Wanawake wenzangu mnazoeaje maumivu haya ya tumbo?

Wanawake wenzangu mnazoeaje maumivu haya ya tumbo?

Status
Not open for further replies.
mdogowangu alikuwa Kama wewe hadi tukahisi amerogwa mana kiladawa amekunywa lakini wapi.

nilipo mwozesha akaenda kuchezea rungu malalamiko yatumbo,nyonga na homa zisizo nampango zikaisha.

ilakunadawa yaasili inapunguzaga maumivu ukinywa.kama unahitaji njoo pm nikuelekeze
Sawasawa
 
nenda hosp....mara nyingi wanaoumwa sana huishia kukosa hadi mimba! unakua hupati ng'o...sisi wengine vizaz vya paka na panya hatusikii kabisa hayo maumivu..dah .zaidi ya moodswings
 
1. Pole, upate afueni mapema.

2. Huu ni mtandao, umeshahifadhi taarifa yako, kwa nia njema na mbaya kutokana na aina ya binadamu.

3. Kunaambao kuanzia leo wataanza kukubesabia kalenda, siku na mwaka ushasahau kama ulikuja hapa JF ila watakupa pole ya kuumwa na utashangaa wamejuaje.

4. Wakati ukuta, dunia inazunguka zaidi ya pia... hakuna namna zaidi ya kuenenda nayo. Kuelezea ya wakati wetu uliopita hayasaidii ila yanaleta kumbukumbu mrejesho na kupata simulizi huko nyuma watu walifanyaje kwenye nyakati kama hizi.

Simulizi......

Enzi hizo ukiwa mtoto unarukaruka na kucheza cheza utakavyo. Hasa mie niliezaliwa na watoto wa kiume tupu michezo yote ya utundu wa kiume nimecheza. Makovu kama yote, shukria mama Kasie hakuacha nipaka majani asili ya kufuta makovu.

Siku ya siku kifaa cha kukupeta na kuchambua mchele kilipovunjika sina hili wala lile nikavutwa pembeni na mama, nikaambiwa moja mbili tatu nne tano na kuendelea. Na vitisho kedekede, ukifanya ubishi na kisirani unashika mimba, mwisho na marufuku kuchezacheza barabarani na watoto wa kiume, mwisho kurukaruka kwenye miti na juu ya nyumba, mwisho kuvaa nguo zisito za staha.... nililiaaaaa maana niliupenda utoto. Nilikuwa napenda sana kuvaa vigauni vifupi, vikaptura, visketi vya kuchanua.... sasa vyote hivyo marufuku daaah....

Nilijiona nakuwa mtawa hivihivi, mbona bado mie mtoto kwanini nisiendelee kucheza...? Basi ndo nikawa mkubwa namna hivyo na tukio likija kila mwezi niliambiwa marufuku mtu kujua, ni hatari. Nilifundishwa kulinda tarehe na kalenda yangu na mambo mengine mengi ikiwemo usafi wa mwili, kuwa mpole na kuwa na aibu ya kike, kutokuongea sana, kuwa mvumilivu, usitizamane uso kwa uso na mwanaume, yaani makorokoro kibao.
Mwisho mama akanikabidhi kitabu cha mschana jitambue.... nilikitunza hiki kitabu kikajapotea nilipoenda jeshini.....😔😔.

Mara mbili tofauti kwenye uschana wangu niliwahi kuumwa nusura ya kuzimia, na hapo nilikuwa nagugumia mwenyewe simwambii yeyote. Safari moja tulikuwa kwenye kongamano la vijana, tukiwa tumekaa na waschana wengine, nilizidiwa nikajilaza pembeni kwenye majani. Kongamano lilikuwa uwanjani, nikapitiwa na usingizi mzito kuja kustuka majasho yananitoka ila maumivu yamepungua.
Mdada mmoja akaniambia polee, niliona aibu ila nikastuka kajuaje mbona sijalalamika kama naumwa..? Nikajikausha kumkatalia kuwa hapana niko kawaida tuu kumbee.....
Baada ya hapo mishahara ya mwezi ilikuwa inakuja na maumivu kiasi ya tumbo na miguu hadi nilipojaza fomu ya floo ya 5 nikarudisha bahasha ya kupokea mshahara kila mwezi.

Ila mara zote kuna sehemu za mwili zilikuwa na joto flani hivi, akitokea amelishika mwanaume na mikono yake anahama akili. Joto hilo lilikuwa maeneo ya kwenye mapaja, matiti na mgongoni.
Macho ndo ilikuwa kitambulisho kikuu kwa mtu aliyekuwa ananifatilia kila mwezi, nilikuwa msimu ukianza macho yanarembuka kuliko kawaida.

