Wanawake wengi wameolewa ila hawawapendi waume zao kutoka moyoni

Wanawake wengi wameolewa ila hawawapendi waume zao kutoka moyoni

FANYEN FAMIĹY MAPING KABLA YA NDOA ZINASAIDIA SANA NA TOPICNILIWEKA HUMU IMEWASAIDIA WENGI SANA
 
Huo ndio uhalisia... Mume kamzidi mke gap la mika 10 na kitu unategemea nini 😂
Mkuu,tunachohitaji ni kwao ni heshima,hawanaga Upendo kwetu.Na hawa viumbe,jinsi gepu umri linavyozidi kuwa dogo,na heshima yao huwa ndogo hivyo hivyo,japokuwa mimi nashauri gepu lisizidi miaka 10++
 
Uko sahihi sana

Wanawake wengi wanalazimika tu kuingia kwenye ndoa kwa sababu ya age catching with them, kuepuka aibu kwenye jamii na uwepo wa kibunda

Sasa baadaye anaanza kuishi maisha halisi na mume. Kama material things anazoea anakuta anakosa kitu kimoja hana hisia za kweli za upendo kwa mume
 
Changamoto nyingine ni hawa wanaooa single maza

Single maza huwa hawana upendo wa kweli ni wanafiki tu

Single maza sikuzote anatafuta mwanaume mjinga mjinga wa kumbebesha zigo la kumtunza yeye na mtoto wa baby daddy wake
 
Nimeketi zangu room, sina habari, nje wameketi Mwanamke mmoja wa 1998 na mwingine wa 1979... Wote wameolewa 1998 Mume wake ni wa 1990, na wa 1979 mume wake ana miaka 70+

Huyu wa mwanamke wa 1998, mume wake ana wivu wa kupitiliza na uwa inapelekea wanakwaruzana mara kwa mara, mpaka dogo anashindwa kujaliwa mume akihisi atapendeza sana kisha kuwavutia mahalamia, ni kweli binti ana uzuri fulani hivi ila matunzo zero. Kwa upande wa bi mkubwa wa 1979 yeye ni wa kawaida na mume wake ni mzee na uwa ana pressure. Wote hawa wanawake story zao zinafanana, hani wamepitia mistrust issues na some sort of domestic violence.

Sasa niwapangaji wenzangu, mimi nimeketi zangu ndani, Bi Mkubwa wa 1979 apiga story na huyo mwanamke wa 1998, story zao wote ni kuwa hawapendi waume zao, yani wanaishi nao kinafiki tu. Huyu bibie wa 1979 mume wake ana shida ya figo na ilitolewa na ana pressure, huyo wa 1998 yeye mume wake ni mpambanaji tu na yuko fit ila kama nilivyosema ni kuwa jamaa ana wivu sana kitu kinachopelekea mke wako kuwa kama mfungwa hata sisi wapangaji wakiume tunapunguza mazoea ili tusilete kashikashi.

Yani kwa kifupi hawa wanawake wote wawili wanapiga story waziwazi, kuwa hawawapendi waume zao, wanaishi nao tu ilimradi tu. Kauli ambayo ilinitisha kidogo, yani kumbe kuna wanaume wanalea familia huku wake zao hawapendi, yani wanawake hawa wapo kwenye hizi ndoa kwa sababu fulani fulani tu ila sio mapenzi. Huyu bi mkubwa ndio mother house, na ana watoto wakiume tu na ana wajukuu ambao wapo mkoa mwingine huko, yeye anaishi na mume wake tu ambae ni mzee wa miaka 70+, anasubiri mzee akate moto tu. 😂

Jamani unaweza ukahisi mke wako anakupenda, kumbe yupo na wewe kwa sababu fulani fulani tu kama watoto, au hana namna ya kimaisha tu kwa hiyo kaamua kujistiri kwako, au angalau wewe una unafuu wa maisha au kuna sababu yoyote tu inayomfanya ishi na wewe ila moyoni mwake haupo.

