Wanawake wanajua kudeka we acha tu!

Wanawake wanajua kudeka we acha tu!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,421
Kuna wakati mwanaume anakuwa na kazi nyingi sana, au anatumia muda wake mwingi kwenye kujisomea, hata pale mwanamke anapoonyesha kwamba anahitaji kuwa naye kwa muda fulani.

Kuna wakati pia mwanaume anaweza kuonesha kwamba anajali zaidi kazi zake kuliko mambo mengine ambayo mkewe anayataka na kuyaona ya maana.

Kwa mfano, kama mwanamke anataka kufanya jambo fulani ambalo inabidi mwanaume amsaidie inapotokea mwanaume kuonyesha kwamba hajali sana juu ya jambo hilo, bila kujali kama inawezekana au haiwezekani, mwanamke huanza kuhisi kutoneshwa. Pale mwanaume anapokaa na mkewe na kujadili juu ya jambo hilo na kuonesha uzingativu, hata kama hatalifanya mwanamke hujihisi vizuri zaidi.

Kuna wakati mwanaume anaweza kumwambia mwanamke moja kwa moja, "yaani niache kazi zangu nikae kukusikiliza wewe….wewe subiri nikipata nafasi tutaongea mambo hayo".

Kauli kama hizi huwa ni sumu kali sana katika uhusiano.
Wanaume wengi husema au kutojali kuhusu utashi wa kihisia wa wanawake kwa kuamini kwamba wanawake wanachojali ni kupewa fedha au mali basi. Kwa hiyo, wanahalalisha kazi kuwa kitu muhimu kuliko mahitaji ya kihisia na hata kimwili ya wake au wapenzi wao.

Ukweli ni kwamba wanawake kimaumbile huhitaji sana kuona mume au mpenzi anawaona kuwa wao ni maalum na hawawezi kulinganishwa na kitu kingine. Kumuonyesha mwanamke kwamba yeye hana thamani kubwa kuliko kazi au shughuli nyingine ya mwanaume ni kosa kubwa ajabu.
 
nakubaliana na wewe hiyo ni ile kutaka attention hata kwa kitu ambacho sio cha muhimu sana ila anataka ujue kuwa amekifanya au anakifanya
 
Uko sahihi mkuu, hizi kazi zinatupotezea sana
we have to always balance our time also to be careful with maneno yetu
 
kila kitu/jambo lina nafasi yake na muda wake....
 
Halafu kudeka nako ni sanaa kuna wanaojulia kudeka mpaka basi
na kuna wengine wanadeka but hawapatii namna ya kudeka...wanakuwa kero hivi....
 
Halafu kudeka nako ni sanaa kuna wanaojulia kudeka mpaka basi
na kuna wengine wanadeka but hawapatii namna ya kudeka...wanakuwa kero hivi....

hivi hebu saidia kudeka na usumbufu kunatofautianaje?
na kutaka 'attention' ni kudeka?
 
kudeka inaenda na kushawishi hivi....sauti laini..tabasamu kubwa hivi..

Kero ni kupandisha sauti au kujiliza bila sababu...

na kutaka attention ya laaziz je? ni kudeka?
 
lol....avatar na comment vimelandanaje!!!

bht afadhali umenipa la kuongea.... Mtambuzi kawasoma wanawake huyu... mwanamke wake ana raha... sijui taabu.... hata sielewi....
 
  • Thanks
Reactions: bht

Mtambuzi... i love being a woman... na hio inahusisha nijisikie mwanamke kwa my Man... Hivo kudeka ni in conjunction... Sijitetei ila ukweli ni kwamba naangalia na situation, sitaki lazimisha - for ukilazimisha kudeka hali yeye yupo busy, wala hata hakudekezi roho ikafurahi... Ni sawa na kusema awe anaangalia mpira alafu umuite akusaidie kupigilia msumari ukutani... Hata akija; at that particular moment... he almost hates you...
 
Hakuna raha duniani kama kupata mwanaume anayejua ku pay attention kwa mkewe (sipendi kutumia neno kudekeza kwani ni broader na lina connotation mbaya). Tena wanaume wa hivyo hawajali mko kwenye kadamnasi au mko faragha wanaona fahari ku act as real men kwa wenza wao. Acha tu.

Mkiwa baa anavuta kiti for you.

Anafungua mlango upite kwanza.

Anakusevia chakula.

Anakuuliza kama umechoka.

Ila wengi wa hivyo nasikitika kuwa ni wazinzi maana wanawake wengi wanawapenda.
 
bht afadhali umenipa la kuongea.... Mtambuzi kawasoma wanawake huyu... mwanamke wake ana raha... sijui taabu.... hata sielewi....

AshaDiii una Visa weyeeeee!!!!
 
Mtambuzi... i love being a woman... na hio inahusisha nijisikie mwanamke kwa my Man... Hivo kudeka ni in conjunction... Sijitetei ila ukweli ni kwamba naangalia na situation, sitaki lazimisha - for ukilazimisha kudeka hali yeye yupo busy, wala hata hakudekezi roho ikafurahi... Ni sawa na kusema awe anaangalia mpira alafu umuite akusaidie kupigilia msumari ukutani... Hata akija; at that particular moment... he almost hates you...

Niliwahi kusema siku moja kuwa, ni shughuli pevu kumuelewa mwanamke, lakini inahitaji moyo wa subira kuweza kumudu jambo hilo..... ni wanaume wachache sana wenye moyo wa subira katika hilo. kwa mfano wako wa kumnyanyua mume wakati anaangalia mpira ili kupigilia msumari ukutani... ni wanaume wachache sana watakaokubali kunyanyuka bila kulalamika...
 
Hakuna raha duniani kama kupata mwanaume anayejua ku pay attention kwa mkewe (sipendi kutumia neno kudekeza kwani ni broader na lina connotation mbaya). Tena wanaume wa hivyo hawajali mko kwenye kadamnasi au mko faragha wanaona fahari ku act as real men kwa wenza wao. Acha tu.

Mkiwa baa anavuta kiti for you.

Anafungua mlango upite kwanza.

Anakusevia chakula.

Anakuuliza kama umechoka.

Ila wengi wa hivyo nasikitika kuwa ni wazinzi maana wanawake wengi wanawapenda.

ooooooh umeanza uzuri mwisho ukanitisha mwenzio...
 
Mwanamke kudeka mwenzangu, na hasa ukiwa na mdekezaji inaleta raha
 
Back
Top Bottom