Halafu kama wewe ndo umeachwa anakurudishia simu. Anakuambia "kwani unaniumbua sumbua nini, sitaki unipigie simu, au kwakua ulininunulia hili kopo lako nawe waliita simu..eeh?? chukua takataka yako" Hapo ashanunuliwa simu mpya, muda si mrefu kama miezi mitano itapotea au kunyang'anywa. baada ya siku mbili baada ya kunyang'anywa utasikia simu inaita. Mara "mambo? siku hizi umenisusa kweli, hata simu hupigi?
Mwenzio nipe pole, simu yangu nimeibiwa hapa nilipo nina hasira kama nini. Huna simu ambayo huitumii uniazime kwa siku mbili tatu'. Makubwa!. mia