Wanawake wanajua ni muda gani sahihi wa kumshinda Mwanaume

Wanawake wanajua ni muda gani sahihi wa kumshinda Mwanaume

Ila kwanini wao ni zaidi?
Kwao imeonekana kuwa Mara nyingi huwaacha waume zao katika nyakati zao ngumu. Why?

Sababu kubwa ni visasi.
Wanawake ni viumbe waliojawa na Kisasi.

Mkiwa kwenye neema wengi hunyanyasa, hutoa lugha chafu na hufanya matendo yasiyo ya haki kwa wenza wao.
Inafikia hatua Mwanamke anaomba dua usifanikiwi ili naye afurahi
 
Upo sawa. Kuna kitu wataalam wa mahusiano huwa wanaita ''submission''. Usiombe ukutane na mwanamke mtaalam wa hili jambo. Hii ndiyo makachero wanawake wa kirusi huitumia kupata siri. Ni somo pana sana sana na lina vipengele vingi mno. Mwanamke anaku-control kwa kuwa submissive kwako. Ogopa kabisa. Ndiyo waswahili huwa tunasema jamaa kalishwa limbwata, kumbe ni kucheza na akili tu.

😂😂
Haiwezikani mtu unamfanyia mambo ya ajabu alafu ati awe submissive kwako. Hata kwaakili ya kawaida hilo haliwezekani.

Lakini kuna wanaume wengi wajinga wanaona ni kawaida
 
Mama nani alisema eti tangia hizi kelele za wanawake wanawake ziwe nyingiii, matatizo ndio yameongezeka zaidi. Nikapigaaa 'hiiii' na masingo mama wanaongezeka zaidi kila siku. Hapa dadake ni singo mama, anti yake kaachika miaka karibu 20 na huko....mamake mjane.....yeye mdomo mrefu mnooo.....u knw wat? She is pleasing now for the mistakes she did last year. Hii sio ya kuchekesha. Hii ni live feed natoa hapa. Kumbe watibeli ni kama wacuba tu, akili mingi mnoo.....kama kobe taratibu sheria mkononi hapana. Akili mtu wangu. Kataa ndoaaa kwa ustawi wako na jamii kiujumla
 
Sawa dada kwa taarifa
WANAWAKE WANAJUA NI MUDA GANI SAHIHI WA KUMSHINDA MWANAUME.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Mwanamke yeyote anayejifanya mjuaji kikawaida huwa na akili ndogo. Ni wengi huishia kwenye kushindwa vita nyingi kwa sababu ya upeo mdogo.

Kwa sisi Watibeli, tunajua moja ya mbinu za Watu Smart hasa Zinazotumiwa na Wanawake ni kujifanya wajinga, kujifanya hawajui chochote, kujifanya ni slow Learner.

Wanaume wengi sana yaani kati ya wanaume 10 basi wanaume nane wamejikuta wakishindwa vita na wanawake kwa sababu ya mbinu kabambe za Wanawake ikiwemo hiyo ya kujifanya wao wanaakili ndogo, wao ni dhaifu, wao ni wepesi kudanganywa na kushawishiwa. Jambo ambalo ni uongo.

Wanawake wengi wanajua wakati gani sahihi wa kumshinda mwanaume. Ila wanaume wengi hawajui ni muda gani sahihi wa kumshinda Mwanamke.

Mwanamke ni kiumbe anayetumia hisia zake kuficha hila, njama na akili zake usizitambue. Ni rahisi Mwanamke Kulia au kukuzuga katika mbinu za unyumenyume ili uingie mkenge. Haieleweki chochote.

Ni kweli utamtesa Mwanamke, ni kweli utamdharau Mwanamke na kumfanyia yote utakayoweza kumfanyia.
Lakini wakati unafanya hayo lazima uelewe mambo haya;

1. Mwanamke ni mvumilivu wa mateso ikiwa kuna jambo analitaka kutoka kwako.
Wewe kwa vile umezidiwa upeo na akili. Hujiulizi tuu. Unatesa, unam-cheat, yeye kila siku analia. Lakini kuondoka hataki. Kwa upeo wako mdogo unafikiri huyu kwa vile hana pakwenda, au kwao maskini, au ananipenda sana na yameisha.
Huna Akili boya wewe.

