Wanawake wana visirani sana ila huyu wa leo kazidi

Wanawake wana visirani sana ila huyu wa leo kazidi

Itakua na wewe una tatizo la afya ya akili,
Aliyekwambia mtoa mada ana kosa nani?
Au wameeleweshwa waliomzonga huyo Mama kua pengine huyo Mama hakua sawa kiakili
🤣🤣🤣 Dr. Kacharukwaa..
Relaaaax, wewe twende vzr sasa, tena naanzia kwenye hii comment yako...

"NDIO" Nina tatizo la akili na umeligundua, vizuri,
Sasa ngoja niamini wewe ni dr. Kweli, Mimi ni mgonjwa wa akili na umegundua,
Nipe uhalali wako wa kunitangazia hapa..?
 
Dr. Swali linajibiwa kwa swali kweliii?
Nijibu basi swali langu kwanzaa...

Halafu baadae nikuulize umesoma uzi vizuri...?
Eeh Mwanafalsafa mmoja anasema swali kwa swali hupatikana jibu,
Umehoji kua alipona baada ya kupata pesa! na wewe ukaulizwa ulijuaje kama alipona sababu hamkua safari moja?

Kama wewe una tatizo la Afya ya Akili na ukanitukana nikikurudishia mimi nitaonekana ni kichaa kabisa niliyokosa maana,

Uzi nimeusoma na kuuelewa vema na ndio maana nikahitimisha kua huyo Mama ana tatizo la Afya ya Akili hakuna timamu angeweza kufanya hayo aliyoyafanya na nikaongezea tena kua huna uelewa wa Afya ya Akili ndio maana umechukulia kiuwepesi,

Wengi wenu mnadhani mtu mwenye tatizo la afya ya akili basi hua kichaa anayevua nguo, lakini nikwambie haipo hivyo.
 
Dr. Swali linajibiwa kwa swali kweliii?
Nijibu basi swali langu kwanzaa...

Halafu baadae nikuulize umesoma uzi vizuri...?
Niachie huyu nitembee naye, napendaga watu wana attack sana watu badala ya hoja, bahati nzuri sinaga hasira na lugha chafu,

Haya Dr. Mariposa Twende pamoja just relax ni hoja ukiwa na fact naitika.
 
Akanigeukia, "wewe ndio una akili akilituu sijui ulikua wapi wengine maboksi"

Daa nilichoka, dereva akafunga blek akaamka aje kumzibua, watu wakamzuia, tusije pata mikosi.
Alitaka uwe mshirika wa kurusha makombora Ukraine
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Dr. Kacharukwaa..
Relaaaax, wewe twende vzr sasa, tena naanzia kwenye hii comment yako...

"NDIO" Nina tatizo la akili na umeligundua, vizuri,
Sasa ngoja niamini wewe ni dr. Kweli, Mimi ni mgonjwa wa akili na umegundua,
Nipe uhalali wako wa kunitangazia hapa..?

Kwa kukujibu ni kua sijagundua kama una tatizo la afya ya akili sababu sijaingia kwenye session na wewe ila nimepatwa na mashaka/wasiwasi kua "itakua una tatizo la Afya ya Akili" kulingana na ulichojibu ndio mashaka hayo yalipojitokeza,

Kitendo cha kujibu "NDIO nina tatizo la akili" ni wewe ndie umejitangaza na sio mimi.
 
Eeh Mwanafalsafa mmoja anasema swali kwa swali hupatikana jibu,
Umehoji kua alipona baada ya kupata pesa! na wewe ukaulizwa ulijuaje kama alipona sababu hamkua safari moja?

Kama wewe una tatizo la Afya ya Akili na ukanitukana nikikurudishia mimi nitaonekana ni kichaa kabisa niliyokosa maana,

Uzi nimeusoma na kuuelewa vema na ndio maana nikahitimisha kua huyo Mama ana tatizo la Afya ya Akili hakuna timamu angeweza kufanya hayo aliyoyafanya na nikaongezea tena kua huna uelewa wa Afya ya Akili ndio maana umechukulia kiuwepesi,

Wengi wenu mnadhani mtu mwenye tatizo la afya ya akili basi hua kichaa anayevua nguo, lakini nikwambie haipo hivyo.
Oky, wewe umejuaje ya kua ana tatizo la kiafya...
NB : jibu la hili swali ni muhimu sanaa.
 
