Ni kweli ukiolewa uwezekano wa kutoboa sana ni mdogo unless umpate mume muelewa sanaaa, sio hawa wetu ambao ukimzidi elfu5 tu tayari umetangaza vita.
Lakini pia unajua mafanikio ya mwanamke tangu anapokuwa mdogo ni ndoa. Ndio maana mara nyingi kukuta mwanamke anafanya maendeleo binafsi akiwa hayupo kwenye ndoa ni nadra sana.
Kuna yule anayeona sio jukumu lake ataolewa na mwanaume mwenye pesa then atapata maendeleo.
Wa pili ni yule anayeona akifanikiwa sana atakosa wa kumuoa as wanaume watamuogopa. Kwakuwa akili zetu ziko centred kwenye ndoa ndio maana wanaume wanajiona miungu watu juu yetu.
Hapa mie naona mtoa mada anatishwa na maendeleo ya wanawake as anatambua tukitusua basi ile dhana ya wao kututawala itadidimia mwisho kufa.
Sent using
Jamii Forums mobile app