Wanawake wana visirani sana ila huyu wa leo kazidi

Wanawake wana visirani sana ila huyu wa leo kazidi

Nadhani kuna kitu umemiss kwenye maelezo ya mtoa mada, kwa mujibu wa mtoa mada yule Mama hakua anahitaji pesa ndio maana aliweza kusafiri na kulipia nauli yake na watoto wake, alikerwa na maswali ya konda licha ya kumwambia kua hayupo sawa, mtoa mada akasema walianza mzozo hapo sasa ndio konda ali trigger kile kitu ambacho tangu mwanzo yule mama alisema hayupo sawa,

Dereva kamuwakia anataka amshushe na gari zima likakubali kweli ashushwe hapo ni wazi aliwaza nikishuka hapa je nitarejeshewa nauli yangu? Itakuaje hatma yangu na watoto? Lakini alipojitokeza huyo mzee na kusema atamlipia kila kitu na cha juu akasema "hebu nishuke nimechoshwa na kelele za humu ndani" ni wazi hakua na sababu ya kuendelea kua kwenye bus ambalo watu wote wamemkasirikia hadi dereva ila kwa kua alishapata refund yake ikawa rahisi kwake kushuka,

Je hapo ana kosa gani? Ulitamani akatae refund na kuendelea kulumbana na hao watu kwenye bus?
Unaikumbuka hii Dr.
"hamna wa kunigusa hapa wala mwenye hela ya kunishusa,"

Haya mawazo alibadilishaje?
 
Pole kwa kutapeliwa ila principle ya utapeli inasema "ni Tamaa zako ndio zinakuponza"

Wamatumbi wanamsemo wao "Don't hate the Player, hate the Game"
[emoji12][emoji12][emoji12][emoji12]Dr. Mimi nina tatizo la akili, nimekuja kwako
Otea...?
 
Unaikumbuka hii Dr.
"hamna wa kunigusa hapa wala mwenye hela ya kunishusa,"

Haya mawazo alibadilishaje?
Hahahaha unataka tuanze kulichambua neno moja moja la mtu aliyekosa utimamu wa akili?
Mbona kama na sisi jamii itatushangaa?

Labda wewe useme exactly kwa mada husika, msimamo wako ni upi?
 
[emoji12][emoji12][emoji12][emoji12]Dr. Mimi nina tatizo la akili, nimekuja kwako
Otea...?
Unataka niotee utakachosema next, unataka niotee tatizo lako la akili au unataka niotee wewe kuja kwangu?

Funguka vizuri
 
Hahahaha unataka tuanze kulichambua neno moja moja la mtu aliyekosa utimamu wa akili?
Mbona kama na sisi jamii itatushangaa?

Labda wewe useme exactly kwa mada husika, msimamo wako ni upi?
Ni kwamb hakuna uhakika Ya kua yule dada ana Matatizo ya akili.
 
Tumefika mzee alitoa bunda akamuuliza unashuka hushuki, akasema sishukiii, Kugeuka nyuma kuona bunda iliyoshikwa, akageuka akawambia "wanangu amkeni nimechoka hizi kelele"[emoji23]
Hiyo ndio pesa sasa haina maneno mengi mmmk....
 
Alitakiwa atoke kigagula mmoja ampige kizizi aharishe basi zima ndio ajue wa kumgusa wapo
 
Tupo tunasafiri, kuna mdada mmoja mzuri, body si haba na kavaa smart kabisaaa, Wakati yupo chini konda akamuomba jina ili amuandikie tiketi.

Ninukuu baadhi ya majibizano, sio yote kisa ni kirefuu.

Akajibu "Niache nitulie andika hao wengine"

Akaachwa, tupo ndani konda akamfuata akamuambia naomba nitajie jina mbele kuna traffic na wewe umekaa mbele anaweza ashtukie tiketi iwe faini.

Akajibu "Wee naweee, haya andika..."

Alitaja jina moja tena la kiume, konda akumuomba jina la pili.

Akajibu "Andika hilo, kama hutaki acha"

Konda akaandika, akamuoma jina la mwanae angalau mmoja maana wamekaa kwenye siti ili nalo liandikwe kwenye ticket yao,

Akajibu "Wanangu majina yao sio ya kukaa kwenye magazeti..... braa braa na maneno mengi nishasahau"

Akaulizwa "mbona wewe msumbufu sanaa wenzako wameonesha ushirikiano hili ni jambo la kawaidaa

Akajibu "wao ni wao mimi nina taratibu zangu, wengi waoga"

Hapo ndio watu wakacharukwa, majibishano yakawa makubwaa, mimi nilikua nimekaa naye, mwenyewe nina mambo yangu nimevurugwa kuepuka mavurugo, nikamwambia

Ngoja mimi niende pale wanao waje hapa ukae nao,
(wakati anakata ticke mi nilishawahi ile siti hakupata duble).

Akaanigeuzia mimi ( "Yaani umenionaje? Kwa nn mda wote usiseme? Mi nakupigia kelele hapa? Nanuka?)