Sekondari nilisoma shule ya wasivhana watupu Korogwe, nilikuwa nachukia baadhi ya waschana utasikia naomba niangalie nikiamka kama sijachafuka......😏😏😏

Nikawa siwaelewi hawa hawajafunzwa kwao namna ya kujipanga na muda wa kubadilisha....!!!

wakati ukuta, ukipigana nao utaumia....

miaka 30 ijayo wataokuwa na miaka kuanzia 20 na kuendelea watakuwa wanashangaa namna wa miaka hii walivyoenenda.

Ndivyo ilivyo, dunia duara.

Mtanisamehe kwa kushindwa kufupisha habari.

Wasalaaamu.

Bibi Kasinde.
 
Habari ya asubuhi,

Wenzangu huwa mnazoeaje haya maumivu jamani?[emoji29][emoji29]

Yaani iko hivi, tumbo linauma kama mtu yupo tumboni anavutavuta utumbo, yaani kama yuko na kijiko anakwangua ukoko kwenye sufuria vile. Sasa ushuke chini kiuno jamani, ni kinakamaaa kama sijui nini, ukijinyoosha tu maumivu yake ni shida khaa![emoji2955][emoji2955]

Kuja sehemu nyingine huku chini ni kama sindano zinachomwa chomwa huko ndani, ni full shida yaani haaaa.[emoji24][emoji24][emoji24] Hapo bado uje kwenye matiti ni yanauma jamani,[emoji26][emoji26] yamesimaa halafu ni mekundu, yaana moto kama sijui kitu gani yaani, bra yenyewe nimepata shida kuvaa maana nikivuta tu mkanda nasikia maumivu sio ya nchi hii.

Yaani nimekunywa dawa zote unazozijua za kutuliza maumivu lakini wapi.[emoji29][emoji29] Wakasema ninywe maji ya moto ila nakaribia kumaliza chupa hapa lakini sioni dalili ya maumivu kupungua, mkojo tu unabana nikienda chooni kuchuchumaa nako tabu haaaa![emoji37][emoji37]

Yaani hapa niko ofisini siwezi kukaa, natembea tembea tu muda wote, nasubiri kila mtu aingie ofisini kwake nibebe PC yangu nikajilaze kwenye kochi la wageni pale reception. Maana nina tabu jamani kusimama muda wote, nikisema nikae yaani kama nakalia sindano haaa![emoji24][emoji24]

Wenzangu mnawezaje kuzoea, maana mimi nashindwa jamani? Sijui Mungu aliwaza nini kuniumba wa kike, naumia mwenzenu, [emoji26][emoji26][emoji26]nifanyeje eti?
Pole sana nicheki nikuambie dawa
 
Habari ya asubuhi,

Wenzangu huwa mnazoeaje haya maumivu jamani?😓😓

Yaani iko hivi, tumbo linauma kama mtu yupo tumboni anavutavuta utumbo, yaani kama yuko na kijiko anakwangua ukoko kwenye sufuria vile. Sasa ushuke chini kiuno jamani, ni kinakamaaa kama sijui nini, ukijinyoosha tu maumivu yake ni shida khaa!🤨🤨

Kuja sehemu nyingine huku chini ni kama sindano zinachomwa chomwa huko ndani, ni full shida yaani haaaa.😭😭😭 Hapo bado uje kwenye matiti ni yanauma jamani,😥😥 yamesimaa halafu ni mekundu, yaana moto kama sijui kitu gani yaani, bra yenyewe nimepata shida kuvaa maana nikivuta tu mkanda nasikia maumivu sio ya nchi hii.

Yaani nimekunywa dawa zote unazozijua za kutuliza maumivu lakini wapi.😓😓 Wakasema ninywe maji ya moto ila nakaribia kumaliza chupa hapa lakini sioni dalili ya maumivu kupungua, mkojo tu unabana nikienda chooni kuchuchumaa nako tabu haaaa!😖😖

Yaani hapa niko ofisini siwezi kukaa, natembea tembea tu muda wote, nasubiri kila mtu aingie ofisini kwake nibebe PC yangu nikajilaze kwenye kochi la wageni pale reception. Maana nina tabu jamani kusimama muda wote, nikisema nikae yaani kama nakalia sindano haaa!😭😭

Wenzangu mnawezaje kuzoea, maana mimi nashindwa jamani? Sijui Mungu aliwaza nini kuniumba wa kike, naumia mwenzenu, 😥😥😥nifanyeje eti?
Fanya mazoezi,kula mboga chungu,kunywa tangawiazi
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom