Wanawake wana visirani sana ila huyu wa leo kazidi

Tupo tunasafiri, kuna mdada mmoja mzuri, body si haba na kavaa smart kabisaaa, Wakati yupo chini konda akamuomba jina ili amuandikie tiketi.

Ninukuu baadhi ya majibizano, sio yote kisa ni kirefuu.

Akajibu "Niache nitulie andika hao wengine"

Akaachwa, tupo ndani konda akamfuata akamuambia naomba nitajie jina mbele kuna traffic na wewe umekaa mbele anaweza ashtukie tiketi iwe faini.

Akajibu "Wee naweee, haya andika..."

Alitaja jina moja tena la kiume, konda akumuomba jina la pili.

Akajibu "Andika hilo, kama hutaki acha"

Konda akaandika, akamuoma jina la mwanae angalau mmoja maana wamekaa kwenye siti ili nalo liandikwe kwenye ticket yao,

Akajibu "Wanangu majina yao sio ya kukaa kwenye magazeti..... braa braa na maneno mengi nishasahau"

Akaulizwa "mbona wewe msumbufu sanaa wenzako wameonesha ushirikiano hili ni jambo la kawaidaa

Akajibu "wao ni wao mimi nina taratibu zangu, wengi waoga"

Hapo ndio watu wakacharukwa, majibishano yakawa makubwaa, mimi nilikua nimekaa naye, mwenyewe nina mambo yangu nimevurugwa kuepuka mavurugo, nikamwambia

Ngoja mimi niende pale wanao waje hapa ukae nao,
(wakati anakata ticke mi nilishawahi ile siti hakupata duble).

Akaanigeuzia mimi ( "Yaani umenionaje? Kwa nn mda wote usiseme? Mi nakupigia kelele hapa? Nanuka?)

Sikumjibu nikaweka earphones nikaegamia zangu dirishani (nikaomba tuu hapa asije akatuma tusi tu) akageukia wengine, kila anayemuongelesha anapita naye kwa kila lugha chafu.

Watu wakasema kama vipi ashushwe asituletee nuksi humu, akasemaa,"nani anishushe...? Kwa kosa ganii...? hakuna anayenijua humu ulizieniii"

Gari ikasimama kweli, mimi nikawa nawaza huyu kashanitibua nimtetee?

Nikasema haina haja mtu mwenyewe kwa mawasiliano tuu aliyokua akifanya ni kama ana matatizo nyumbani.

Nikashauri "huyu tukimshusha katikati huku jua hili na watoto wadogo ni hatari hasa kwa hivi vitoto", wapo 3 kimoja kichanga.

Akanigeukia, "wewe ndio una akili akilituu sijui ulikua wapi wengine maboksi"

Daa nilichoka, dereva akafunga blek akaamka aje kumzibua, watu wakamzuia, tusije pata mikosi.

Akaanza "hamna wa kunigusa hapa wala mwenye hela ya kunishusa, hii gari nimepanda tu, ila ningekua na uwezo wa kuja na gari yangu ila sababu ya huyu mtoto mdogo, Hata kukodi sishindwii".

Mzee mmoja akawa kama kamaindi hivi, akamuuliza

"Una hela wewe, hivi unajua pesaaa? Yaani, yaanniii....."

ikawa kama mtu flani ile kauli imemuuma anataka aprove kama hana pesa wenye pesa wapo kimya ila anshindwa kumalizia.

Akamuambia konda, tukifika kituoni tunamshusha nitamlipa hela zake asitupigie kelele, halafu ampigie yeyote anayedai anamfahamu.

Akasema, "hamna wa kunishusha" ,akaambiwa
"wewe nakulipia nauli yako, wanao wote siti, hela ya kula, kulala, dharura na inabaki".

Tumefika mzee alitoa bunda akamuuliza unashuka hushuki, akasema sishukiii, Kugeuka nyuma kuona bunda iliyoshikwa, akageuka akawambia "wanangu amkeni nimechoka hizi kelele" akapewa akamtuma mwanae aje kuzipokea, alivyomfikia tuu akazikwapua akaweka kwenye pochi.

Wote tulichokaa, kwanza tulijua atakataa, alishuka fasta hakuongea kitu tena tukamuona anaongea na konda wa gari nyingine inayoenda tulikotoka kama vile anataka kurudi, kwa ufupi ilikua ni maneno mengi ya kukera mengi nimesahau na hivyo niliamua kusikiliza mziki, kuna jama wa watu alimuwakia kwa kumuangalia tuu.... ila mwisho ikawa hivyo.

