Wanawake wana visirani sana ila huyu wa leo kazidi

Wanawake wana visirani sana ila huyu wa leo kazidi

Mwanaum
Tupo tunasafiri, kuna mdada mmoja mzuri, body si haba na kavaa smart kabisaaa, Wakati yupo chini konda akamuomba jina ili amuandikie tiketi.

Ninukuu baadhi ya majibizano, sio yote kisa ni kirefuu.

Akajibu "Niache nitulie andika hao wengine"

Akaachwa, tupo ndani konda akamfuata akamuambia naomba nitajie jina mbele kuna traffic na wewe umekaa mbele anaweza ashtukie tiketi iwe faini.

Akajibu "Wee naweee, haya andika..."

Alitaja jina moja tena la kiume, konda akumuomba jina la pili.

Akajibu "Andika hilo, kama hutaki acha"

Konda akaandika, akamuoma jina la mwanae angalau mmoja maana wamekaa kwenye siti ili nalo liandikwe kwenye ticket yao,

Akajibu "Wanangu majina yao sio ya kukaa kwenye magazeti..... braa braa na maneno mengi nishasahau"

Akaulizwa "mbona wewe msumbufu sanaa wenzako wameonesha ushirikiano hili ni jambo la kawaidaa

Akajibu "wao ni wao mimi nina taratibu zangu, wengi waoga"

Hapo ndio watu wakacharukwa, majibishano yakawa makubwaa, mimi nilikua nimekaa naye, mwenyewe nina mambo yangu nimevurugwa kuepuka mavurugo, nikamwambia

Ngoja mimi niende pale wanao waje hapa ukae nao,
(wakati anakata ticke mi nilishawahi ile siti hakupata duble).

Akaanigeuzia mimi ( "Yaani umenionaje? Kwa nn mda wote usiseme? Mi nakupigia kelele hapa? Nanuka?)

Sikumjibu nikaweka earphones nikaegamia zangu dirishani (nikaomba tuu hapa asije akatuma tusi tu) akageukia wengine, kila anayemuongelesha anapita naye kwa kila lugha chafu.

Watu wakasema kama vipi ashushwe asituletee nuksi humu, akasemaa,"nani anishushe...? Kwa kosa ganii...? hakuna anayenijua humu ulizieniii"

Gari ikasimama kweli, mimi nikawa nawaza huyu kashanitibua nimtetee?

Nikasema haina haja mtu mwenyewe kwa mawasiliano tuu aliyokua akifanya ni kama ana matatizo nyumbani.

Nikashauri "huyu tukimshusha katikati huku jua hili na watoto wadogo ni hatari hasa kwa hivi vitoto", wapo 3 kimoja kichanga.

Akanigeukia, "wewe ndio una akili akilituu sijui ulikua wapi wengine maboksi"

Daa nilichoka, dereva akafunga blek akaamka aje kumzibua, watu wakamzuia, tusije pata mikosi.

Akaanza "hamna wa kunigusa hapa wala mwenye hela ya kunishusa, hii gari nimepanda tu, ila ningekua na uwezo wa kuja na gari yangu ila sababu ya huyu mtoto mdogo, Hata kukodi sishindwii".

Mzee mmoja akawa kama kamaindi hivi, akamuuliza

"Una hela wewe, hivi unajua pesaaa? Yaani, yaanniii....."

ikawa kama mtu flani ile kauli imemuuma anataka aprove kama hana pesa wenye pesa wapo kimya ila anshindwa kumalizia.

Akamuambia konda, tukifika kituoni tunamshusha nitamlipa hela zake asitupigie kelele, halafu ampigie yeyote anayedai anamfahamu.

Akasema, "hamna wa kunishusha" ,akaambiwa
"wewe nakulipia nauli yako, wanao wote siti, hela ya kula, kulala, dharura na inabaki".

Tumefika mzee alitoa bunda akamuuliza unashuka hushuki, akasema sishukiii, Kugeuka nyuma kuona bunda iliyoshikwa, akageuka akawambia "wanangu amkeni nimechoka hizi kelele" akapewa akamtuma mwanae aje kuzipokea, alivyomfikia tuu akazikwapua akaweka kwenye pochi.

Wote tulichokaa, kwanza tulijua atakataa, alishuka fasta hakuongea kitu tena tukamuona anaongea na konda wa gari nyingine inayoenda tulikotoka kama vile anataka kurudi, kwa ufupi ilikua ni maneno mengi ya kukera mengi nimesahau na hivyo niliamua kusikiliza mziki, kuna jama wa watu alimuwakia kwa kumuangalia tuu.... ila mwisho ikawa hivyo.

Sisi tukasepaa.
Mwanaume mwenzangu km alikuwa hayupo nyumbani,basi hiyo fedha aliyo pewa huyo Delilah karudia vitu vyote vya ndani,pengine kaacha godoro tu na kusepa.

Maana kwa kiburi chake katimuliwa,kwenye bus nako katimuliwa. Sijui kwao atapokelewa?
 
