Wanawake wengine wanawezaje kumaintain miili yao baada ya kujifungua?

Wanawake wengine wanawezaje kumaintain miili yao baada ya kujifungua?

mh mtu unaeza kupenda kufanya mazoezi kweli labda kama ni hobi yako aisee,,hapa nahitaji nguvu za ziada kuendelea manake vigimbi havifai,,ila sabbu ni plan ya mwka huu sina budi
Haha sana tu unajikuta unapenda ,tafuta na namba siku nyingine unaruka kamba
 
Hongera Evelyn Salt.
Umesema kwa sasa Mazoezi huwezi, njaa inakuchanganya.

Itabidi uvumilie tu hadi miezi 6, uanze kupunguza misosi, na uanze Mazoezi, nikimaanisha hutohitaji kutengeneza maziwa mengi.

Tunatofautiana genes, wengine ni rahisi ku shift the baby weight wengine ndio mpaka tujiandikishe gym.

Good luck New Mum.
ahsante sana, najua nikipunguza msosi nitapungua pia
 
Wengi wao hawanyonyeshi so probably hawali vyakula vya uzazi,,, me naona wewee piga msosi tuu na jitahidi unyonyeshe 6 month mwili usikupe shida utapungua wenyewe bila shida maana itafika Mahala mtoto ananyonya haswa then kula kawaida tuu mwili utaisha tuu
Ahsante, kumbe huwa hawanyonyeshi
 
njaa napata njaa kila dakika, na nikihisi njaa sitaki kuchelewa hata dakika, mwanzo nilijibana mwili ukawa poa tatizo Maziwa nayo ya mawazo nmeamua kula nimefumuka sipendi unene, nifanyeje nileje.
Njaa ni kawaida. Kula kiasi kidogo cha chakula kila baada ya mda mfupi. Usile chakula kingi at once
 
Pole maliza kunyonyesha mwil utarudi, au tafuta Dr mzur akushauri vyakula vya kula ili mwil ukae sawa, maana wengine tuna miili mikavu ya asili
 
Pamoja na mazoezi msosi vipi, make mie kunachoninenepesha ni msosi tu
Usipate mawazo utapungua mtoto akianza kula ila hata kwa sass ukiweza kupunguza portion ya msosi itakuwa poa njaa huwa inasumbua lakini baada ya muda tumbo litazoea. Msosi wako weka mboga nyingi kuliko starch, na between the meal kula matunda badala ya vitu vizito.Zoezi naona hutaki kabisa ila ukifanya walking kidogo basi si mbaya, ukipunguza msosi kunyonyesha tu yenyewe inasaidia sana kuburn fat. Hongera kwa baraka ya mtoto
 
duh! polee..

nachofahamu chakula bora+mazoezi ndio pekee inayoweza kukusaidia ukarudia mwili wako...ila sababu huna kipaji ya hiyo ya pili basi egemea zaidi kwenye chakula bora.
 
Mwenzio kazaa mara tano, na anajitunza mwenyewe;
zari-hassan-dangote.jpg
 
Ni aina ya mwili kwa jinsi Mungu alivyoumba, si sababu ya chakula.
Kuña wengine huonekana ni wazee wakati wana umri mdogo, na wengine huonekana vijana wakati kumbe umri wao ni mkubwa(hawazeeki upesi)
 
Kwani unakula nini? coz the more mtoto ananyonya the more utasikia njaa, na unavyovila mtoto anavimaliza kwenye maziwa, labda kama unatega kunyonyesha, lakini ukinyonyesha vizuri lazima utapungua tu.
Fanya mazoezi na uwe makini na vyakula unavyokula, maana kama unafanya mazoezi alafu ukirudi unapiga sinia na wali nyama maharage hutaka upungue tehe tehe tehe
 
Usipate mawazo utapungua mtoto akianza kula ila hata kwa sass ukiweza kupunguza portion ya msosi itakuwa poa njaa huwa inasumbua lakini baada ya muda tumbo litazoea. Msosi wako weka mboga nyingi kuliko starch, na between the meal kula matunda badala ya vitu vizito.Zoezi naona hutaki kabisa ila ukifanya walking kidogo basi si mbaya, ukipunguza msosi kunyonyesha tu yenyewe inasaidia sana kuburn fat. Hongera kwa baraka ya mtoto
mazoezi nayataka ila yenyewe hayanitaki, ahsante nitapunguza kidogo, kwakweli nakula utadhani kuli
 
Back
Top Bottom