Wanawake wa chachamaa bungeni, Kificho ikabidi asimame

Asha Rose Migiro amezoea kuteuliwa tu hajawahi kugombea jinga kabisa hili UN Failure.

Wanataka kuleta mambo ya Anna Makinda wajinga tu hawa.
 
Mwenyekiti amefanikiwa kuwatuliza, ngoja tusikie mama Anna anaongea
 
Leo na mimi nimo karibu kabisa ya Bunge la Katiba. Nafuatilia mjadala kwa ukaribu mno. Bunge husika sasa linapitisha kifungu kwa kifungu cha Rasimu za Kanuni za Bunge hilo. Tangu mjadala uanze, naziona dalili za siku 90 za Bunge hili kutotosha.Sababu ni kuwa kuna ubishano mwingine hauna wa maana unaoendelea humu Bungeni.

Wapo wanaobisha kuhusu kuwekwa wazi kwa Hati ya Muungano;wapo wanaotaka usawa wa kijinsia uzingatiwe katika uchaguzi wa viongozi wa Bunge la Katiba na Kamati mbalimbali za Bunge hili. Wanawake wanataka 50/50.Wanaume vivyohivyo.Wanawake wanaenda mbele 'kulazimisha' kuwa endapo Mwenyekiti atakuwa mwanaume,Makamu Mwenyekiti awe mwanamke au kinyume chake.

Kwa namna mambo yanavyokwenda Bungeni sasa,nauona ugumu wa makubaliano juu ya mambo mbalimbali kuelekea kupata Katiba mpya. Kwasasa Bunge limejaa vijembe,kelele,kebehi,na nyimbo. Hapa Bungeni,hapatoshi! Ni VUTA-NKUVUTE kweli kweli.Tuendelee kushuhudia na kusikia kinachoendelea.

Mzee Tupatupa wa Lumumba(sasa Dodoma)

 
Last edited by a moderator:
Hoja ya Wenje imejieleza vizuri sana na kwa hakika kama mwenyekiti angekuwa na busara basi angechukua hoja ya Wenje.

Hoja yenyewe ilikuwa ni kwamba, mwenyekiti, makamu mwenyekiti au kiongozi yeyote asichaguliwe kwa kuangalia jinsia yeke, bali uwezo wake.
 
ndio shida ya kujaza machangu bungeni, kwani wamekatazwa kugombea?

Hapo hata mie nashangaa, hakuna aliyenyimwa kugombea sasa zogo lote la nini??? Si wagombee na kama mtu anakubalika si atachaguliwa jamani khaaa..
 
Najaribu kuimagine wangechaguliwa hao wadada tu kwenye uongozi, sijui wanaume wangeichukuliaje hii.
 
nini msimamo wa wanawake wasomi kaka prof tibaijuka na Dr migiro?au na wao mule mule tu akina vicky kamata
 

Mambo ya jinsia ndio yanatukwamisha katika mambo mbalimbali....Watu wachaguliwe kutokana na uwezo.....
 
Kwa mwenendo huu wa hili bunge.. sidhan kama lengo litafikiwa, hawa wabunge walienda pale kwa mfano wa wabunge wa jamuhuri na matendo yao wakiwemo bungeni
 
Tunahitaji mwenyekiti na makamu mwenyekiti mwenye sifa haijalishi ni wote wanawake au wanaume isije ikawa kama wakati wa kutafuta spika wa bunge la jamhuri la muungano ambapo watanzania walitaka spika CCM wakamleta mwanamke na si spika.
 
Malima kasaidia kidogo, kasema upande wa visiwan ukitoa mwenyekiti mwanamke basi bara atoke makam mwenyekiti mwanamme na kinyume chake
 
hawa watu wanaboa watu wakubwa wanabehave kama watoto wa chekechea
 
Naona mwanasheria mkuu wa Zanzibar anazungumza kisheria zaidi simwelewi maana mimi si mjuzi ktk eneo hili
 
Tunahitaji mwenyekiti na makamu mwenyekiti mwenye sifa haijalishi ni wote wanawake au wanaume isije ikawa kama wakati wa kutafuta spika wa bunge la jamhuri la muungano ambapo watanzania walitaka spika CCM wakamleta mwanamke na si spika.

Umenena vyema kabisa.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…