Wanawake mtambue mwanaume kuvumilia usaliti ni 1 kati ya 10 chezeni kwa step

Wanawake mtambue mwanaume kuvumilia usaliti ni 1 kati ya 10 chezeni kwa step

Ahsante kwa pole yako, mwanaume anatakiwa atumie akili kumpata mke/girl sahihi, ndo maana unaambiwa tafuta wa kufanana nae wewe, shida Wanaume wanaongozwa na hisia za sio akili wakati wa kuchagua, narudia tena tumieni akili kuchagua na kuishi nao(wake/girl)
Hapo kwenye kuchagua Ni Mungu tu kwakweli. Ni Mungu tu atuelekeze maana yeye ndio anajua yupi sahihi
 
Inawezekana kabisa, Inategemea na imani yako pamoja na jinsi gani unamwishia Mungu, hili jambo sio la kutumia akili za kibinadamu mkuu, ukiambiwa akili ujue ni akili ya kimungu mkuu, na hata unapowaza hili ukiwaza kibinadamu huwezi kukubaliana na hili, (Hakuna jambo gumu la kumshinda Mungu)
Tuko pamoja Chief
 
Unaacha afu unaenda oa perhaps alieachwa pia
Nadhani kabla ya kuacha angalia kama haujachangia tatizo kwanza..
Je unampa mkeo haki inavostahili?.amechepuka kwa sababu gani?.
Kama kweli we ni msafi and u was doing ur best basi sawa
Othrwise Mungu anawaona
Ukishaona mumeo hakutimizii mahitaji yako na yupo mwingine unahisi ataweza kukutimizia basi omba kuachana na mumeo ili uende kwa mwanaume mpya lakini tatizo lenu mnataka kuliwa kule na huku hiyo haivumiliki hata kama mwanaume ndio kachangia tatizo.
 
Mm ndo sinaga kurembesha nitamvumilia mwanaume vyote lkn kamwe siwezi kumvumilia mwanaume malaya naachana nae mchana kweupe sijui nmetoka nae mbali hilo mm siangalii. Simpe di mwanaume asiyejua kufunga zipu yake.
 
Ukiona ndoa imevunjika ujue mwanaume kasababisha, (Ishi na mke wako kwa ajili)
Ndugu ngoja nikusaidie kitu ili uweze kuelewa..ndoa nyingi huvunjika hasa miaka ya hivi karibuni kwasababu wanawake wametoka kwenye misingi yao,mleta uzi ameeleza vyema.Wanaume huwa wanavumilia sana maudhi ya wake zao au wapenzi wao huwa hawasemi au kusimulia kwa mtu akiamini mwanamke wake atabadilika.lakini kwa bahati mbaya sana wanawake huanza kuelewa wakati tayari mwanaume ameshachoka na anaanza kuonesha sasa kuwa yale maudhi na karaha yaliyokusanyika katika moyo wake kwa kipindi chote.hapo mwanamke ndipo ataanza kulalamika kuwa ananyanyaswa,anateswa,mwanaume hampendi tena n.k.lakini kumbe hapo mwanzo alikuwa na nafasi ya kurekebisha kipindi cha nyuma wakati mume wake anajaribu na kumtaka kuwa na tabia au mwenendo fulani unaofaa.hivyo kujisahau kwa wanawake katika kufuata kanuni zile za kuishi na mwanaume anakuwa anatengeneza timed bomb ambalo halijulikani litalipuka lini.kwa kifupi ni hivyo ndugu.
 
Ukishaona mumeo hakutimizii mahitaji yako na yupo mwingine unahisi ataweza kukutimizia basi omba kuachana na mumeo ili uende kwa mwanaume mpya lakini tatizo lenu mnataka kuliwa kule na huku hiyo haivumiliki hata kama mwanaume ndio kachangia tatizo.
Kabisa haivumiliki hiyo
 
Mwanamke? Nifanyie ujinga lkn sio usaliti. Usaliti nikauthibitisha nilazima tuachane tu tena nbora uniache mapema kabla sijajua, kwasababu nikijua ,ukiona sijakuacha km weee ni mpenzi/mchumba tutaishia tu kukutumia lkn sitokaa nifanye hatua nyingine yabhapo naabadae bado tutaachana tu kwasababu hata mahusiano yenyewe hatokaa ayafurahie tena,..... Shida moja nilonayo nimgumu kusahau na msamaha wangu unategemea nakosa .

Simpo.
Hahahaa we mshkaji unaonekana umetupania sana wanawake [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Hahahaa we mshkaji unaonekana umetupania sana wanawake [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Hapana mkuu sio km nimewapania, bila shaka mwanamke anaakili na anayejua zuri nabaya..kwaupande wangu nitajitajidi kua namkumbusha.

Alafu ktk yote bado anisaliti?? Alafu nitulie?? Hapana.....nmekua mgumu sana maishan mwangu kuruhusu ujinga wamtu ndo uniumize.

Nitakua wamwisho kwakweli. Nibora nionekane mkoloni tu.
 
Mkuu unadhani wanaochukua hatua za kuuwa hawatafakari. Hapa ni kuomba hekima za kimungu
Unamuonea tu Mungu!kichwa amekupa cha nini sasa kama hukitumii. Uliacha kunyonya ziwa ur first food,haikuwa kesi,labda ulishapoteza wapendwa kibao maisha yakaendelea,ukafeli shule ukatafuta option nyingine!!!aaah Leo mapenzi yakupeleke jela?utapoteza mangapi? Mtafute hata Lulu tu akupe ushauri nasaha.
 
Mwanaume anayevumilia usaliti atakuwa na mchanganyiko wa roho yake, maana roho ya kiume halisi haiwezi vumilia kabisa hayo mambo
 
Nilikuwa na wazo la kuchepuka ,ila baada hizi comments naona nitamkera mke wangu akijua ,nabaki njia kuu,eeh Mwenyezi Mungu nisaidie
 
Back
Top Bottom