Wanawake wa JF mbona hamjibu Private messages?

Wanawake wa JF mbona hamjibu Private messages?

Nimeenda PM kwa wanawake 29, mmoja tuu ndio nilimwambia mambo akajibu "kwa yesu!" wengine wote wapo kimya, nioneeni huruma nahitaji upendo wenu, wadada wa jf nawapenda sana jibuni meseji.

Nipate hata mmoja wa kupiga nae story tam tam namimi najua kupenda haswaaa!!

Halafu nikionaga tuu jina la dada ya jf kuna kaharufu kananijia puani inaonekana muwasafi na wazuri na mna ladha nzuri sana, nahitaji kampani yenu.

Nyie ndio kimbilio letu hapa JF

Sent using Jamii Forums mobile app
kwani unadhani hao ni wanawake ? ni midume hiyo itakutafuna
 
Kimtu kinakuja kabisa kinakusalimia vizuri kabisa,
Unaweka mapozi pembeni unakijibu halafu kinakuchunia.! Ni kama kilikuwa kinakupima tu kama utamjibu ama la..!!

tukileta pozi mnatusema, tukiwa wastaarabu tukajibu mnaanza kutu take for granted.! Na tutawachunia mpaka mkome.!
Msitufanyie hivyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanaume wengi hawajielewi kabisa mtu anakuja pm badala ya salamu anaanza oyo uko pande za wapi? **
Hiyo hapo number nitafute whatsap utadhani alininunulie yeye simu **
Mara ooh wewe mrembo sana naomba picha sijui nani kamwambia kuwa nagawa picha

Lugha zenu sio nzuri kabisa !! Halafu wengi kujimwambafai kwingi wakati wanashindia mihogo .....** Badilikeni ....vingine mtakuwa mnakaushiwa sana ...na ukiona mwanamke mrembo jua huyo tayari ana mtu wake
Tafuta na ww wa kwako mtengeneze awe kama unavyopenda

Sent using Jamii Forums mobile app
Jina lako ndio linafanya wakutumie meseji kama hizo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo jamaa amenichekesha sana, yupo very straight.
Sema naona hapa tunachanganya mada, kuna mtu kumtafuta mtu kwa sababu ambayo haihusiani na mapenzi, na kuna kutongoza.

Kwenye kutongoza, huwa tunaanza mdogo mdogo, unamchekesha huku unawasilisha matatizo yako. Kama ni wa kukuelewa atakuelewa tu.

Ila hizi nyingine unataka msaada, wewe sema tu habari, halafu tiririka shida yako. Mbona tumesaidiwa na tumesaidia wengi kwa mtindo huo



Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Msitufanyie hvyo buanaa
Kimtu kinakuja kabisa kinakusalimia vizuri kabisa,
Unaweka mapozi pembeni unakijibu halafu kinakuchunia.! Ni kama kilikuwa kinakupima tu kama utamjibu ama la..!!

tukileta pozi mnatusema, tukiwa wastaarabu tukajibu mnaanza kutu take for granted.! Na tutawachunia mpaka mkome.!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ndio nzuri sasa mtu anakusalimia swali linalofuata uko wapi? Yaani ndani ya siku moja anataka kujua unaishi wapi, una miaka mingapi, unafanya kazi gani, una watoto wangapi. Watu wa namna hii hata nikiwajibu huwa wanajibiwa lolote linalokuja kichwani muda huo

Sent using Jamii Forums mobile app

Hahaha, inakuwa kama mlishajadili mwanzoni kwa hiyo mmefikia hapo.

Ngoja nireview PM yangu na Joanah nijue tulianzaje anzaje.
 
Muda mwengine watu wapo bussy na JF ina uzi mwingi kila muda unaingia so unaweza usione kama hujaangalia au kuweka notifications on. Pole sana
 
Back
Top Bottom