Wanawake njooni hapa mfahamu wanaume tunataka mwanamke wa aina gani

Rorscharch

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2013
Posts
878
Reaction score
2,014
Tumekaa Wakataa Ndoa na tulio ndani ya Ndoano, tumekuja na Ukweli Mchungu kwa Faida yenu wanawake

Ndoa sio lelemama, sio karata za Bahati Nasibu, na kwa hakika sio safari ya majaribio. Hii ni safari ya milele inayohitaji maarifa, uvumilivu, na upendo wa kweli. Tukiwa tumejifunza mengi kupitia kushuhudia ndoa nyingine au kuishi katika ndoano wenyewe, tunaamua kuwapa ushauri huu muhimu kwa faida yenu. Kama mna nia ya kuyafanyia kazi, hakika mtajenga ndoa zenye nguvu. Kama mtaamua kufumba macho na kushupaza shingo, basi mjiandae kupambana na matokeo.

1. Fubaza Hicho Kiburi Chako – Ni Sumu ya Ndoa

Kiburi ni silaha inayotoboa moyo wa mwanaume bila huruma. Hakuna kinachochosha mume zaidi ya kuwa na mke asiyesikiliza. Yeye anakushauri kitu cha maana, unakimbilia kufanya kinyume. Kibaya zaidi, ukionesha kiburi chako kwenye miradi ya maendeleo, hali itazidi kuwa ngumu. Mumeo akikufungulia biashara, halafu ukaichoma kutokana na jeuri au kutokufuata maelekezo, atapoteza imani nawe. Siku akiona huwezi kushirikiana naye kujenga ndoto zenu, atakutenga kutoka kwenye maamuzi makubwa. Utashushwa daraja na kuwa mtu wa kutumwa tu vitu vidogo vidogo vya dharura. Kama bado hamjazaa, jiandae kwa kibuti – maana kwake huonekani kuwa na faida.

2. Usigeuze Kichwa Chako Kuwa Beseni la Mawazo ya Mashosti na Jamaa

Tabia ya kulinganisha ndoa yako na maisha ya wengine ni bomu linalosubiri kulipuka. “Asha kafanya hivi,” “Baba fulani kafanya vile,” kila mara unaenda nyumbani na mifano ya watu wengine. Hii ni kero kubwa kwa wanaume wengi. Mumeo siku akichoka kelele zako, atakutolea uvivu: utaambiwa "Nenda ukaishi huko kwa Asha na Baba fulani.” Badala ya kushinda ukimlaumu, kuwa mshirika wa kweli katika changamoto zake. Kama mumeo anakwama kusimamia miradi kwa sababu ya shughuli nyingi, vaa viatu vyake na uwe msaada. Simamia miradi hiyo kwa upendo na maarifa. Ukikaa tu na kuwa “mdomo wa lawama,” atakuchukulia kama mzigo, na unajua mzigo unavyoshushwa unapokuwa mzito kupita kiasi.

3. Dhama za Mama wa Nyumbani Zimepitwa na Wakati – CHANGAMKA!

Hata kama unahisi miradi ya mumeo haikuvutii , tafuta shughuli zako. Kuwa na kazi, biashara au shughuli yoyote itakayokuwezesha kuchangia kwenye maisha yenu ya kila siku. Sio kila jambo ulitegemee mumeo. Dunia ya sasa haihitaji wanawake tegemezi wa kila kitu – kuanzia pedi hadi nywele. Mumeo akikosa pesa na ukashindwa kujihudumia, hakika ataanza kujiuliza maswali mazito na pia yeye mwenyewe yataanza maswali mazito ("huyu mwanamke anaweza akaanza umalaya apate hela za nywele). Ukitaka mumeo akuheshimu, jitahidi kuwa mchango katika maendeleo ya familia yenu. Ukikaa bila kujishughulisha, atakuona kama mzigo, na mzigo siku zote hupelekea mwanaume kutafuta “mpambanaji” huko nje.