NB: Ishi na hawa viumbe kwa akili sana
Unatushauri nini sisi mabachelor
 
Changamoto nyingine ni hawa wanaooa single maza

Single maza huwa hawana upendo wa kweli ni wanafiki tu

Single maza sikuzote anatafuta mwanaume mjinga mjinga wa kumbebesha zigo la kumtunza yeye na mtoto wa baby daddy wake
Ahahahah bro weka kituo basi mbona una mukari sanaaaaaaaaaaa
Ila singo mother nyoko
 
Wanawake hawapendi mwanaume mweny gubu bora asiye na pesa ukiwa na gubu basi atakuchukia tu...Kuna wanaume haswa watu wazima wanakuwa na hasirq kila siku kuangalia makosa ya wake zao.

Wanawake wanapenda mwanaume aliyekuwa serious ,sio kukaa kitu kidogo kelele haswa wazee wanapokaribia kustaafu, wanakuwa na gubu sana hata wanaume wasiokuwa na pesa hawana mishe kazi kufuatilia wake zao.

Mambo ya kumfuatilia mke kama una mshutumu sio poa ,chagua kwanza mweny tabia nzuri kabla sio kuanza kumfuatilia kama mko shule.
 
Mleta mada una hoja ya msingi ila maelezo yako yamekaaa kama umbea flan hv
 
Niliwahi kusoma mahala. Nadhani ni kwenye vitabu vya hawa washauri wa ndoa wa Naijeria kama siyo kwa Rev. Munroe.

Kwamba mwanaume zingatia sana fomyula hii unapotafuta mke:

Hakikisha mkeo ndiye anakupenda zaidi kuliko wewe unavyompenda yeye.

Sasa wewe unakurupuka unapenda usipopendwa mtu anataka tu angalau umuoe ili kumwondolea nuksi, au kafata maokoto, mbona usiishie kuona rangi zote zilizopo hapa duniani?

1. Mume akimpenda sana mkewe kuliko mke anavyompenda mumewe = mateso ya kila aina kwa mume. Ndoa itadumu tu kama mume ni mvumilivu! Mke hisia zake zitakuwa kwa mwanaume mwingine anayempenda, aliyewahi kumpenda au atakayempenda!

2. Mwanamke akimpenda sana mumewe kuliko mume anavyompenda mkewe = Shida ndogo ndogo kwa mke lakini kutokana na uvumilivu wa wanawake ndoa itadumu sana. Wanaume siyo watu wa hisia bali ni watu wanaotaka kuheshimiwa. Utii na heshima vinakuja naturally kwa mwanamke kama anampemda mumewe kikweli. Hawa wataishi vizuri tu hasa kama mwanaume anajitambua (hachukulii upendo wa kweli wa mkewe kwake for granted)

3. Mume na mke wote wakipendana sawa sawa. Hawa ni soulmates na huu ni muunganiko mtakatifu kiroho. Hawa ni nadra sana kutengana na wakiungana sawasawa ndiyo hutenda maajabu na kufanikiwa sana (power couple). Inasemekana mtu hukutana na soulmate wake mara moja tu maishani na kuna imani kwamba kwa wanawake mara nyingi ni yule mwanaume anayembikiri. Ndiyo maana eti huwa vigumu sana kwa mwanamke kumsahau mwanaume aliyeifungua ile njia ielekeayo kwenye kiini cha uhai na maisha. Na hiki ndicho chanzo cha ule usemi kwamba kama umeoa mwanamke ambaye hukumbikiri kimsingi umeoa soulmate (mke halali wa kiroho) wa mtu. Ndiyo maana migogoro haiishi katika ndoa (incompatible souls).

Kwa sasa ni hayo tu! 🚶🏿‍♂️🚶🏿‍♂️🚶🏿‍♂️

I mean no malice to nobody 🖐
 
Changamoto nyingine ni hawa wanaooa single maza

Single maza huwa hawana upendo wa kweli ni wanafiki tu

Single maza sikuzote anatafuta mwanaume mjinga mjinga wa kumbebesha zigo la kumtunza yeye na mtoto wa baby daddy wake
Vita vyako na singo mazazi sijui vitakuja kuisha lini. Sijui walikukoseaga nini masikini! 😭
 
Back
Top Bottom