Weka akilini Mwanamke atavumilia kila kitu ikiwa jambo lake analotaka halijafikia.
Elewa zaidi kuwa mwanamke ni lazima alipe kisasi. Usijejichanganya mjinga wewe.

2. Mwanamke atakuvumilia ikiwa upo kwenye Pick na yeye ndiye atakayekudondosha kwa kishindo mpaka jamii ishangae.
Mwanamke hawezi kukuacha ukiwa kwenye nafasi nzuri.
Ukiona mwanamke anaanza kukuletea dharau kwa sisi Watibeli hatukurupuki kufanya maamuzi yoyote.
Dharau kwa mwanamke ni dalili za mwanzoni kuwa muda wa kushughulikia umefika.

Pia mwanamke ukiona unamfanyia mabaya alafu yeye anazidi kukunyenyekea na kukutii hiyo ni medani za ya kivita. Huo ni mtego. Jiongeze.

Hata siku moja usijefikiri kuwa mtu unayelala naye chumba kimoja hana chochote cha kukufanya. Hizo ni akili za mtu mwenye upeo mdogo kabisa wa kufikiri.

Wanawake ni mabingwa wa mipango Ovu. Mabingwa wa hila na njama.
Wanawake sio wazuri wa kupanga maendeleo lakini linapokuja swala la kusuka mipango yakuangamiza wapo very Smart.

3. Wanawake wanajua ni wakati gani sahihi wa kukushambulia.
Hakuna Watu watunza Siri kama Wanawake.
Ingawaje kwa nje wanajionyesha kama hawawezi kutunza siri lakini hiyo ni Janjajanja yao kama kawaida yao.

Taikon kama mwanasaikolojia nimechunguza kwa umakini mkubwa nimegundua yakuwa Wanawake wanajua kutunza siri kuliko wanaume.

Hata huku mitandaoni huwezi kuta wanawake wanaropokaropoka hovyo. Ila kwa wanaume ni wepesi sana kuropoka.

Mpira ni dakika tisini.
Kama ilivyo kwenye Sex, Wanaume wengi huwahi kutangulia kufika mshindo ilhali wanawake huchelewa. Kwenye vita, wanaume wengi hushinda kipindi cha kwanza lakini ikifika kipindi cha pili wengi hushindwa na wanawake huibuka kidedea.
Wengi wa wanaume wamejikuta wakifa kabla ya wakati wao kisa Wanawake.

Wakati walipokuwa wanawatesa na kuwanyanyapaa na kuwanyanyasa Wake zao, Wake zao walivumilia. Lakini Wake wakianza kujibu mashambulizi wengi huishia kupata visukari, presha na stroke na hatimaye kufa kabisa.

4. Wanawake hujua wapi panapouma.
Wanawake hujua wapi wakipiga utajisikia vizuri yaani utaipenda.

Wanawake kumbuka wanatrick yao moja ya kutosema kweli. Mfano wanaweza wakazuga kuwa unawafikisha kileleni kunako 6*6 ili wakupumbaze. Lakini ukweli wanaoujuaga wao.

Elewa wanawake nyakati za mwanzo hutumia muda mwingi kukufahamu na kukujua nguvu na udhaifu wako. Ndio maana nyakati za mwanzo ndio kipindi ambacho Mwanamke huwa na mitego mingi na maswali mengi ya kimitego kukupima na kukujua vyema. Hii huwasaidia kujua maumivu yako yako wapi zaidi.

Wakati huo wao wengi wao hu-pretend na kukupa sifa na tabia za uongo. Wakati Unafikiri unamjua mkeo kumbe humjui.

Hata hivyo wanaume katika hili tunashindwa kwa sababu muda mwingi tunautumia kuwaza maisha na kuilisha familia wakati wenzetu muda huo wanaotumia kujifunza sisi ni Watu wa aina gani.
Unapoambiwa uishi na Mwanamke kwa akili inamaana kubwa sana kuliko wengi wanavyofikiria.

Mwanamke ni kiumbe ambaye hahitaji umfanyie Makosa.😊 Hasa Makosa ya Usaliti. Atajifanya amekusamehe lakini ukweli ni kuwa hajakusamehe. Na ni hakika atakulipa tuu. Ingawaje wapo Exceptional ambao ni wachache mno ambao huweza kusamehe.

Kwa sisi Watibeli, unapofanya kosa kama la Usaliti na mkeo akajua. Nafasi pekee ya kumshinda huyo Mwanamke ni kutengana naye tuu. Hatuamini katika msamaha wa mwanamke hasa uliyemuumiza moyo wake. Hatuamini.

Unapodondoka kinafasi, kicheo na kihadhi mara nyingi Mwanamke hujua ndio nafasi yake ya pekee kukuangusha moja kwa moja. Uzee na kupoteza Mamlaka na sauti mbele ya watoto ndio Mwanamke unaweza kumtambua kuwa alikuwa ni mtu wa namna gani kwako.

Ndio kipindi pekee ambacho mwanamke atakukumbushia mambo ambayo huenda ulimfanyia miaka 40 huko iliyopita. Ndio wakati wa kukumbusha jinsi ulivyokuwa unatumbua pesa na MICHEPUKO.

Ndio wakati sahihi wa yeye kuvunja ndoa, tena ile ndoa ambayo yeye ndio alikuwa anaipigania wakati ule ukiwa unamfukuza na kumwambia aende kwao. Muda umefika sasa.

Ndio wakati ambao atahitaji mgawanyo wa mali, huku akijua kabisa umeshastaafu au umefukuzwa kazi. Na mali unazozitegemea ndio hizohizo na huna uwezo wa kuchuma nyingine.

Ndio wakati sahihi wa kukuambia kuwa yule mtoto unayempenda na kumtegemea kiuchumi sio mtoto wako.
Hayo yote yataanza kwa Drama na mafumbo kama ndoto za usiku. Utahisi kama anatania lakini wanawake hawanaga utani kikawaida.

Ndio wakati pekee kile kiburi na jeuri yako imepungua na unahitaji kujivunia watoto wako lakini kwa bahati mbaya Mwanamke huyo anakutenga na watoto wako. Yaani unakuwa umepigwa kwa namna ambayo unabaki huelewi elewi.

Ndio wakati ambao unaugua zako kisukari ambacho unahitaji huduma nzuri hasa ya chakula lakini Mwanamke anakukumbushia wapo wapi wale wanawake uliokuwa unalala nao, hafanyi kwa weledi anafanya ilimradi. Muda wa chakula anapitiliza na ukiongea anakuambia usimpelekeshe.
Amekuvumilia vya kutosha sasa ni muda wa kukutolea uvivu.

Kipindi cha kwanza ulikuwa unaongoza kwa bao 2-0 lakini Mwanamke anakuja kurudisha kipindi cha pili na kukuongezea mabao kama yote tena yote yanakuwa mabao ya Kisigino.

Mwisho unakufa, Mwanamke anaibuka mshindi. Anapongezwa kwa mafao yako uliyokuwa unafanya kazi. Picha linakuwa limeisha. Atalia kwa huzuni na kusikitishwa na yote lakini hayo ndio maisha na lazima yaendelee.

Wito; ni vizuri unapoingia kwenye familia utende Haki, uwe mwaminifu, uwe na upendo, uwe na maarifa na akili kisha umche Mungu. Siku zote ukiwa na mambo hayo wewe ni mshindi.