4. Kipato Chako Ni Cha Familia, Sio Chako Pekee

Kama unapata kipato, ni vyema kukitumia kwa maendeleo yenu wote. Achana na tabia ya kusema “Pesa yangu ni yangu na ya mume wangu ni yetu.” Fikiria zaidi kuhusu uwekezaji kama kununua matofali ya kujenga nyumba badala ya kupoteza pesa kwenye sherehe zisizo na faida. Katika uchumi wa sasa, ni vigumu mwanaume kubeba kila mzigo peke yake. Wanawake wa kizazi hiki wanahitajika kuwa washirika wa kweli wa maendeleo. Fikiria mke anayemwambia mume wake, “Wewe pambana na ada za watoto, nitaweka hela ya kodi.” Je, unafikiri mume huyo hatakuona kuwa mwanamke wa kipekee? Badala ya kupoteza pesa zako kwenye mambo yasiyo na faida, hakikisha unachangia juhudi za kuimarisha maisha yenu.

5. Acha Utoto – Umeolewa Sasa

Ndoa sio mahali pa kudeka au kununiana kwa sababu hujapewa zawadi fulani. Huu sio uchumba – hapa kuna majukumu mazito ya kushughulikia. Ukishakuwa mke, kumbuka kwamba majukumu yako yamebadilika. Mume wako hawezi tena kuendeleza utoto wako wakati anafikiria nguo za watoto, kodi ya nyumba, na mahitaji mengine ya familia. Kama bado unaendeleza tabia za single ladies, huenda ukashindwa kudumu katika nafasi yako. Heshimu ndoa yako, heshimu mume wako, na tambua kwamba umeingia katika maisha yenye changamoto lakini pia yenye malipo makubwa kwa wale wanaojitahidi. Mmefika mwezi December na kikoba chenu kimenona kinaruhusu ujidamshi basi mumoe hataona shida kufanya kile unachowaza akufanyie ila sio unaona kabisa hapa hata ada ya watoto Januari kuzungumkuti na wewe unamuongezea stress kwa kununa juu ya kwamba hajakununulia sijui wigi la laki moja ulilokuwa unataka; hapa ataona humo ndani ukiondoa yeye, wewe na hao wanao uliomzalia wote ni watoto

Ndugu Zangu Wanaume, nadhani kuna mengi ambayo tumegusia, lakini kama kuna jambo nimeacha, tafadhali ongezeni. Tuwasaidie dada zetu kujua jinsi ya kushikilia ndoa zao na kuwa wake wa viwango. 😄
 
Swali ni je, yeye anataka wa aina yako? Hainaga formula hiyo tutajua huko huko tukifika
Angekua hataki wa aina yangu angeendelea kuota jua kwenye kibalaza cha usimbe kama mjusi
 
SIo mbaya kama umepata ambae ni maskini hana means yoyote ya kuishi. Afadhali umemsaidia
 
Inashangaza Sana wanakuja na standard kibaaaaao as if sie tunawataka vyovyote walivyo msiiiiew.
Siku hizi tunawapatia mbona, tunasubiri mnafika miaka 30 tunaanza kujichagulia kama mnadani , tena wateja tunapambaniwa
 
SIo mbaya kama umepata ambae ni maskini hana means yoyote ya kuishi. Afadhali umemsaidia
SIo mbaya kama umepata ambae ni maskini hana means yoyote ya kuishi. Afadhali umemsaidia
I'm lucky, Mimi nimepata second in command; yaani hata nikifa kesho najua watoto wangu wapo mikononi salama
 
Tumekaa Wakataa Ndoa na tulio ndani ya Ndoano, tumekuja na Ukweli Mchungu kwa Faida yenu wanawake

Ndoa sio lelemama, sio karata za Bahati Nasibu, na kwa hakika sio safari ya majaribio. Hii ni safari ya milele inayohitaji maarifa, uvumilivu, na upendo wa kweli. Tukiwa tumejifunza mengi kupitia kushuhudia ndoa nyingine au kuishi katika ndoano wenyewe, tunaamua kuwapa ushauri huu muhimu kwa faida yenu. Kama mna nia ya kuyafanyia kazi, hakika mtajenga ndoa zenye nguvu. Kama mtaamua kufumba macho na kushupaza shingo, basi mjiandae kupambana na matokeo.

