Wanawake tuwe waelewa tukiwa kwenye ndoa jamani

Wanawake tuwe waelewa tukiwa kwenye ndoa jamani

Halafu tukisema humu mwanamke aliyesoma ni LIABILITY kwenye ndoa tunaonekana wapuuzi, mara ohoo.. hatujiamini..blah blah blah!

Labda tuwekane sawa kwenye kitu kimoja na wote mnaojiandaa kuoa wanawake wasomi/wenye kazi muipate hii.

-Kadri mwanamke anavyozidi kusoma umuhimu wake kwa mwanaume unapungua. Na hata akiangia kwenye ndoa ni kwa ajili ya kupandisha social status tu.

-Mwanamke aliyeelimika hasa aliyefika ngazi za juu ana ndoto binafsi nyingi sana za kutimiza na huwa hazifi hivi hivi tu. Anaweza akazitelekeza kwa muda lakini siku akipata fursa ya kuzitimiza ndoto zake lazima aitumie fursa hiyo hata kama tayari yumo ndoani na hajari kama itaathiri ndoa.

-Mwanamke hata awe na uchumi mkubwa kiasi gani lakini ile natural instinct ya utegemezi haiwezi kumtoka, sana sana akijitahidi atakupunguzia mzigo tu kama mmezaa nae yeye atajigharamia mwenyewe huku watoto akikuachia wewe.

-Kadri mwanamke anavyozidi kuishi na wewe kwenye ndoa ndivyo anavyozidi kukuchoka hasa kama anajiweza kiuchumi na haoni hatari kuvunja ndoa maana hana cha kupoteza.

Kiufupi tu ni kwamba wanawake wasomi ni watu wenye matatizo mengi sana ndoani.

To a woman more education more problems in marriage-wise.
Umemaliza kila kitu
 
Mwanamke umebahatika kupata mwanaume wako wa ndoa,mnaishi vizuri tu,lakini kwa nini sisi wanawake tunakuwa tunawategea wanaume na huku unajua fika hali ya mmeo? Na huku tuna ingiza vipato vyetu wenyewe

Kuna mkaka nimemuonea hadi huruma

Huyu kaka ni mfanyakazi wa serikali na mke wake pia

Siku za hivi karibuni amemaliza chuo,ila gharama za chuo alikuwa anajigharamikia kwa kiasi kikubwa na kulingana na maisha ya chuo na gharama ,aliweza kukopa kwenye Benki moja hivyo kwa wastani kwa makato ya mshahara wake ,mshahara ukawa mdogo sana,na ulivyotoka wa mwezi uliopita alilipa kodi ya nyumba na nyingine kwenye shughuli za kilimo,akawa hana kitu

Na bahati nzuri mke wake anajua hali yake ya uchumi na kila kitu

Sasa leo mke wake kasafiri kwenda nyumbani kwao,na kwa vile mke wake anajua hali ya mme wake,mwanaume akafikiri mwanamke angefanya shopping ya mahitaji ya ndani kabla hajaondoka ili watoto wao watatu na mmewe wasipate shida

Lakini mwanamke hakununua mahitaji ya ndani ameondoka kwenda kwao akisema wazazi wake wamemuita kwa dharura

Mwanaume alivyojaribu kumuuliza "Mbona umetuacha bila kitu ndani?

Majibu ya mwanamke" Hivi wewe si ndo mwanaume, yaani unadiriki kuniambia jambo kama hilo,kwani mimi ndo mwanaume wa familia,wewe fanya mpango mle na wanao lakini sio kuniambia mambo ya ajabu"

Loh! Kaka wa watu mpaka nimemhurumia,

Jamani na sisi wanawake tuwe na utu,familia ni ya wote, na kama mwanaume hali si nzuri,ajibika asilimia 100,lakini si kwa roho mbaya hiyo
Ukimpata mwanamke wife materials, mwenye hofu ya Mungu..anaweza akakufunika kwenye mambo mengi sana...

Ukikutana na mwanamke kimeo, ukiyumba kiuchumi atakunyanyasa mpaka kazini kwako wafahamu kinachoendelea chumbani kwenu...

Hii sijahadithiwa...nimeiona kazini...[emoji41][emoji41][emoji41]
 
Mkuu Nakuunga mkono!!!!

