Wanawake wote ndivyo mlivyo hata mkikataa. Wanaume kuweni makini katika maamuzi yenu

Wanawake wote ndivyo mlivyo hata mkikataa. Wanaume kuweni makini katika maamuzi yenu

CONTROLA

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2019
Posts
7,001
Reaction score
23,449
Hamna mahali popote pameandikwa mwanamke utakae zaa nae ndio unatakiwa umuoe awe mke waako wa ndoa"hakuna".

Ila pia hakuna mahali pameandikwa kwamba mwanamke utakae mzalisha usimpende wala usimpe huduma zote muhimu "hakuna"

Mwanaume unaweza kuwa ulishawahi kuwa na mtoto kwa mwanamke ambae si mkeo kwa sasa so kutokana na kujitambua kwako ukaona uendelee kutoa huduma zote za muhimu kwa mwanao kwasababu unajua fika ile ni damu yako,na hakuna mwingine wa kufanya hivyo zaidi yako.

Bahati nzuri ni kwamba mama mtoto wako (yule x) Anaolewa na mwanaume mwingine na Maisha yao kiuchumi si mazuri. Hata wewe umeona,unaamua kumwomba mama mtoto wako (yule x) umchukue mtoto ili asiteseke unamleta mwanao. Kuja kulelewa na mkeo nyumbani (makosa makubwa sana haya)

Acha nikwambie kitu,

Mkeo hatakwambia simtaki huyo mtoto (ila moyoni mwake kashakwambia)

Mkeo hatokwambia hapendi hata kumuona huyo mtoto (ila moyoni mwake jua hampendi)

Mwanaume wewe unamleta mwanao ukiamini atapata upendo kama wa kwa mama yake (unajidanganya)

Hata kama mama mtoto wako (yule x) utamuona anapitia maisha magumu kwa asilimia 200 usije thubutu mpokonya mtoto. Uje umlete kwa huyu mkeo ulie nae,Pamoja na shida atakazopitia mama mtoto wako (yule x) hatoruhusu shida zile zimpate

Mwanae na hata kama zikimpata mwanao mama yake atajua jinsi ya kumpa maneno mazuri ya kumbembeleza ajione naye yupo kawaida. Wanaume nataka tu muelewe jambo 1 hao wanawake mliowaoa (anakupenda wewe tu) usije jidanganya atampenda.

Mtu mwingine tofauti na wewe na wanae wa kuwazaa. Jitahidi uwezavyo kama una mtoto nnje na ulikua na mpango mwakani (umchukue uje uishi nae), acha maana unamleta jehanam mtoto wako mwenyewe (usijipe moyo kwa matendo yanayofanywa na mkeo ukiwepo) acha huo ujinga.

Muache mtoto wako huko huko kwa mama ake kama ni matumizi mtunze akiwa huko huko kwa mama ake. Kama unahisi unampenda sana huyo mwanao hutaki ateseke (mrudie mama yake muoe). Sasa jitie kichwa ngumu (mletee mkeo mtoto wa mwanamke mwenzie) utaona what next.

Wanawake ndivyoo hivyo walivyo, waelewe then ishi nao kwa akili mingi mingi.



1430924876step-5.gif
 
Kuna wanawake ni watesaji sana, mtoto anafinywa mashavu, anavutwa masikio kisa siyo wa kwake. ni shida sana...
ila BABA ukirudi nyumbani mtoto huyo huyo aliekua akifinywa mashavu ukiwa haupo

utamuona mama (mkeo) akimuita na kujifanya anampakata na kujitia anamdekeza (basi hapo mwanaume unaona yeees)

Kumbe zote zuga tu, ukiondoka kazini mambo ni yale yale.

Ni basi tu watoto hawawezi kusema kwa kuogopa vitisho alivyopewa (ole wako baba ako akija nikuone fyoko fyoko fyoko)
 
Thaq mnk nilikuwaa kwenye mpango wa kumchukuwa mwanangu ila imegonga mwamba acha nimlee akiwaa kwa mam ake ...
usijaribu na mshukuru Mungu kwa kusaaidia mipango igonge mwamba

Mlee mwanao huko huko akiwa kwa mama ake.
 
Unamwogopa mwanamke unayeishi naye ndani, unamwamini mwanamme mwingine aliyemuoa huyo ex akulelee mwanao nawe unakenua kwa amani kabisa.... huwezi kuwa sawa kichwani kuna namna dishi limecheza tu.
Kasema unamlea akiwa kwa mama yake, kwani nini kinashindikana hapo vitu vingine ukiwa na pesa wala havisumbui
 
Back
Top Bottom