Wote tulichokaa, kwanza tulijua atakataa, alishuka fasta hakuongea kitu tukamuona anaongea na konda wa gari nyingine inayoenda tulikotoka kama vile anataka kurudi, kwa ufupi ilikua ni maneno mengi ya kukera mengi nimesahau na hivyo niliamua kusikiliza mziki, kuna jama wa watu alimuwakia kwa kumuangalia tuu.... ila mwisho ikawa hivyo.
Ni Kanda maalumu au North
 
Tumefika mzee alitoa bunda akamuuliza unashuka hushuki, akasema sishukiii, Kugeuka nyuma kuona bunda iliyoshikwa, akageuka akawambia "wanangu amkeni nimechoka hizi kelele"[emoji23]
Fanya mchezo nini na bunda siyo poa kwamba nimechoka kelele. [emoji23][emoji23]
 
Niachie huyu nitembee naye, napendaga watu wana attack sana watu badala ya hoja, bahati nzuri sinaga hasira na lugha chafu,

Haya Dr. Mariposa Twende pamoja just relax ni hoja ukiwa na fact naitika.
Hahahahahaha sasa nani ameku attack? Kujibiwa hoja yako imekua nongwa!?
Basi nisamehe mimi huyo Mama hana tatizo la Akili ni jeuri, kiburi, mwenye dharau iliyopitiliza na angekutana na wewe ungemkomesha ipasavyo,

Happy??
 
Tumefika mzee alitoa bunda akamuuliza unashuka hushuki, akasema sishukiii, Kugeuka nyuma kuona bunda iliyoshikwa, akageuka akawambia "wanangu amkeni nimechoka hizi kelele"[emoji23]
🤣 hakuna mkate mgumu mbele ya chai
 
Oky, wewe umejuaje ya kua ana tatizo la kiafya...
NB : jibu la hili swali ni muhimu sanaa.
"Uzi nimeusoma na kuuelewa vema na ndio maana nikahitimisha kua huyo Mama ana tatizo la Afya ya Akili hakuna timamu angeweza kufanya hayo aliyoyafanya na nikaongezea tena kua huna uelewa wa Afya ya Akili ndio maana umechukulia kiuwepesi,"

Swali lako lilijibiwa hapo
 
Kwa kukujibu ni kua sijagundua kama una tatizo la afya ya akili sababu sijaingia kwenye session na wewe ila nimepatwa na mashaka/wasiwasi kua "itakua una tatizo la Afya ya Akili" kulingana na ulichojibu ndio mashaka hayo yalipojitokeza,

Kitendo cha kujibu "NDIO nina tatizo la akili" ni wewe ndie umejitangaza na sio mimi.
Sawa Dr.
Mgonjwa kaja kwako ana dalili UNAZOAMINI ni mgonjwa wa HIV, bila vipimo
Professional yako inakuruhusu kwa mashaka yako kumtangazia ya kua ana HIV?
 
"Uzi nimeusoma na kuuelewa vema na ndio maana nikahitimisha kua huyo Mama ana tatizo la Afya ya Akili hakuna timamu angeweza kufanya hayo aliyoyafanya na nikaongezea tena kua huna uelewa wa Afya ya Akili ndio maana umechukulia kiuwepesi,"

Swali lako lilijibiwa hapo
😯😯😯 yaani comment hio hio unayojibu unauliza swali liko wapi tena dr wetuu??

Anyway ngoja basi nikuwekee ???
Wewe umajuaje ya kua ana tatizo la kiafya..?
 
Tupo tunasafiri, kuna mdada mmoja mzuri, body si haba na kavaa smart kabisaaa, Wakati yupo chini konda akamuomba jina ili amuandikie tiketi.

Ninukuu baadhi ya majibizano, sio yote kisa ni kirefuu.

Akajibu "Niache nitulie andika hao wengine"

Akaachwa, tupo ndani konda akamfuata akamuambia naomba nitajie jina mbele kuna traffic na wewe umekaa mbele anaweza ashtukie tiketi iwe faini.

Akajibu "Wee naweee, haya andika..."

Alitaja jina moja tena la kiume, konda akumuomba jina la pili.

Akajibu "Andika hilo, kama hutaki acha"

Konda akaandika, akamuoma jina la mwanae angalau mmoja maana wamekaa kwenye siti ili nalo liandikwe kwenye ticket yao,

Akajibu "Wanangu majina yao sio ya kukaa kwenye magazeti..... braa braa na maneno mengi nishasahau"

Akaulizwa "mbona wewe msumbufu sanaa wenzako wameonesha ushirikiano hili ni jambo la kawaidaa

Akajibu "wao ni wao mimi nina taratibu zangu, wengi waoga"

Hapo ndio watu wakacharukwa, majibishano yakawa makubwaa, mimi nilikua nimekaa naye, mwenyewe nina mambo yangu nimevurugwa kuepuka mavurugo, nikamwambia

Ngoja mimi niende pale wanao waje hapa ukae nao,
(wakati anakata ticke mi nilishawahi ile siti hakupata duble).

Akaanigeuzia mimi ( "Yaani umenionaje? Kwa nn mda wote usiseme? Mi nakupigia kelele hapa? Nanuka?)

Sikumjibu nikaweka earphones nikaegamia zangu dirishani (nikaomba tuu hapa asije akatuma tusi tu) akageukia wengine, kila anayemuongelesha anapita naye kwa kila lugha chafu.

Watu wakasema kama vipi ashushwe asituletee nuksi humu, akasemaa,"nani anishushe...? Kwa kosa ganii...? hakuna anayenijua humu ulizieniii"

Gari ikasimama kweli, mimi nikawa nawaza huyu kashanitibua nimtetee?

Nikasema haina haja mtu mwenyewe kwa mawasiliano tuu aliyokua akifanya ni kama ana matatizo nyumbani.

Nikashauri "huyu tukimshusha katikati huku jua hili na watoto wadogo ni hatari hasa kwa hivi vitoto", wapo 3 kimoja kichanga.

Akanigeukia, "wewe ndio una akili akilituu sijui ulikua wapi wengine maboksi"

Daa nilichoka, dereva akafunga blek akaamka aje kumzibua, watu wakamzuia, tusije pata mikosi.

Akaanza "hamna wa kunigusa hapa wala mwenye hela ya kunishusa, hii gari nimepanda tu, ila ningekua na uwezo wa kuja na gari yangu ila sababu ya huyu mtoto mdogo, Hata kukodi sishindwii".

Mzee mmoja akawa kama kamaindi hivi, akamuuliza

"Una hela wewe, hivi unajua pesaaa? Yaani, yaanniii....."

ikawa kama mtu flani ile kauli imemuuma anataka aprove kama hana pesa wenye pesa wapo kimya ila anshindwa kumalizia.

Akamuambia konda, tukifika kituoni tunamshusha nitamlipa hela zake asitupigie kelele, halafu ampigie yeyote anayedai anamfahamu.

Akasema, "hamna wa kunishusha" ,akaambiwa
"wewe nakulipia nauli yako, wanao wote siti, hela ya kula, kulala, dharura na inabaki".

Tumefika mzee alitoa bunda akamuuliza unashuka hushuki, akasema sishukiii, Kugeuka nyuma kuona bunda iliyoshikwa, akageuka akawambia "wanangu amkeni nimechoka hizi kelele" akapewa akamtuma mwanae aje kuzipokea, alivyomfikia tuu akazikwapua akaweka kwenye pochi.

Wote tulichokaa, kwanza tulijua atakataa, alishuka fasta hakuongea kitu tukamuona anaongea na konda wa gari nyingine inayoenda tulikotoka kama vile anataka kurudi, kwa ufupi ilikua ni maneno mengi ya kukera mengi nimesahau na hivyo niliamua kusikiliza mziki, kuna jama wa watu alimuwakia kwa kumuangalia tuu.... ila mwisho ikawa hivyo.

Sisi tukasepaa.
Watasingiziwa

1681389296186.png
 
Sawa Dr.
Mgonjwa kaja kwako ana dalili UNAZOAMINI ni mgonjwa wa HIV, bila vipimo
Professional yako inakuruhusu kwa mashaka yako kumtangazia ya kua ana HIV?
Afya ya Akili ni tofauti na Afya ya Mwili,
Afya ya Mwili ni lazima vipimo vya maabara vihusike na Afya ya Akili ina sessions zake japo kuna indicators zinaweza kutokea na ukahisi huyu ana tatizo la afya ya akili utaingia nae kwenye therapy ili kujipa uhakika.
 
Hahahahahaha sasa nani ameku attack? Kujibiwa hoja yako imekua nongwa!?
Basi nisamehe mimi huyo Mama hana tatizo la Akili ni jeuri, kiburi, mwenye dharau iliyopitiliza na angekutana na wewe ungemkomesha ipasavyo,

Happy??
Ahaaa, twende vzr, nakunukuu mwenyeweee

"wewe una tatizo la afya ya akili"

"Kwa kukujibu ni kua sijagundua kama una tatizo la afya ya akili sababu sijaingia kwenye session na wewe"

Haya tumeweka kumbukumbu vizuri, Rudia kama huja ni attack....
 
Unaweza kuta ni aina mpya ya utapeli mjini. Analeta ubishi wee akifahamu kuna abiria watakereka na kumrudishia nauli yake na posho juu
 
Back
Top Bottom