Wanawake ni viongozi na wasimamizi bora wa jamii na nchi

Wanawake ni viongozi na wasimamizi bora wa jamii na nchi

Willima

Member
Joined
Jul 27, 2022
Posts
26
Reaction score
39
Kumekuwa na mtazamo wa kimazoea hasa Katika nchi za Afrika, Kuwa mwanamke hawezi kusimamia jamii na nchi kwa ujumla, maranyingi mwanamke huonekana kama mtu ambaye uwezo wake wa kusimamia hutegemea muongozo wa mwanaume na Kuwa mwanamke mwenyewe hawezi kusimamia na kufanya maamuzi hata Katika familia.

Jambo hili ni lakimtazamo duni sana kwani tunaona uwezo wa wanawake walio bahatika kupata nyadhifa mbalimbali za uongozi na kufanya mambo mazuri na yenye faida kumbwa kwa jamii na nchi kwa ujumla, ingawa kumekuwa na changamoto kwa wanawake Waliopata nyadhifa mbalimbali za uongozi, hasa Katika jamii na nchi za Afrika.

Changamoto nyingi zinatoka Katika jamii hizo ambazo hutokea wanawake wenyenye nyadhifa za uongozi. changamoto kuu ni viongozi wa kike kutokupata ushirikiano kutoka kwa wanajamii wanao waongoza. Mwanamke pia ni msimamizi bora wa jamii na nchi kama atapokea ushirikiano kutoka kwa jamii yake.
 
Back
Top Bottom