Sawaa, na kama sikoseni, pia unamanisha hio inaweza ikawa ni hali ya kuja na kupita, kwahio yeyote ukamkuta katika moment kama hio tunaweza jumuisha ana matatizo ya akili.
Nakuelewesha tena kuhusu Afya ya Akili,
Kama ilivyo kwenye Mwili, unachoka, unapata vihoma homa unapona, ila kuna magonjwa mengine yanakua makubwa na kupelekea kifo kama Kansa, Figo, n.k

Basi na Akili ni hivyo hivyo, kuna muda unaweza ukasongwa na jambo ukapata mawazo (stress) ukatetereka ukakosa usingizi vizuri, ila ukimalizana na hilo jambo unarudi kua sawa mfn, kuandaa research huku unakimbizana na deadline,

Kuna muda unakua na mambo zaidi ya moja, stress ya kazi, mapenzi, familia, biashara, n.k hii inaitwa msongo wa mawazo (depression) sasa kwa kua ni muunganiko wa vitu vingi hata kuondoka kwake itachukua muda, lakini pia isipoondoka kwa haraka itazalisha ugonjwa wa akili na hata kifo,

Kwa hiyo yes, tatizo la Afya ya Akili linamkumba kila mtu, litakuchukua vipi hiyo inatokana na ukubwa wa tatizo na uharaka wa kupata tiba.
 
Maisha yana mengi sana, huenda anapitia mengi magumu yanayohitaji msaada. Japo pia sio sawa kutukana wapi hovyo hata kama una matatizo binafsi.

Ila watu wanapitia magumu me gi, kiuchumi, kiafya, kimahusiano na kijamii.
Nakazia hapa
 
Ukiona mtu wa hivyo jua anakumbwa na mengi Sana Kwenye maisha yake,ikiwemo ugumu wa maisha yenyewe
 
Shida ya akili wapi mbona kaona pesa kiranga chote kimemuisha.Inshort alitaka apigwe apate advantage ya kulipwa bahati nzuri Mzee akashtukia mchezo[emoji1787]
 
amakweli rizki ya mbwa i miguuni mwake! yaani mwanamke kapata kibunda kimasihara masihara tu
 
Huenda kuna jambo gumu kuhusu mahusiano. Mtaani kwetu kuna mdada ni single-mother. Anao watoto wake kadhaa, aisee! Zimefyatuka kweli.
 
nilishawahi kuwa kwenye mahusiano na kichwa kimoja. Huyu akasome. Picha linaanza akiwa anaongea na Mama yake mzazi kwenye simu unaweza usiamini utasikia 'Mama Raja siku hizi anamk...u huoo yaani anakuwa wanamgongajee?'.
Huwa natamani sana kuleta uzi juu yake ila nahofia kumdhalilisha(siwezi).
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Umenikumbusha kisa kimoja kwenye daladala (eicher) za kivukoni-kinyerezi.

Kuna dada askari alipanda gari ikiwa ishajaa, basi pale mlangoni nadhani alikanyaga mtu, yule mtu kumwambia umenikanyaga askari akajibu kunya. Dada aliekanyagwa nae akawaka ukawa mtifuano na watu wengine kuingilia. Katikati ya mabishano askari akaanza kujinasibu eti unajijua mimi wewe, unajua mimi ni nani.

Aloo gari zima lilimgeukia yeye na hicho kipindi Magu katoka kuingia ikulu, walimuwashia moto askari, tukujue ili iweje, wewe ni njia, wewe unatujua sisi ni kina nani, kwanza raisi hayo mmambo kayakataza we unasema kama nani mpaka alishukia njiani yule dada.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] watu mbna vitukooo lol
 
afu wakiwaga kwenye usafiri ndo wanakuwa wehu kabisa sijui huwa ni kwanini,huwa natamani kununua ugomvi

Kuna mmoja aliwah mung'ata kijana kisa kakatalia kwenye siti yake
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kuna kisa nilicheka sana kwenye hizi dadadala(eacher).
Kuna maza mmoja mtu mzima sana miaka kama 50+ sema ana mwili wa mazoezi ko kidogo yuko skanganga, alikanyagwa bahati mbaya na binti wa kama miaka 26 hivi.

Yule maza alivyokanyagwa kwenye purukushani za kugombea siti alikausha tu. Purukushani zilivyotulia alimfata yule dada(alikua siti ya nyuma yake), akamfinya mkononi(kwenye msuli hapa).
Dada: kheeeh we mama vipi mbona unanifinya

Maza: we ulivonikanyaga ulihisi utamu eeh

Dada: sa ndo unifinye, hujui nimeumia, mbona hujiheshimu we mama

Maza: nijiheshimu kwako wewe kitoto kidogo nakuzaa huku nakimbia..

Raia ikabidi wamtulize binti maana show ya maza ilikua si ya kitoto.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nimekumbuka kitu nachekaa hadi machozii.
 
Back
Top Bottom