Wanawake wa sasa hawahitaji akili kuishi nao, wanahitaji moyo mgumu

Thawabu ya kweli utaipata kwa kusaidia watoto yatima na wasio jiweza.acheni kujipa kazi ya uzazi kwa wakubwa wenzenu.....Kama baba yake na mama yake hakuwaelewa wewe Ni nani.....? Mwishowe mchapane makofi muanze kwenda kupeana maarifa kwa ocd na ustawi wa jamiii [emoji23][emoji23][emoji23] huo muda nunua gunia la viazi na mbuzi mmoja pela kwa watoto yatima nao waamke asubuhi na supu nzito.


Na hapo penye kujifanya nyie ndio waalimu wa kufundisha watu wazima hao wanawake ndipo wanapo chukulia point tatu muhimu......kwa akili yako unadhini huyo mwanamke anacho kifanya hakijui.....? Kwa kuwa yeye Ni punda au sio.....?[emoji2][emoji2][emoji2]
 
Vijana wana uoga Sana, hawatambui vipawa walivyojaaliwa na Muumba wao.
Hivi unajijua una Mambo 99 yanakungoja ukiachana na hilo moja la mwanamke ........muda Ni Mali mzee .....acha kujifanya wewe ndio mwalimu wa kuwafundisha watu wazima ambao wanajua kwenye hiyo ndoa wamefata nn.....?

Mtu kwenye ndoa kafuata pesa ...wewe utaanza kumfundisha kuwa pesa Ni za shetani sijui nini nini.....?

Kama ndio hivo wanawake wanakuchora tu huku wakisubiri muda wao ufike wa terminate mission waendelee mbelee . Wakuache ukilialia na uwalimu wako
 
Uoga unapitiliza yani kiasi ya kwamba sasa nahisi wanawake watatutawala mkuu
Wanawake wanaanza kukutawala ukianza kuonyesha mwenyewe hujiamini.

Mwanaume unaejiamini huwez kuogopa kudate na mwanamke yeyote uliempenda.

Ukianza kuwaogopa Sana wanawake hata majukum ya kuwahudumia utaona Kama unaonewa.

Kumbe ni wajibu wako mwenyewe Unapaswa kumhudumia mwanamke wako.

Asilimia kubwa ya Wanaume wasiojiamini ndo wale wanaokimbia MAJUKUMU yao na kuanza kuipigia hesabu pesa ya aliyoitolea jasho mwanamke wake.
 
Acha kuwa karirisha watu eti kumu endekeza mwanamke mjinga ndio uwanaume [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] huo Ni uboya Kama uboya mwingine . Uwanaume Ni kutambua kuwa hapa sipo sehemu sahihi kuwepo. Nahitaji kuwa sehemu Fulani nikifanya jambo Fulani kwa ajiri fulani.

Sasa Kama unazani ulikuja duniani kuja kuwaendekeza wanawake ongeza juhudi.......ila nakukumbusha pia "Mzazi mwenye hekima huacha urithi hado kwa watoto wa watoto zake" Sasa wewe Kama unadhani utarithisha hayo malumbano yako yasiyo na kichwa Wala miguu kwa hao wanawake wako sawa ......
 
Kwa mwanaume anayetaka amani ya moyo na utulivu wa nafsi na kuondoa migongano katika mahusiano basi bado atahitaji akkli kyishi na mwanamke.

Kama mwanaume bado ni mtu asiyejali amani ya moyo na ambaye hajali migongano yani ni mwanaume asiyejali shari basi anahitaji moyo mgumu tu kuishi nae.

Ukiishi na mwanamke kiugumu ugumu unazingua kweli yani.

Ndio maana dini ikaruhusu uongo katika ndoa wenye lengo LA KUTENGENEZA NDOA IDUMU ZAIDI NA KUEPUSHA MIGONGANO.

Kuna siku nilipewa off kibaruani,basi niliporudi wife akaniuliza mbona mapema nikamuambia "nimeomba ruhusa kwa bosi kuwa mke wangu anaumwa lkaini najua huumwi ila tu nimekumiss kweli sijui kwa nini"

Kuna jambo alinuna lakini nipomuambia hivi akafurahi akaanza story zingine
 
Hawa wanadhani kutolerate bullshit ya this other gender ndio uanaume..

