Wanawake wakiwa kwenye siku zao(Hedhi) wanakuwa hatari kwenye mazao na watoto wachanga!

Wanawake wakiwa kwenye siku zao(Hedhi) wanakuwa hatari kwenye mazao na watoto wachanga!

Nimekosa namna ya kuweka Heading vizuri. I'm sorry 😔.

Kwa uelewa wangu na uzoefu wangu Hadi nimefikia hapa nilikuta dhana kama hizi

Mwanamke akiwa hedhi akiingia kwenye shamba la nyanya ama nyanya chungu mazao hayo huathirika na kuharibika shamba Zima hili ni kweli 💯

Pia mwanamke akiwa katika Hali hiyo akishika mtoto mchanga huyo mtoto hugua maupele Fulani wao huita mazam zam. Sijui huko huitaje.Hii Huwa nasikia wamama wakisema. Na dawa mtoto huvalishwa shilingi kiunoni Hadi yatakapoisha ukimuacha hata kaa yaishe Hadi uzeen wake wote haponi!

Dhana hizi zipo nyingi sehemu na sehemu Mimi Kwa sababu ni mkulima hiyo ya kwanza ni kweli kabisa kabisa.

Maana Kuna kipindi alikuja dada kununua nyanya shambani alikuwa mfanya biashara mkubwa tu akakataa kuingia shambani baada ya kumbana sana akasema yupo kwenye Hali hiyo.

Nikamwambia hizo ni dhana potofu tu ingia shambani tuvune wote hapa hatuna miiko hiyo!

Baada ya siku3 mbele nyanya zilianza kuoza sijawahi ona piga dawa hapa na pale lakini wapi.

Ilifikia hatua hatujazi hata ndoo1 ya nyanya nzima ambayo Haina shida!

Hapo ndo nikajua ndio maana hata kwenye maandiko Mungu Jehova alikataza wanawake kushika kitu chochote kilicho kitakatifu ama kuingia hekaluni akiwa kwenye hedhi!

Naomba kuwasilisha kwenu ninyi wanasayansi ni kwanini hutokea hivyo Kuna uhusiano Gani kati ya vichache hivi nilivyotaja na hedhi ya mwanamke kisayansi?
Hizo dhana hazina ukweli wowote. Ila ni vizuri kwa jamii kuamini kwa vile lengo lake ni kumlinda mwanamke mwenyewe na kutunza heshima yake akiwa kwenye hedhi.
 
Tunaongelea hedhi na sio mwanamke kucheat.
Ni kweli kabisa!

Ukienda mbali sana kwenye KAZI Fulani za kipato,na mkeo aka cheat huku nyumbani,mambo Yako Huwa magumu na kuharibika hata pesa utakayoipata haitikua na impact yoyote!

Kama ni muindaji unaweza kuumwa na nyoka au kushambuliwa na wanyama wakali!!

Kuna positive na negative energy ambayo huachiliwa kwenye mambo Halisi kwenye maisha kwa situation Fulani Fulani za
 
Hakuna uhusiano wowote wa kisayansi kati ya mwanamke kuwa kwenye hedhi na kukauka au kuharibika kwa mazao. Jambo hili ni imani potofu na utamaduni uliopitwa na wakati ambao umekuwepo kwenye jamii nyingi duniani kwa karne nyingi.

Chimbuko la Imani Hii
Kihistoria, tangu enzi za waroma wa kale (kama ilivyoandikwa na mwanahistoria Pliny the Elder), damu ya hedhi ilionekana kuwa na "nguvu za kichawi" zinazoweza kukausha mimea, kufanya nyuki wakimbie mizinga, au hata kufanya visu viwe butu.

Katika jamii nyingi za Kiafrika, miiko hii ilitumiwa kama njia ya kuwatenga wanawake wakati wa siku zao kwa kuwa walionekana "sio wasafi".
Ahsante sana
 
Unajuaje kama mwanamke yuko kwenye hedhi? au kuna utaratibu mpya inabidi wawe wanatoa taarifa?

Kwahiyo mama ukiwa na kichanga chako na uko period inabidi ukigawe kwa muda mpaka utakapomaliza au hii inaathiri wanawake wengine na siyo mzazi wa mtoto?

Hakuna kitu kama hicho, mimi wiki mbili zilizopita nilikua shambani kwangu na niko period mpaka leo hamna kitu kimeoza wala kuharibika, ni imani potofu tu!

Hebu share hayo maandiko kaka, mimi najua walutheri na wakatoliki hawabagui mtu kuingia kanisani wala kutumika madhabahuni kwa kigezo cha hedhi, Jehova amesema wapi kwamba tusiingie mahekaluni?

Hakuna uhusiano 💯
Hakuna ulichojibu hapa.
 
Hizo imani potofu kuna shule ya secondary ya mabinti wanalima bustani za mboga na kuna kuku wa mayai. Hizo mboga hazikauki ndio wanakula na siku za Jumapili huwa wanauza kwenye kanisa
Katika hao walimu walezi wao wanajua kilakitu na namna ya kukinga.

Mimi siwezi Pingana hapa ingawa liliwahi kunitokea na Hadi sasa naweka Kinga sitakaa naiche kuweka Kinga Kwa hasara niliyopata kipindi kile!

Bila shaka kama ni Imani potofu Wacha mi niendelee kuamini ni kweli maana nilipata hasara na tangia hapo sijawahi pata changamoto hiyo tena
 
Back
Top Bottom