Asili ya mwanamke ni kuhudumiwa na kuongozwa+ kutawaliwa na mwanaume siyo kutoa huduma (Japo siyo wote wako hivyo) ndiyo maana mimi huwa nashauri usioe mwanamke kwa kuangalia kipato chake au elimu. Vijana wa sasa walio wengi hukimbilia kuoa wafanyakazi kwa kigezo cha kusaidiana bila kujua maana na mapana ya neno "Kusaidiana"

Kuhusu Wanawake kuwa na urafiki na shetani, naomba uweke akiba ya maneno (maana hata mama zetu na dada zetu ni hao hao wanawake)
Ambia wanaume wenzio wakusikie
 
Jukumu la kutunza familia ni la mwanaume, imeandikwa katika vitabu vyote vya dini. Sitaishi kwa kumtegemea mwanamke hata awe kiongozi mkubwa na mwenye mshahara mkubwa mara 10 yangu.

Nitaishi kadri ya uwezo wangu na cha mke wangu itakuwa ni ziada tu ila daima sitamtegegemea haswa katika yafuatayo 1. Kulisha familia, 2. Ujenzi wa nyumba, 3. Ada za watoto, 4. Malipo ya maji, umeme, TV, nguo za wanafamilia, malipo ya wafanyakazi (house girl, house boy, mlinzi) n.k.

Mwanamke anachopata kitakuwa nyongeza tu. Ndio kanuni ilivyo hata kama analipwa mara tano Zaidi yako usimtegemee utakuja kulia kilio cha mbwa koko mdomo juu
Watakupinga hapa,, watakupiga mawe wakati Kuna vitabu vya kiimani vimetoa miongozo, wao wanashikiria mabadiliko ya kidunia........ Tunapokuja kwenye swala la maandiko hakuna cha mabadiliko ya kidunia maandiko yaheshimiwe

Ova
 
Ukweli ni kwamba hamtakiwi kukwama, kukwamwa kwa mwanaume ni uzembe wa hali ya juu. Yaani mwanaume unakwamaje kwa mfano[emoji134][emoji134][emoji134][emoji134][emoji134][emoji134]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Majukumu ya familia ni ya mwanaume tu kumbe? Ndo mana mwanaume akifa mwanamke anaishia kuliwa na kila mtu mana hajui kujitegemea
Ndugu unaniquote nimesema wapi hayo?mie nimeongeza volume tu
Isitoshe mwanamke ni kiumbe dhaifu,tegemezi,hajasoma,hana pesa wala chochote cha kumuingizia pesa sasa hayo majukumu unayotaka akusaidie wewe mume na asiwe tegemezi anayafanyaje?ama unaongelea majukumu ya kupiga deli,kuzaa,kufua,kupika ,kulea watoto na mumewe?
 
Watakupinga hapa,, watakupiga mawe wakati Kuna vitabu vya kiimani vimetoa miongozo, wao wanashikiria mabadiliko ya kidunia........ Tunapokuja kwenye swala la maandiko hakuna cha mabadiliko ya kidunia maandiko yaheshimiwe

Ova
Tena vitabu vya dini zote vimeandika hakuna dini inasema mwanamke ni kichwa cha familia. Kuwa kichwa ina maana ni kuongoza ustawi wa familia. Hata Wanyama wenyewe dume ndio linaongoza familia angalia nyani, simba, tembo, kuku na wengine wote kama wanaongozwa na majike.

Mwanamke kazi yake ni kulea na kuangalia watoto hiyo ndio nature ilivyo
 
Tena vitabu vya dini zote vimeandika hakuna dini inasema mwanamke ni kichwa cha familia. Kuwa kichwa ina maana ni kuongoza ustawi wa familia. Hata Wanyama wenyewe dume ndio linaongoza familia angalia nyani, simba, tembo, kuku na wengine wote kama wanaongozwa na majike.

Mwanamke kazi yake ni kulea na kuangalia watoto hiyo ndio nature ilivyo
Hawataki story za nature, wanasema dunia imebadilika,... Hawajui iliyobadilika ni dunia ila maandiko yamesimama palepale
 
Back
Top Bottom