Mzee wangu alishawahi kuniambia usimuendekeze mwanamke maisha ya starehe hata kama pesa unayo, akaniambia pia hakikisha asijue kipato chako yaani statement yako ya bank hadi salaryslip iwe siri yako hata akiba yako jitahidi kuwa msiri maana huwa hawariziki kwa kweli mzee sikumuamini
Nna mwanamke wangu ambaye niko nae kwenye mahusiano mwaka wa tatu huu ana miaka 23, hana elimu yoyote ya maana , alizungushaza olevel akawa mtaani tu maana analelewa na ndugu wazazi alishapoteza
Nimeanza nae mahusiano akiwa kwenye hali tete maaana alikuwa akiishi maisha magumu sana hata hao ndugu kumjali walikuwa hawamjali, wanaume aliokuwa nao ndio wale masharobaro kula kwa mama
Hivyo kuanzia mwaka huu umeanza nikaona maisha ya mwanamke kukaa nyumbani tu si mazuri nikaona nimpush na yeye aingize kipato na mimi majukumu ya kutoa pesa ya matumizi kila siku yapungue nipate ahueni na yeye apate pesa afanye mambo yake ya muhimu
Hivyo nikawa nashirikiana nae kwenye biashara zangu kila siku, nikawa namlipa 15,000 siku nyingine 20,000 hadi 17,000 na siku hali ikiwa tete mara chache sana nampa 12,000, hapo nauli,kula,vocha juu yangu mimi na akirudi nyumbani kwao halipi kodi, maji wala chakula hanunui anakikuta mezani ye hela nayomlipa ni kuweka tu
Lakini wakuu kipindi cha hivi karibuni akawa amenza malalamiko na vijembe vya chini chini yaani anasema simjali, mean simpi pesa, mean mimi ni bahili, vijembe anaweka hadi wahtsapp mwanaume bahili hafai ila huwa nakausha tu napita kimya kimya
Ila sikutegemea zarau kama hizi maana nilitegemea mwenzangu tunachotafuta na kugawana angerizika lakini now anataka nimpe na pesa nyingine tena ya matumizi hapo ndio nimechoka
Ila nachowashauri tu hivi viumbe tuishi navyo kwa Tahadhari sana maana haviriziki wala kujua ugumu wa kutafuta pesa , na unachowapa hawaridhiki wanaona wanahitaji kikubwa zaidi ya walichonacho
Think hana elimu yoyote
Kwa siku namlipa 15,000-17,000 hadi 20,000, nauli kula maji na vocha ni juu yangu , yeye akifika nyumbani kwao ni kula kulala halipi kodi maji wala umeme, hela anayoipata ni kuweka, then analalamika simpi hela ya matumizi..
Nimewasilisha tu..