Hafai, muache tafuta mwingine

Hawa ndio wale hadi wanaanza kupiga wanawake.... instead of beating her leave her as a widow. Huo ndio ugentroman sasa[emoji23][emoji23]

Sent from my SM-G950F using JamiiForums mobile app
 
Badilika mkuu,
kua na mtazamo chanya juu ya wanawake.

Uyo mwanamke Unaweza wewe shindwa kuendana nae, akapata mwingine wakaendana Safi kabisa.

Tena mtu akakakushangaa ulikwama wapi mkuu[emoji2]

Lilotokea kwako kwa uyo mwanamke wako,

Haliwez kugeneralize kitakachotutokea wanaume wengine kwa uyo mwanamke wako.

Apo mjinga Ni wewe ulieshindwa kumtuliza kiumbe unayemmudu KWENYE himaya yako.
 
Kwa hiyo unataka kusema kuwa uliacha kazi ukaondoka ili ukamfurahishe mwanamke nyumbani kisa kajinunisha[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] sawa bana nimekuelewa
 
Kama Mimi nimewahi leta uzi humu wa kulialia kuhusu kutendwa na wanawake basi nitaacha [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]


Kwa taarifa yako Mimi wanawake kwangu wapo chini yangu hakunaga mjanja wa Alie fanikiwa kuniendesha . Sio kusema sijawahi toswa no nilitoswa na nikaumia na kupondeka vizuri tu ila kipondo kile kiliniimarisha na kunifanya niwe makini Sana na hizi safari za mapenzi .Kama ujuavyo tunaumia ili kujifunza sio kulegea .

Tafuta nyuzi zangu utaelewa nincho maanisha
 
Kwa hiyo unataka kusema kuwa uliacha kazi ukaondoka ili ukamfurahishe mwanamke nyumbani kisa kajinunisha[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] sawa bana nimekuelewa
Sikupingi, ila
Inaonekana umetumia Nguvu kubwa Sana kuisoma comment ya jamaa,

mwisho wa siku hamna ulichoelewa.

JAMAA YUKO CLEAR KABISA,[emoji106]

Ukiachilia changomoto alizokua nazo, KATUMIA AKILI sana KUEPUSHA MIGOGORO NA KUJENGA furaha na UPENDO NA MWENZIE.

Na Apo anatufikishia ujumbe wa kua na kifua Cha kiume,
kuweza kuhimili Changamoto nzito na still ukabaki normal.

Pia kutokuleta stress zako za kazini KWENYE mambo ya kifamilia.

INSHORT, comment ya jamaa imekaa ki-Gentleman Sana.
 
Sijapingana na wewe,
ila nmekusihi TU ubadilishe saikolojia yako khs Hawa viumbe.
 
Waheshimuni wanawake umekuja/umeletwa duniani kwa kupitia mwanamke iweje leo unawadharau, heshima na upendo unaomuonyesha mama yako mzazi itumike hata kwa wanawake wengine kumbuka amri kuu ya mungu ni upendo. 'Pendaneni' na tunda tunda la roho ni upendo kama hujaoa au haupo kwenye ndoa ngumu sana kumeza.

Binti mrembo au mwanamke yeyote unaemdharau leo ndio mama mzazi mpendwa wa kijana furani huko mbeleni kama vile wewe unavyompenda mama yako naamini ukimuuliza mwanaume yeyote anaekubaliana na mtoa post upendo wake mkuu upo kwa mama yake.

Ishi na mwanamke kwa akili anaelewa maana halisi ya msemo huu na aelewe.
 
Kwa hiyo unataka kusema kuwa uliacha kazi ukaondoka ili ukamfurahishe mwanamke nyumbani kisa kajinunisha[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] sawa bana nimekuelewa
Umakini wako katika comment yangu umepotea.

Nimesema nilipewa off kibaruani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…