Acha Nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Mama nani alisema eti tangia hizi kelele za wanawake wanawake ziwe nyingiii, matatizo ndio yameongezeka zaidi. Nikapigaaa 'hiiii' na masingo mama wanaongezeka zaidi kila siku. Hapa dadake ni singo mama, anti yake kaachika miaka karibu 20 na huko....mamake mjane.....yeye mdomo mrefu mnooo.....u knw wat? She is pleasing now for the mistakes she did last year. Hii sio ya kuchekesha. Hii ni live feed natoa hapa. Kumbe watibeli ni kama wacuba tu, akili mingi mnoo.....kama kobe taratibu sheria mkononi hapana. Akili mtu wangu. Kataa ndoaaa kwa ustawi wako na jamii kiujumla

Hatari sana
 
NI wakati ambao unaugua zako kisukari unahitaji chakula bora halafu mwanamke anakuambia wako wapi malaya zako........ duuuuh mke wangu moyoni mwako ndo uko hivyo????
 
Mwanamke kwenye JF, mwanamke Kwenye ma redio, mwanamke kwenye tv, mwanamke wa shoka, mwanamke live, mwanamke akiwezeshwa anaweza, mwanamke super woman, mwanamke kila mahali ni nini shida hasa??!! huyu mwanamke abaki kwenye nafasi yake, ni kama mnapush agenda zisizo na kichwa wala miguu, Mwanamke ataendelea kuwa mwanamke na Mwanaume ataendelea kuwa mwanaume, Hizi stori za mwanamke hivi, mwanamke vile zinachosha sasa, maana kila mahali stori ni mwanamke tu. WTF???!!!!!!!!!!!!!!!
Kaaa kwenye nafasi yako vyema wala hutochokaa na wanawake zaidi sana utawafurahia.
 
NI wakati ambao unaugua zako kisukari unahitaji chakula bora halafu mwanamke anakuambia wako wapi malaya zako........ duuuuh mke wangu moyoni mwako ndo uko hivyo????
Eeeeh kama unamtendea mambo mabaya ndo yupo hivyo moyoni😁😁😁
 
Mwanamke kwenye JF, mwanamke Kwenye ma redio, mwanamke kwenye tv, mwanamke wa shoka, mwanamke live, mwanamke akiwezeshwa anaweza, mwanamke super woman, mwanamke kila mahali ni nini shida hasa??!! huyu mwanamke abaki kwenye nafasi yake, ni kama mnapush agenda zisizo na kichwa wala miguu, Mwanamke ataendelea kuwa mwanamke na Mwanaume ataendelea kuwa mwanaume, Hizi stori za mwanamke hivi, mwanamke vile zinachosha sasa, maana kila mahali stori ni mwanamke tu. WTF???!!!!!!!!!!!!!!!
Eti wanaitangwa "malkia wa nguvu"
 
Mama nani alisema eti tangia hizi kelele za wanawake wanawake ziwe nyingiii, matatizo ndio yameongezeka zaidi. Nikapigaaa 'hiiii' na masingo mama wanaongezeka zaidi kila siku. Hapa dadake ni singo mama, anti yake kaachika miaka karibu 20 na huko....mamake mjane.....yeye mdomo mrefu mnooo.....u knw wat? She is pleasing now for the mistakes she did last year. Hii sio ya kuchekesha. Hii ni live feed natoa hapa. Kumbe watibeli ni kama wacuba tu, akili mingi mnoo.....kama kobe taratibu sheria mkononi hapana. Akili mtu wangu. Kataa ndoaaa kwa ustawi wako na jamii kiujumla
Nakuunga mkono Curtiz
 
Ni maamuzi tuu au unasababishwa ya msingi?
Nimeoa lakin nichokuja kugundua ni kuwa "Ndoa" kwa maana yake na kusudio lake ni njema, na nilioa Kadri ya mapokeo ya wazee na desturi ya jamii. Lakin kwa Karne hii ya kumpandishwa kwa mwanamke kumepelekea mwanaume kupoteza either mamlaka au nafsi yake asilia matokeo yake ndoa imepoteza maana yake na kuwa kama taasisi ya kitapeli, ambapo imepelekea ss wanaume kupungua maisha yetu ya furaha na aman ya kwel.
 
Back
Top Bottom