Sikumjibu nikaweka earphones nikaegamia zangu dirishani (nikaomba tuu hapa asije akatuma tusi tu) akageukia wengine, kila anayemuongelesha anapita naye kwa kila lugha chafu.

Watu wakasema kama vipi ashushwe asituletee nuksi humu, akasemaa,"nani anishushe...? Kwa kosa ganii...? hakuna anayenijua humu ulizieniii"

Gari ikasimama kweli, mimi nikawa nawaza huyu kashanitibua nimtetee?

Nikasema haina haja mtu mwenyewe kwa mawasiliano tuu aliyokua akifanya ni kama ana matatizo nyumbani.

Nikashauri "huyu tukimshusha katikati huku jua hili na watoto wadogo ni hatari hasa kwa hivi vitoto", wapo 3 kimoja kichanga.

Akanigeukia, "wewe ndio una akili akilituu sijui ulikua wapi wengine maboksi"

Daa nilichoka, dereva akafunga blek akaamka aje kumzibua, watu wakamzuia, tusije pata mikosi.

Akaanza "hamna wa kunigusa hapa wala mwenye hela ya kunishusa, hii gari nimepanda tu, ila ningekua na uwezo wa kuja na gari yangu ila sababu ya huyu mtoto mdogo, Hata kukodi sishindwii".

Mzee mmoja akawa kama kamaindi hivi, akamuuliza

"Una hela wewe, hivi unajua pesaaa? Yaani, yaanniii....."

ikawa kama mtu flani ile kauli imemuuma anataka aprove kama hana pesa wenye pesa wapo kimya ila anshindwa kumalizia.

Akamuambia konda, tukifika kituoni tunamshusha nitamlipa hela zake asitupigie kelele, halafu ampigie yeyote anayedai anamfahamu.

Akasema, "hamna wa kunishusha" ,akaambiwa
"wewe nakulipia nauli yako, wanao wote siti, hela ya kula, kulala, dharura na inabaki".

Tumefika mzee alitoa bunda akamuuliza unashuka hushuki, akasema sishukiii, Kugeuka nyuma kuona bunda iliyoshikwa, akageuka akawambia "wanangu amkeni nimechoka hizi kelele" akapewa akamtuma mwanae aje kuzipokea, alivyomfikia tuu akazikwapua akaweka kwenye pochi.

Wote tulichokaa, kwanza tulijua atakataa, alishuka fasta hakuongea kitu tena tukamuona anaongea na konda wa gari nyingine inayoenda tulikotoka kama vile anataka kurudi, kwa ufupi ilikua ni maneno mengi ya kukera mengi nimesahau na hivyo niliamua kusikiliza mziki, kuna jama wa watu alimuwakia kwa kumuangalia tuu.... ila mwisho ikawa hivyo.

Sisi tukasepaa.
.
JamiiForums790734876.jpg
 
Ni kwamb hakuna uhakika Ya kua yule dada ana Matatizo ya akili.
Rejea kule juu kwenye maana niliyokupa kuhusu Afya ya Akili, ukiielewa ile maana basi moja kwa moja utajua kua huyo dada kwa tukio lile ni wazi ana tatizo la Afya ya akili,

Ni kama kwenye Afya ya Mwili mgonjwa atasema ana pata homa, maumivu ya kichwa, maumivu ya mgongo, kukosa usingizi, kwa maelezo yale daktari atamwambia akapime Malaria na UTI ili ajue anaanzia wapi,

Tukirudi kwa huyo mama, hali iliyojitokeza tayari iliashiria ana tatizo la Afya ya Akili/ kakosa utulivu wa Akili, sasa kama ndio anapelekwa kwa mtaalam, litaanza somo rasmi ili kubaini tatizo lake la Afya ya Akili ni lipi,

NB: Afya ya Akili sio Mtu kua chizi au mwendawazimu, ukishakua na msongo mzito wa mawazo kiasi kwamba ukashindwa kufanya maamuzi yaliyo chanya, tayari wewe Afya yako ya Akili imeshatetereka.
 
Kwahio wale waliokua wanajibishana naye, dereva anyetaka kumpiga nao tunaweza kusema wana tatizo la akili?
 
Sawaa, na kama sikoseni, pia unamanisha hio inaweza ikawa ni hali ya kuja na kupita, kwahio yeyote ukamkuta katika moment kama hio tunaweza jumuisha ana matatizo ya akili.
 
Huyo mwanamke nyama nyama zipo kweli kwa namna ulivyomuona mtoa mada???? [emoji4]
 
Kwahio wale waliokua wanajibishana naye, dereva anyetaka kumpiga nao tunaweza kusema wana tatizo la akili?
Majibizano hua hayana shida ila kitendo cha dereva kutaka kumpiga mwanamke mwenye mtoto mchanga ni wazi kua dereva na yeye ana tatizo la afya ya akili,

Rejea tena maana ya Afya ya Akili,

Si umeona wewe ulikaa kimya? sababu akili yako ilikua na utulivu.
 
Ila mwamba na wewe una kipaji cha umvea,yote haya umekuwa na uwezo wa kuyakariri na kuyaleta hapa jukwaani.
 
Back
Top Bottom