Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,809
- 15,421
Kuna wakati mwanaume anakuwa na kazi nyingi sana, au anatumia muda wake mwingi kwenye kujisomea, hata pale mwanamke anapoonyesha kwamba anahitaji kuwa naye kwa muda fulani.
Kuna wakati pia mwanaume anaweza kuonesha kwamba anajali zaidi kazi zake kuliko mambo mengine ambayo mkewe anayataka na kuyaona ya maana.
Kwa mfano, kama mwanamke anataka kufanya jambo fulani ambalo inabidi mwanaume amsaidie inapotokea mwanaume kuonyesha kwamba hajali sana juu ya jambo hilo, bila kujali kama inawezekana au haiwezekani, mwanamke huanza kuhisi kutoneshwa. Pale mwanaume anapokaa na mkewe na kujadili juu ya jambo hilo na kuonesha uzingativu, hata kama hatalifanya mwanamke hujihisi vizuri zaidi.
Kuna wakati mwanaume anaweza kumwambia mwanamke moja kwa moja, "yaani niache kazi zangu nikae kukusikiliza wewe….wewe subiri nikipata nafasi tutaongea mambo hayo".
Kauli kama hizi huwa ni sumu kali sana katika uhusiano. Wanaume wengi husema au kutojali kuhusu utashi wa kihisia wa wanawake kwa kuamini kwamba wanawake wanachojali ni kupewa fedha au mali basi. Kwa hiyo, wanahalalisha kazi kuwa kitu muhimu kuliko mahitaji ya kihisia na hata kimwili ya wake au wapenzi wao.
Ukweli ni kwamba wanawake kimaumbile huhitaji sana kuona mume au mpenzi anawaona kuwa wao ni maalum na hawawezi kulinganishwa na kitu kingine. Kumuonyesha mwanamke kwamba yeye hana thamani kubwa kuliko kazi au shughuli nyingine ya mwanaume ni kosa kubwa ajabu.