Dr Matola PhD
JF-Expert Member
- Oct 18, 2010
- 60,050
- 104,466
WANAUME WANA MAUMIVU PIA
Mwanamke mmoja aliniambia, 'Ilinichukua miaka kujua kwamba wanaume pia hulia. Nilimchukulia mume wangu kama binadamu bora. Ninamwona akitoka nyumbani kila siku na kurudi akitupa mahitaji yetu. Siku moja nikiwa nimetoka nyumbani na yeye alikuwa nyumbani, nilikumbuka kwamba nilihitaji kuchukua kitu nilikuwa nimekisahau nyumbani, niligeuka na kuelekea nyumbani. Nilipofika nyumbani, nilijaribu kupitia mlango wa nyuma ambao ulikuwa karibu na dirisha la chumba chetu. Nilimsikia mume wangu akilia kama mtoto mchanga akimwomba Mungu anisaidie nipate kazi ili nimsaidie kutunza familia. Hajawahi kunilalamikia hapo awali lakini siku hiyo, nilitokwa na machozi nikigundua kuwa mume wangu ameshikilia maumivu makali yake peke yake"
Binti msichana aliyeolewa muda si mrefu sana, aliwahi kwenda kulalamika kwa mama yake kwamba mume wake amekuwa hamtimizii mahitaji yake, basi yule mama kwa busara kubwa akamuuliza binti yake, ‘Umenunua vitu vingapi kati ya hivyo?” binti akakaa kimya na kusema, ‘Lakini huyo ni mume wangu si ana wajibu wa kunihudumia? Mama akamjibu, 'Je, umewahi kujua vitu ambavyo mumeo anataka umnunulie?".
Wanaume daima hujaribu kuficha maumivu yao.
Wanaume wanaweza kuwa kwenye msoto na wakati mgumu kifedha lakini wanaweza kufake kujifanya kuwa wana kila kitu.
Wanaume wengi wameoa lakini wana maisha ya upweke kupita maelezo.
Wewe mwanamke wakati mwingine jaribu kuongea na mume wako kwa utaratibu na utulivu utapata kitu kikubwa sana kutoka kwa wanaume, Wanaume huwa sio kwamba wako busy kila wakati kama wanawake wanavyofikiria.
Unapaswa kuelewa kwamba mume wako ana maumivu na ana mahitaji pia. Usimhukumu kwa mambo unayotaka kutoka kwake tu, Wakati mwingine mume wako hana mambo unayotaka wewe.
Wanaume pia wana mahitaji na matatizo ya kihisia. Wanaume bado wanalia kwa mapenzi na wanahitaji upendo wa mwanamke ...