Wanawake ni wazuri wakiwa kazini

Wanawake ni wazuri wakiwa kazini

Habari za Jumapili.
Nikiwa nimetulia ndani jioni namuona mamsap akirudi toka kwenye mishe. Pia alipitia saluni. Katengeneza nywele zake vizuri anavutia kumtazama

Sasa ujinga ni kuwa kufika tu kachukua kilemba kafungia nywele humo kazibania vizuri hata isionekane hata moja! Hapo tayari kuanza mishe za nyumbani. Ule mvuto aliokuja nao ukatoweka.

Ikifika asubuhi anajikwatua tena na kuziachia vizuri tayari kwenda kazini. Huko anakutana na wenzake. Mabosi, vijana, wababa, wapita njia, n.k. Wote kwa nyakati tofauti wanavutiwa nae kwa muonekano ambao alipokuwa nyumbani aliuficha.

Jioni inafika tena anafika nyumbani na kujitupia tambara lake kichwani. Tena anaweza kutafuta na nguo nguo huko akajitupia kisha akaendelea na mishe za nyumbani.

Kwa hali hii hamasa itakuwepo? Hakika yatabakia mazoea tu
Yaani huyo ni mimi kabisaaaaa,
Hapa yenyewe nipo kama nimetoka kwenye mashimo ya migodi nywele zipo kitimtim, sina habari nazo.
 
Mimi mama watoto wangu alileta swaga hizo za kuchakaa tukiwa wote nyumbani huku kazi anafanya msaidizi, nikamchana makavu akajinunisha kidogo ila naona kwasasa mambo mazuri kabadilika.

Ni afadhali kuambiana ukweli kuliko kuishi na sononeko na kukufanya faza geto ubadili tabia. Hata mimi kama nazingua huwa ananichana tu
 
Mwili kupumua sawa kabisa lakini uko maridadi umependeza siyo ndani ya visempele na kwa kuwa nywele ziko nyuku nyuku kuzificha ndani ya TAMBARA 🤣🤣🤣🤣 nakwambia KE wengi ndani ya ndoa hawawezi kuthubutu kwenda makazini kwao na visempele vyao wanavyovaa majumbani.

Jamani tunafunga nywele maana haitakiwi tupike na nywele wazi zitaangukia kwa chakula jamani. Sasa kutwa nzima nimejibana nikirudi home kadera lazima kahusike mwili upumue kidogo.
 
Jamani tunafunga nywele maana haitakiwi tupike na nywele wazi zitaangukia kwa chakula jamani. Sasa kutwa nzima nimejibana nikirudi home kadera lazima kahusike mwili upumue kidogo.
Kama najiona nikitoka mishe huko dera liko wapi hata sidiria sivai ziwa linacheza segere tu kifuani, halafu Kuna Yale Madera ya kushindia yamepauka 🤣🤣🤣🤣 dah, Yale yaliyoiva mapya mapya eti yakutokea.
 
Akina Mama na akina dada ikiwapendeza tuzingatie mafunzo ya Kungwi laoo Irene Mbowe kuhusu vazi la wkend
Anasema uvae vzuri upendeze na haiba yako mwanamke hasa Mr akiwepo
Kama inavyoonekana hp pichani kwa kungwi laoo
F5056DA5-B3DE-46E9-8774-4B1A21337530.jpeg
8E179884-281E-476A-AF3F-8669DFA5F607.jpeg

Cc
Espy Karucee kajojo
Beef lasagna
Evelyn Salt
 
Mwili kupumua sawa kabisa lakini uko maridadi umependeza siyo ndani ya visempele na kwa kuwa nywele ziko nyuku nyuku kuzificha ndani ya TAMBARA [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] nakwambia KE wengi ndani ya ndoa hawawezi kuthubutu kwenda makazini kwao na visempele vyao wanavyovaa majumbani.
Mweeeh!! Mnatunanga hadi sio poa[emoji1787]
 
Kama najiona nikitoka mishe huko dera liko wapi hata sidiria sivai ziwa linacheza segere tu kifuani, halafu Kuna Yale Madera ya kushindia yamepauka [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] dah, Yale yaliyoiva mapya mapya eti yakutokea.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Kweli kabisa vitu vipate hewa jamani. Halafu hivyo videra vilivyopauka vinanoga kweli kushindia nyumbani.

Sasa hadi uje utulie ujipare saa ngapi jamani na majukumu kibaao yanakusubiri[emoji2297][emoji2297]
 
Back
Top Bottom