Tanzania ni nchi ya Amani sana.Ukifanya biashara yoyote,au kazi yoyote ya ufundi,kama ufundi bomba,ufundi magari,ufundi pikipiki,bodaboda,mama lishe au baba lishe,ukiwa na genge la kuuza nyanya,machungwa,mboga mboga,matunda,zabibu au ushonaji wa nguo au kazi yoyote ile,unapata faida nzuri na muendesha maisha,kuliko kupoteza wakati kwa mambo ya kipuuzi.Kuna wanawake wengi,wako masokoni,wanajua bidhaa kwa bei ya jumla,na kuuza reja reja,na wanapata faida nzuri tu.
Kuna nchi nyingine,kama Sudan,Somalia, Liberia,Ethiopia Nigeria Yemen,huwezi kufanya biashara yoyote,kutokana na kukosa Amani,na nchi kuwa jangwa,hakuoti mazao yoyote.Tanzania ni nchi ya Amani,ndugu zanguni,vijana,wanawake,wazee zifanyieni kazi fursa za kibiashara,kilimo,ufundi,ufugaji.Kuna watu wapo masokoni,Wana mashine za kukujia nazi za umeme,mpaka jioni hakosi 50,000 mpaka 100,000.Tumieni fursa.Mbali ya wanaouza mifugo,kama kuku,mbuzi,ng'ombe,maziwa ya ngo'mbe, nk.