Sisi tukasepaa.
si ukute amevurugwa, kafukuzwa na bwana anaondoka na watoto, ana hasira, yeye naye ni mwanadamu anaweza kureact vile kulingana na mazingira.
 
Pesa alipokea ndani ya gari na kuanzia pale akaa kimya, kumbuka alikua alikua ana react kwa kila kile.., iweje tuu achukue watoto akae kimya baada ya pesa?
Mbona kama unarudia maswali ambayo nilishakujibu?

"Inawezekana tatizo lake la akili lilitulizwa na Pesa,
Mtu mwenye tatizo la Afya ya Akili hua kuna kitu kina trigger anaripuka na hua kuna kitu kina mcalm down,

Kwa kua hatujui historia yake tunaweza kusema labda Pesa ndio ilimcalm down"
 
Lakini pia umemlisha maneno mtoa mada,
Hakusema yule Mama alivyopewa tu Pesa alikaa kimya, narejea andiko lake,

"Tumefika mzee alitoa bunda akamuuliza unashuka hushuki, akasema sishukiii, Kugeuka nyuma kuona bunda iliyoshikwa, akageuka akawambia "wanangu amkeni nimechoka hizi kelele" akapewa akamtuma mwanae aje kuzipokea, alivyomfikia tuu akazikwapua akaweka kwenye pochi.

Wote tulichokaa, kwanza tulijua atakataa, alishuka fasta hakuongea kitu tena tukamuona anaongea na konda wa gari nyingine inayoenda tulikotoka....."

Je hapo ni wapi Mtoa mada alionesha kua yule Mama alikaa kimya baada ya kupokea pesa? Bali Mtoa mada anasema alizikwapua kutoka kwa mtoto wake na kushuka fasta.
 
Umenikumbusha kisa kimoja kwenye daladala (eicher) za kivukoni-kinyerezi.

Kuna dada askari alipanda gari ikiwa ishajaa, basi pale mlangoni nadhani alikanyaga mtu, yule mtu kumwambia umenikanyaga askari akajibu kunya. Dada aliekanyagwa nae akawaka ukawa mtifuano na watu wengine kuingilia. Katikati ya mabishano askari akaanza kujinasibu eti unajijua mimi wewe, unajua mimi ni nani.

Aloo gari zima lilimgeukia yeye na hicho kipindi Magu katoka kuingia ikulu, walimuwashia moto askari, tukujue ili iweje, wewe ni njia, wewe unatujua sisi ni kina nani, kwanza raisi hayo mmambo kayakataza we unasema kama nani mpaka alishukia njiani yule dada.
 
afu wakiwaga kwenye usafiri ndo wanakuwa wehu kabisa sijui huwa ni kwanini,huwa natamani kununua ugomvi

Kuna mmoja aliwah mung'ata kijana kisa kakatalia kwenye siti yake
 
Mbona kama unarudia maswali ambayo nilishakujibu?

"Inawezekana tatizo lake la akili lilitulizwa na Pesa,
Mtu mwenye tatizo la Afya ya Akili hua kuna kitu kina trigger anaripuka na hua kuna kitu kina mcalm down,

Kwa kua hatujui historia yake tunaweza kusema labda Pesa ndio ilimcalm down"
Ahaaa hapo umejibu sasa, All Squared.
Inawezekana tatizo lake la akili lilitulizwa na Pesa,
Mtu mwenye tatizo la Afya ya Akili hua kuna kitu kina trigger anaripuka na hua kuna kitu kina mcalm down,

Kwa kua hatujui historia yake tunaweza kusema labda Pesa ndio ilimcalm down.

Sasa Dr. Hiki si ilikua kitu cha kueleza tuu mwenyewe bila kuulizwa,
 
Ahaa kule ndio kuna chanzo
Hii ndio comment niliyo i quote na wewe ndio ukaiingilia

"hakuna ata mmoja wenu alijaribu kufahamu anasumbuliwa na nini hadi yeye kufanya au kujibu hivyo.