View: https://www.facebook.com/reel/1569856757236504
 
Na hapo ndipo mnapofeli wanaume kujiwekea matarajio mengi yasiyo na uhalisia kwa wanawake halafu mwisho wa siku mkikuta mambo tofauti mnapata vihoro, yani unataka mwanamke afanye majukumu yake bado akusaidie na yako huku wewe ukifanya yako tu je yake nani anamsaidia na mbaya zaidi bado unataka akutii, sasa hapo umuhimu wa mwanaume kwa mwanamke uko wapi kama mwanamke anaweza kufanya majukumu yote hivi huwa mko serious na mnayoyaandika au huwa mnatania tu
 
Huyu jamaa kamandika madin sana. Ni ngumu sana kwa ambaye bado hajaoa/kuolewa kuelewa alichoandika humu ila kwa walio ndani ya ndoa haswa wanaume lazima wakubali alichoandika jamaa.
 
Tumekaa Wakataa Ndoa na tulio ndani ya Ndoano, tumekuja na Ukweli Mchungu kwa Faida yenu wanawake

Ndoa sio lelemama, sio karata za Bahati Nasibu, na kwa hakika sio safari ya majaribio. Hii ni safari ya milele inayohitaji maarifa, uvumilivu, na upendo wa kweli. Tukiwa tumejifunza mengi kupitia kushuhudia ndoa nyingine au kuishi katika ndoano wenyewe, tunaamua kuwapa ushauri huu muhimu kwa faida yenu. Kama mna nia ya kuyafanyia kazi, hakika mtajenga ndoa zenye nguvu. Kama mtaamua kufumba macho na kushupaza shingo, basi mjiandae kupambana na matokeo.

1. Fubaza Hicho Kiburi Chako – Ni Sumu ya Ndoa

Kiburi ni silaha inayotoboa moyo wa mwanaume bila huruma. Hakuna kinachochosha mume zaidi ya kuwa na mke asiyesikiliza. Yeye anakushauri kitu cha maana, unakimbilia kufanya kinyume. Kibaya zaidi, ukionesha kiburi chako kwenye miradi ya maendeleo, hali itazidi kuwa ngumu. Mumeo akikufungulia biashara, halafu ukaichoma kutokana na jeuri au kutokufuata maelekezo, atapoteza imani nawe. Siku akiona huwezi kushirikiana naye kujenga ndoto zenu, atakutenga kutoka kwenye maamuzi makubwa. Utashushwa daraja na kuwa mtu wa kutumwa tu vitu vidogo vidogo vya dharura. Kama bado hamjazaa, jiandae kwa kibuti – maana kwake huonekani kuwa na faida.

2. Usigeuze Kichwa Chako Kuwa Beseni la Mawazo ya Mashosti na Jamaa

Tabia ya kulinganisha ndoa yako na maisha ya wengine ni bomu linalosubiri kulipuka. “Asha kafanya hivi,” “Baba fulani kafanya vile,” kila mara unaenda nyumbani na mifano ya watu wengine. Hii ni kero kubwa kwa wanaume wengi. Mumeo siku akichoka kelele zako, atakutolea uvivu: utaambiwa "Nenda ukaishi huko kwa Asha na Baba fulani.” Badala ya kushinda ukimlaumu, kuwa mshirika wa kweli katika changamoto zake. Kama mumeo anakwama kusimamia miradi kwa sababu ya shughuli nyingi, vaa viatu vyake na uwe msaada. Simamia miradi hiyo kwa upendo na maarifa. Ukikaa tu na kuwa “mdomo wa lawama,” atakuchukulia kama mzigo, na unajua mzigo unavyoshushwa unapokuwa mzito kupita kiasi.

