Nitakupa steps mpaka kufikia mahari
* KWanza binti (mchumba) wako ataenda kuwaambia wazazi wake kuwa amempata kijana na amempenda, angependa waoane. Kama ilivypo kawaida, wazazi watauliza maswali mengi na mengine yanaweza hata kumkatisha tamaa binti, hiyo ni kupima utayari wake, mambo kama kabila na mengine mengi.
* Baada ya hapo familia ya binti watahitaji kuonana na kufahamiana na upande wa kijana na hapo either watataka barua au mwakilishi toka kwa familia yako.Ukiamua kutuma barua, utahitajika kutuma mtu wa kuipeleka ukiweka kiasi kidogo cha fedha ndani ya hiyo barua..Ikiwa utahitajika kwenda, basi uwe na watu kama watano hivi, inawezekana baba na nduguzo wengine au close friends+wazazi(baba)
*Mkifika wewe utakaa nje na baada ya mda utaitwa, ukiingia binti(mchumba wako atakutambulisha) then mazungumzo yataendelea.
* Hatua ya kwanza ni kutoa kilo mbili za sukari na chai itapikwa right away na baada ya hapo utatoa shukrani kwa mama mtu, utampa mchumba nae ataongea maneno flani hivi ya kilugha afu atampa mamake, then yeye ataingia chumbani ili muongee kuhusu mahari
*Huwa mahari inayotolewa ni ng'ombe wanne, wawili wanaotembea na wawili in form of cash. Unaweza kunegotiate kama unaona wanakuminya..teh!
* Kingine utatakiwa kutoa asante kwa mama mtu, kwa kumtunza binti hadi kufikia umri wa kuolewa bila kukutana na mwanaume, yaani unatoa asante ya ubikra wa yule mchumba..... hii haijalishi kwamba ni bikra au sio! Kama alishazaa, hiyo asante huitopi.
* Mkishatoa mahari, sasa nyie mmekuwa wachumba rasmi na mambo ya mipango ya harusi inaanza
N.B Hutakiwi kutoa mahari yote kwa mkupuo, hiyo huonyesha dharau, niliwahi kuwafanyia kaka zangu na hayo ndo nnayojua.