Ukute kuna tatizo binafsi limenfanya asafiri. Umeishia kuhukumu tuu mkuu"

Mimi nika mjibu

"mtoa mada kama sikosei kaandika ya kua ali note kupitia mawasiliano yake kabla, ya kua ana matatizo ndio maana akajiwa na nia ya kumsaidia na kweli alisaidia kwa mawazo lakini pia kukaa kimya, nampongeza kwa utulivu, mwingine angemkaba koo..... oohoooo"

Kumbe mimi nilimquote huyu sbb alikua kama amemlaumu mtoa mada,

Jee wewe ulini quote kwa sbb ganii?

Sababu niliyoku quote ni hii hapa, narejea andiko lako hilo hilo ambalo hayo maneno uliyaruka,

"Na usikute hata hayo matatizo ni ya kujitakia, binafsi naona wame msaidia sana, wewe na kisirani chako unakuja kutukana watu gari zima, watu wanahitaji utulivu, kumbuka hio ni safari, kuna wanaosafiri kwa shida, biashara, makutano, mapatano n.k n.k. Hivyo wanahitaji utulivu.

Binafsi nampongeza kwa utulivu, mwingine angemkaba koo..... oohoooo, utulivu ni kipaji kingine.

Sidhani kama umesoma vzr."

Tayari ulisambaza mawazo hasi kwa kumdhania huyo Mama ana matatizo ya kujitakia baada ya yule memba kusema huenda ana matatizo, bado ukaongeza kua ana kisirani anakuja kutukana gari zima watu wanahitaji utulivu na kama haitoshi ukasema mwingine angemkaba koo,

Quote yangu ilikuja kujibu hayo maneno hapo kua huyo Mama kwa maelezo ya Mtoa mada ni wazi ana tatizo la Afya ya Akili, haikua vema kuendelea kumuattack badala yake wangeweza kumu ignore na kila mtu angesafiri kwa Amani.

Je, kosa langu liko wapi?
 
Basi sikujua kama kuna mashindano,
Haya na wewe ulikua unasumbuliwa na nini?
Huyo mwenzio ameshamaliza hoja zake amebaki kurudia kurudia
Ngoja kuna kitu nikitafute.....nipate jibu.

[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Wewe huna Dr. Wala nini mganga tuu nishakukumbuka ulinitapelii
 
Kuna kisa nilicheka sana kwenye hizi dadadala(eacher).
Kuna maza mmoja mtu mzima sana miaka kama 50+ sema ana mwili wa mazoezi ko kidogo yuko skanganga, alikanyagwa bahati mbaya na binti wa kama miaka 26 hivi.

Yule maza alivyokanyagwa kwenye purukushani za kugombea siti alikausha tu. Purukushani zilivyotulia alimfata yule dada(alikua siti ya nyuma yake), akamfinya mkononi(kwenye msuli hapa).
Dada: kheeeh we mama vipi mbona unanifinya

Maza: we ulivonikanyaga ulihisi utamu eeh

Dada: sa ndo unifinye, hujui nimeumia, mbona hujiheshimu we mama

Maza: nijiheshimu kwako wewe kitoto kidogo nakuzaa huku nakimbia..

Raia ikabidi wamtulize binti maana show ya maza ilikua si ya kitoto.
 
Pole sana mkuu
Alijuwa na msongo wa ubongo kama si mawazo
 
Sababu niliyoku quote ni hii hapa, narejea andiko lako hilo hilo ambalo hayo maneno uliyaruka,

"Na usikute hata hayo matatizo ni ya kujitakia, binafsi naona wame msaidia sana, wewe na kisirani chako unakuja kutukana watu gari zima, watu wanahitaji utulivu, kumbuka hio ni safari, kuna wanaosafiri kwa shida, biashara, makutano, mapatano n.k n.k. Hivyo wanahitaji utulivu.

Binafsi nampongeza kwa utulivu, mwingine angemkaba koo..... oohoooo, utulivu ni kipaji kingine.

Sidhani kama umesoma vzr."

Tayari ulisambaza mawazo hasi kwa kumdhania huyo Mama ana matatizo ya kujitakia baada ya yule memba kusema huenda ana matatizo, bado ukaongeza kua ana kisirani anakuja kutukana gari zima watu wanahitaji utulivu na kama haitoshi ukasema mwingine angemkaba koo,

Quote yangu ilikuja kujibu hayo maneno hapo kua huyo Mama kwa maelezo ya Mtoa mada ni wazi ana tatizo la Afya ya Akili, haikua vema kuendelea kumuattack badala yake wangeweza kumu ignore na kila mtu angesafiri kwa Amani.

