENZANGU NA MAMA MWENYE NYUMBA
NA WAO BILA KUCHUKUA MAELEZO YA PANDE ZOTE MBILI WAISHIA KUNIONA MIMI MBAYA
Wacha niishie hapa maana mambo yapo mengi sana na hapa nilipo tayari nimeshaita wanafamilia kwa ajili ya kikao kesho naamini kesho ndo nitatoa maamuzi rasmi maana huyu mtoto wa pili hataki mimi nitoe jina anataka ampe yeye jina la mama yake wakati mtoto wa kwanza aliniambia nisitoe jina la kulithi kutoka kwa babu wala bibi ila yeye anataka kumpa
Kupika chakula kagoma badala yake kaenda kununua chips kala na mtoto mi kula kwa mama ntilie
Hayo yote niliyosema yametokea leo bado sijasema ya siku za nyuma yaliyopelekea niwe nampiga makofi
Nasubiri amalize arobaini mimrudishe kwao maana kikao cha kesho wanafamilia nitawajulisha hili tu basi
AISEEE...! NAONA BASI INATOSHA NDOA IMEKUWA NDOANA