Jukumu la kutunza familia ni la mwanaume, imeandikwa katika vitabu vyote vya dini. Sitaishi kwa kumtegemea mwanamke hata awe kiongozi mkubwa na mwenye mshahara mkubwa mara 10 yangu.
Nitaishi kadri ya uwezo wangu na cha mke wangu itakuwa ni ziada tu ila daima sitamtegegemea haswa katika yafuatayo 1. Kulisha familia, 2. Ujenzi wa nyumba, 3. Ada za watoto, 4. Malipo ya maji, umeme, TV, nguo za wanafamilia, malipo ya wafanyakazi (house girl, house boy, mlinzi) n.k.
Mwanamke anachopata kitakuwa nyongeza tu. Ndio kanuni ilivyo hata kama analipwa mara tano Zaidi yako usimtegemee utakuja kulia kilio cha mbwa koko mdomo juu