Je, kosa langu liko wapi?

Sababu niliyoku quote ni hii hapa, narejea andiko lako hilo hilo ambalo hayo maneno uliyaruka,

"Na usikute hata hayo matatizo ni ya kujitakia, binafsi naona wame msaidia sana, wewe na kisirani chako unakuja kutukana watu gari zima, watu wanahitaji utulivu, kumbuka hio ni safari, kuna wanaosafiri kwa shida, biashara, makutano, mapatano n.k n.k. Hivyo wanahitaji utulivu.

Binafsi nampongeza kwa utulivu, mwingine angemkaba koo..... oohoooo, utulivu ni kipaji kingine.

Sidhani kama umesoma vzr."

Tayari ulisambaza mawazo hasi kwa kumdhania huyo Mama ana matatizo ya kujitakia baada ya yule memba kusema huenda ana matatizo, bado ukaongeza kua ana kisirani anakuja kutukana gari zima watu wanahitaji utulivu na kama haitoshi ukasema mwingine angemkaba koo,

Quote yangu ilikuja kujibu hayo maneno hapo kua huyo Mama kwa maelezo ya Mtoa mada ni wazi ana tatizo la Afya ya Akili, haikua vema kuendelea kumuattack badala yake wangeweza kumu ignore na kila mtu angesafiri kwa Amani.

Je, kosa langu liko wapi?
Kumwambia mtu ana tatizo la akili bila uthibitisho huoni ni kumsambazia mawazo hasi pia?
 
Hapo waza ndio mkeo nyumbani...
kuna siku nilikuwa nasafiri nikaona nikalale kwa bro kuepusha gharama ili kesho niendelee, jirani ya bro (ni nyumba kubwa) ni mwanamke mmoja ana mdomo kama huyo

yani wapangaji ile nyumba ni kama sita hivi ila yeye ali rap mno pale nje kwenye kikao cha umeme, nahisi hajaolewa
 
Ahaaa hapo umejibu sasa, All Squared.

Sasa Dr. Hiki si ilikua kitu cha kueleza tuu mwenyewe bila kuulizwa,
Nadhani kuna kitu umemiss kwenye maelezo ya mtoa mada, kwa mujibu wa mtoa mada yule Mama hakua anahitaji pesa ndio maana aliweza kusafiri na kulipia nauli yake na watoto wake, alikerwa na maswali ya konda licha ya kumwambia kua hayupo sawa, mtoa mada akasema walianza mzozo hapo sasa ndio konda ali trigger kile kitu ambacho tangu mwanzo yule mama alisema hayupo sawa,

Dereva kamuwakia anataka amshushe na gari zima likakubali kweli ashushwe hapo ni wazi aliwaza nikishuka hapa je nitarejeshewa nauli yangu? Itakuaje hatma yangu na watoto? Lakini alipojitokeza huyo mzee na kusema atamlipia kila kitu na cha juu akasema "hebu nishuke nimechoshwa na kelele za humu ndani" ni wazi hakua na sababu ya kuendelea kua kwenye bus ambalo watu wote wamemkasirikia hadi dereva ila kwa kua alishapata refund yake ikawa rahisi kwake kushuka,

Je hapo ana kosa gani? Ulitamani akatae refund na kuendelea kulumbana na hao watu kwenye bus?
 
Ngoja kuna kitu nikitafute.....nipate jibu.

[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Wewe huna Dr. Wala nini mganga tuu nishakukumbuka ulinitapelii
Pole kwa kutapeliwa ila principle ya utapeli inasema "ni Tamaa zako ndio zinakuponza"

Wamatumbi wanamsemo wao "Don't hate the Player, hate the Game"
 
Tupo tunasafiri, kuna mdada mmoja mzuri, body si haba na kavaa smart kabisaaa, Wakati yupo chini konda akamuomba jina ili amuandikie tiketi.

Ninukuu baadhi ya majibizano, sio yote kisa ni kirefuu.

Akajibu "Niache nitulie andika hao wengine"

Akaachwa, tupo ndani konda akamfuata akamuambia naomba nitajie jina mbele kuna traffic na wewe umekaa mbele anaweza ashtukie tiketi iwe faini.

Akajibu "Wee naweee, haya andika..."

