Nchi Kavu
JF-Expert Member
- Sep 11, 2010
- 4,290
- 2,468
Habari za Jumapili.
Nikiwa nimetulia ndani jioni namuona mamsap akirudi toka kwenye mishe. Pia alipitia saluni. Katengeneza nywele zake vizuri anavutia kumtazama
Sasa ujinga ni kuwa kufika tu kachukua kilemba kafungia nywele humo kazibania vizuri hata isionekane hata moja! Hapo tayari kuanza mishe za nyumbani. Ule mvuto aliokuja nao ukatoweka.
Ikifika asubuhi anajikwatua tena na kuziachia vizuri tayari kwenda kazini. Huko anakutana na wenzake. Mabosi, vijana, wababa, wapita njia, n.k. Wote kwa nyakati tofauti wanavutiwa nae kwa muonekano ambao alipokuwa nyumbani aliuficha.
Jioni inafika tena anafika nyumbani na kujitupia tambara lake kichwani. Tena anaweza kutafuta na nguo nguo huko akajitupia kisha akaendelea na mishe za nyumbani.
Kwa hali hii hamasa itakuwepo? Hakika yatabakia mazoea tu.