Wanawake wakiwa kwenye siku zao(Hedhi) wanakuwa hatari kwenye mazao na watoto wachanga!

🤣🤣🤣🤣🤣🤣. Loooh utajua mwenyewe kama nakula au sili. Ni hivi hedhi sio uchafu bali ni kitu cha kujivunia kwangu mimi kiumbe mwenye jinsia ya kike,sisi wote hapa duniani tupo kwa sababu kuna viumbe wana mzunguko wa hedhi ambao ndio wanatubeba tumboni na kutuzaa. Kama bado una mawazo ya kijima ya kuchukulia hedhi kama kitu kibaya au kichafu au cha kukera poleee.
Mwili hutoa uchafu nje ndio mechanism ya mwili ilivyo, wote sisi ni uchafu wa mwili, km ingekua hivyo hata wewe mpaka leo ungebakia tumboni km ni msafi visafi vinabakia na mwili vichafu muda wa kutoka ukifika vinatoka au la mwili unapata hitilafu, hujiulizi kwanini ukikosa siku zako hua unaanza kuzitafuta unazikosaje na kwanini uzikose?
 
Hizo imani potofu kuna shule ya secondary ya mabinti wanalima bustani za mboga na kuna kuku wa mayai. Hizo mboga hazikauki ndio wanakula na siku za Jumapili huwa wanauza kwenye kanisa
 
Wewe we mtoa mada umejaribu mara ngapi mpaka useme una uhakika, au umeona x1 tu ndo uamini jaribu angalau x3
 
Mwili hutoa uchafu nje ndio mechanism ya mwili ilivyo, wote sisi ni uchafu wa mwili, km ingekua hivyo hata wewe mpaka leo ungebakia tumboni km ni msafi visafi vinabakia na mwili vichafu muda wa kutoka ukifika vinatoka au la mwili unapata hitilafu, hujiulizi kwanini ukikosa siku zako hua unaanza kuzitafuta unazikosaje na kwanini uzikose?
Zisipokuwepo nazitafuta kwa sababu ni za thamani sanaa yaani za thamani mnoo, sio kwa sababu eti ni uchafu ,damu ya hedhi ni kiashiria kwamba mimi ni mwanamke niliyekamilika kuanzia ubongo,ovaries hadi uterus. Halafu mkuu, kwenye topic ya mfumo wa utoaji taka mwili, kwenye zile taka zilizoorodheswa damu ya hedhi haipo. So usiseme damu ya hedhi ni uchafu eee.
 
Hizo imani potofu kuna shule ya secondary ya mabinti wanalima bustani za mboga na kuna kuku wa mayai. Hizo mboga hazikauki ndio wanakula na siku za Jumapili huwa wanauza kwenye kanisa
Mwenyewe shuleni kwetu tulikuwa tunalima mboga na tulikuwa wasichana pekee na hakuna siku mboga zimenyauka,labda kama waseme inastawisha maana mboga zetu zilikuwa zimestawi hadi rahaaa.
 
Zisipokuwepo nazitafuta kwa sababu ni za thamani sanaa yaani za thamani mnoo, sio kwa sababu eti ni uchafu ,damu ya hedhi ni kiashiria kwamba mimi ni mwanamke niliyekamilika kuanzia ubongo,ovaries hadi uterus. Halafu mkuu, kwenye topic ya mfumo wa utoaji taka mwili, kwenye zile taka zilizoorodheswa damu ya hedhi haipo. So usiseme damu ya hedhi ni uchafu eee.
Ushawahi sikia Mwanamke wa kiislamu anapiga azana au anaswalisha msikitini? Siitaki kuingia sana kwenye imani za kidini ila elewa ulichoambiwa
 
Kwa hiyo mama anayenyonyesha akiwa kwenye hedhi asimguse mtoto? Kuna wamama wafanya kazi/biashara anamwacha mtoto na dada wa kazi, kwa hiyo dada akiwa hedhi mama haendi kazini na mama akiwa hedhi mtoto hanyonyi au mnadhibiti vipi?
 
Watakwambia mama akiwa kwenye siku zake asinyonyeshe mtoto atanyonya uchafu
 
Ni kweli kabisa!

Ukienda mbali sana kwenye KAZI Fulani za kipato,na mkeo aka cheat huku nyumbani,mambo Yako Huwa magumu na kuharibika hata pesa utakayoipata haitikua na impact yoyote!

Kama ni muindaji unaweza kuumwa na nyoka au kushambuliwa na wanyama wakali!!

Kuna positive na negative energy ambayo huachiliwa kwenye mambo Halisi kwenye maisha kwa situation Fulani Fulani za watu!!
 
Back
Top Bottom