Alitaja jina moja tena la kiume, konda akumuomba jina la pili.

Akajibu "Andika hilo, kama hutaki acha"

Konda akaandika, akamuoma jina la mwanae angalau mmoja maana wamekaa kwenye siti ili nalo liandikwe kwenye ticket yao,

Akajibu "Wanangu majina yao sio ya kukaa kwenye magazeti..... braa braa na maneno mengi nishasahau"

Akaulizwa "mbona wewe msumbufu sanaa wenzako wameonesha ushirikiano hili ni jambo la kawaidaa

Akajibu "wao ni wao mimi nina taratibu zangu, wengi waoga"

Hapo ndio watu wakacharukwa, majibishano yakawa makubwaa, mimi nilikua nimekaa naye, mwenyewe nina mambo yangu nimevurugwa kuepuka mavurugo, nikamwambia

Ngoja mimi niende pale wanao waje hapa ukae nao,
(wakati anakata ticke mi nilishawahi ile siti hakupata duble).

Akaanigeuzia mimi ( "Yaani umenionaje? Kwa nn mda wote usiseme? Mi nakupigia kelele hapa? Nanuka?)

Sikumjibu nikaweka earphones nikaegamia zangu dirishani (nikaomba tuu hapa asije akatuma tusi tu) akageukia wengine, kila anayemuongelesha anapita naye kwa kila lugha chafu.

Watu wakasema kama vipi ashushwe asituletee nuksi humu, akasemaa,"nani anishushe...? Kwa kosa ganii...? hakuna anayenijua humu ulizieniii"

Gari ikasimama kweli, mimi nikawa nawaza huyu kashanitibua nimtetee?

Nikasema haina haja mtu mwenyewe kwa mawasiliano tuu aliyokua akifanya ni kama ana matatizo nyumbani.

Nikashauri "huyu tukimshusha katikati huku jua hili na watoto wadogo ni hatari hasa kwa hivi vitoto", wapo 3 kimoja kichanga.

Akanigeukia, "wewe ndio una akili akilituu sijui ulikua wapi wengine maboksi"

Daa nilichoka, dereva akafunga blek akaamka aje kumzibua, watu wakamzuia, tusije pata mikosi.

Akaanza "hamna wa kunigusa hapa wala mwenye hela ya kunishusa, hii gari nimepanda tu, ila ningekua na uwezo wa kuja na gari yangu ila sababu ya huyu mtoto mdogo, Hata kukodi sishindwii".

Mzee mmoja akawa kama kamaindi hivi, akamuuliza

"Una hela wewe, hivi unajua pesaaa? Yaani, yaanniii....."

ikawa kama mtu flani ile kauli imemuuma anataka aprove kama hana pesa wenye pesa wapo kimya ila anshindwa kumalizia.

Akamuambia konda, tukifika kituoni tunamshusha nitamlipa hela zake asitupigie kelele, halafu ampigie yeyote anayedai anamfahamu.

Akasema, "hamna wa kunishusha" ,akaambiwa
"wewe nakulipia nauli yako, wanao wote siti, hela ya kula, kulala, dharura na inabaki".

Tumefika mzee alitoa bunda akamuuliza unashuka hushuki, akasema sishukiii, Kugeuka nyuma kuona bunda iliyoshikwa, akageuka akawambia "wanangu amkeni nimechoka hizi kelele" akapewa akamtuma mwanae aje kuzipokea, alivyomfikia tuu akazikwapua akaweka kwenye pochi.

Wote tulichokaa, kwanza tulijua atakataa, alishuka fasta hakuongea kitu tena tukamuona anaongea na konda wa gari nyingine inayoenda tulikotoka kama vile anataka kurudi, kwa ufupi ilikua ni maneno mengi ya kukera mengi nimesahau na hivyo niliamua kusikiliza mziki, kuna jama wa watu alimuwakia kwa kumuangalia tuu.... ila mwisho ikawa hivyo.

Sisi tukasepaa.
Ha ha ha [emoji23]. Dduh
 
Kumwambia mtu ana tatizo la akili bila uthibitisho huoni ni kumsambazia mawazo hasi pia?
Bro, mbona tunarudi kule kule tena?
Kama hoja zimeisha wewe sema lakini pia unaweza kurejea majibizano yetu kuanzia mwanzo huenda ukapata kipya ili uendeleze mjadala.
 
Back
Top Bottom