Mkuu usiseme hivyo, labda kama hujapenda.
Kuna mwanamke unatokea kumpenda ila mkitofautiana unaleta ule uanaume tu kwamba lazima yeye ajinyenyekeze ndiyo umsamehe, ila kimoyomoyo hata wewe unatamani kumuomba msamaha yani.
Nakiri kwamba hii kitu ishanitokea kama mara 3 hivi in my lifetime. Kwa hasira utajikuta unafuta namba yake ya simu kumbe unayo kichwani [emoji1], uki-mute siku 3 na yeye aka-mute unaumia kinoma.
Mara unaiacha simu maghetoni au unaiweka kwenye silent mode ukidhania kwamba ukiishika utakuta missed call na msgs za "baby I am sorry", ukiicheki simu unakuta hola, moyo unazidi kuvuja damu.
Sasa ndiyo usema ampost mwanaume mwingine usiumie? Acha kabisa mkuu, tena hakuna status mbaya kama ile anampost mwamba mwingine halafu haweki caption yoyote. Alahaulaa...[emoji23]
Unajua kinachokuumiza ni nini? Ni ile una-imagine vile analalamika kipindi hicho mko faragha kwenye bedfight, sasa this time around, huo upendeleo wote anapewa mwanaume mwingine...[emoji3]
Acha tu braza. Inauma ingawa masela tunajifanyaga wagumu. Sema tu ndiyo ile falsafa ya kilio cha samaki, machozi yanaenda na maji. Kama hujamuelewa mbona fresh tu, hata afanye nini ndiyo kwanzaa unashukuru [emoji3].