3. Dhama za Mama wa Nyumbani Zimepitwa na Wakati – CHANGAMKA!

Hata kama unahisi miradi ya mumeo haikuvutii , tafuta shughuli zako. Kuwa na kazi, biashara au shughuli yoyote itakayokuwezesha kuchangia kwenye maisha yenu ya kila siku. Sio kila jambo ulitegemee mumeo. Dunia ya sasa haihitaji wanawake tegemezi wa kila kitu – kuanzia pedi hadi nywele. Mumeo akikosa pesa na ukashindwa kujihudumia, hakika ataanza kujiuliza maswali mazito na pia yeye mwenyewe yataanza maswali mazito ("huyu mwanamke anaweza akaanza umalaya apate hela za nywele). Ukitaka mumeo akuheshimu, jitahidi kuwa mchango katika maendeleo ya familia yenu. Ukikaa bila kujishughulisha, atakuona kama mzigo, na mzigo siku zote hupelekea mwanaume kutafuta “mpambanaji” huko nje.

4. Kipato Chako Ni Cha Familia, Sio Chako Pekee

Kama unapata kipato, ni vyema kukitumia kwa maendeleo yenu wote. Achana na tabia ya kusema “Pesa yangu ni yangu na ya mume wangu ni yetu.” Fikiria zaidi kuhusu uwekezaji kama kununua matofali ya kujenga nyumba badala ya kupoteza pesa kwenye sherehe zisizo na faida. Katika uchumi wa sasa, ni vigumu mwanaume kubeba kila mzigo peke yake. Wanawake wa kizazi hiki wanahitajika kuwa washirika wa kweli wa maendeleo. Fikiria mke anayemwambia mume wake, “Wewe pambana na ada za watoto, nitaweka hela ya kodi.” Je, unafikiri mume huyo hatakuona kuwa mwanamke wa kipekee? Badala ya kupoteza pesa zako kwenye mambo yasiyo na faida, hakikisha unachangia juhudi za kuimarisha maisha yenu.

5. Acha Utoto – Umeolewa Sasa

Ndoa sio mahali pa kudeka au kununiana kwa sababu hujapewa zawadi fulani. Huu sio uchumba – hapa kuna majukumu mazito ya kushughulikia. Ukishakuwa mke, kumbuka kwamba majukumu yako yamebadilika. Mume wako hawezi tena kuendeleza utoto wako wakati anafikiria nguo za watoto, kodi ya nyumba, na mahitaji mengine ya familia. Kama bado unaendeleza tabia za single ladies, huenda ukashindwa kudumu katika nafasi yako. Heshimu ndoa yako, heshimu mume wako, na tambua kwamba umeingia katika maisha yenye changamoto lakini pia yenye malipo makubwa kwa wale wanaojitahidi. Mmefika mwezi December na kikoba chenu kimenona kinaruhusu ujidamshi basi mumoe hataona shida kufanya kile unachowaza akufanyie ila sio unaona kabisa hapa hata ada ya watoto Januari kuzungumkuti na wewe unamuongezea stress kwa kununa juu ya kwamba hajakununulia sijui wigi la laki moja ulilokuwa unataka; hapa ataona humo ndani ukiondoa yeye, wewe na hao wanao uliomzalia wote ni watoto

Ndugu Zangu Wanaume, nadhani kuna mengi ambayo tumegusia, lakini kama kuna jambo nimeacha, tafadhali ongezeni. Tuwasaidie dada zetu kujua jinsi ya kushikilia ndoa zao na kuwa wake wa viwango. 😄
Uko sawa ila ndoa ni kama mpila kila kocha na mfumo wake na kila mtu na tamaa zake wengine wanapenda hao wenye kiburi
 
Back
Top Bottom