Wanawake si wabinafsi kama wanaume mnavyotuchukulia, huwa tunawaza msiyo ya waza

Wanawake si wabinafsi kama wanaume mnavyotuchukulia, huwa tunawaza msiyo ya waza

Wanawake tumetoka sayari ya Zuhura (Venus), hata mawazo yetu yako ki Zuhura tofauti inaanzia hapo. Mwanaume anawaza mambo makubwa lakini anasahau kuwa haya madogo yakikosekana tofauti itaonekana

Mwanaume atanunua kiwanja, atajenga nyumba lakini hafahamu kuwa deco ndani ya nyumba ni muhimu na inafanya nyumba kuwa nyumbani. Wanawake wengi deco na upambaji viko kwenye damu zetu. Huwezi kukaa kwenye nyumba ambayo haijapambwa

Mwanaume atalipa Ada ya mtoto milioni tano, atampa mtoto nauli ya kwenda shule na elfu ishirini ya kujikimu. Mama anafahamu kuwa kijana wake amefikia umri wa balehe na anajua Kuna style ya mavazi anayoipenda ili aendane na vijana wenzake. Mama atatoa laki mbili pasi Baba kufahamu kijana anakwenda chimbo kutafuta viwalo

ili tuweze kuishi pamoja katika sayari dunia inabidi tuwe wawazi na tuelewane. Tunahitajiana katika maisha ya kila siku.

Kweli, kuna mwanamke mmoja nilikua namuhudumia alikua mpenzi wangu, tuna mwezi hivi, nakuja kuta wanawasiliana na ex wake

Nikamkanya, akasema ameacha, nikambamba tena nikampiga chini, et akanipa sababu simjulii hali kila siku, aiseeee yaani nakupa kila kitu afu et text tu za umekula nini
 
Back
Top Bottom