Judithkaunda
Member
- Aug 21, 2022
- 90
- 231
Ni kweli wanawake tunapenda kuongea tena ni jadi yetu, lakini tujitahidi kuchuja maneno tusisahau hata Bibilia imeandika, "Mwanamke mwenye hekima huijenga nyumba yake, lakini mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe".
Leo ntaongelea wenzangu na mie mama wa nyumbani.
Dada unajijua huingizi kipato kinachoweza kumudu mahitaji ya familia yako na hata kama unabiashara yako lakini asilimia 80 mume anahudumia familia. Embu tusijisahau rafiki zangu, huenda ni kweli kuna namna mwanaume anakosea au hajatoa pesa kwa wakati imepelekea na wewe ukapata changamoto fulani hapo nyumbani, ndugu yangu ndiyo unune siku nzima jamani?
Mumeo katoka kazini kachoka hujui hata amepitia mangapi huko kazini, karudi nyumbani akitegemea kupumzika, kuliwazwa wewe ndio umenuna hapo, ukiulizwa kelele zinaanza.
Dada mwenye tabia hii chunguza vizuri, wewe ndiyo sababu ya mumeo kuwa mlevi kupindukia. Wewe ndiyo sababu anachelewa kurudi au harudi kabisa. Wewe ndiyo unawapa nafasi kubwa michepuko.
Halafu utasikia mdada anaongea kwa ujasiri, huyu mwanaume hana shukrani amekosa nini kwangu jamani?
Wanawake tusijisahau, mume anahitaji heshima.